Khitma ya Mzee Abeid Karume

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akijumuka na Viongozi mbalimbali wa Serikali na Chama katika Hitma ya Marehemu Mzee Karume iliofanyika ukumbi wa Afisi Kuu ya CCM.

Wananchi mbali mbali wakiongozwa na Dk Ali Mohammed Shein jana wameshiriki katika khitma na dua malumu ya kumuombea Marehemu Abeid Amani karume aliyeuawa Aprili 7 hapo katika ofisi ya Kisiwandui Mjini Zanzibar. Marehemu Karume alikuwa ni muasisi za taifa la Zanzibar wakati huo ambapo mwaka 1972 majira ya saa 12 00 jioni huko katika ofisi iliyokuwa Makao makuu ya chama cha Afro Shirazi Pati (ASP) Kisiwandui Mjini Zanzibar alipigwa risasi na kupoteza maisha.

Madhimisho hayo hufanyika kila mwaka ikiwa ni hatua moja ya kumkumbuka muasisi huyo na kuwashirikisha watu wa madhehebu mbali mbali katika dua hiyo.

Akiongoza dua hiyo Alhadi Musa Salum kutoka Dar Salaam alisema ni muhimu watu wakajitayarisha katika mauti kwani kila mmoja ataonya mauti kwa hali yeyote na kusikistiza mauti yanaweza kutolewa na yeyote hasa wakati mwengine mtu anaweza kupoteza maisha yake na chanzo kikawa ni mpenzi wake lakini jambo la kuzingatia ni kwamba mauti hayo yameshaandikwa yakufike.

Alisema mauti ni suala la ubadilishaji wa mazingira kutoka katika maisha, uhai unahamia katika hali nyengine ambayo ni maisha ya akhera na kuwahimiza watu kutenda mema ili wanaporudi kwa Mola wao wawe tayari wamejitayarisha katika kutenda mema kwani kifo ni mazingatio makubwa ya kuyakumbuka mauti.

Father Cosmas Shayo wa Kanisa la Katoliki la Minara Miwili alisema wananchi wanafaa kuendeleza mazuri aliyoyafanya Mzee Karume kwani alikuwa na nia ya dhati ya kuiendeleza nchi yake kimaendeleo na hivyo kumuombea Mungu amsamehe makosa yake huko alipo.

Akizungumza katika hafla hiyo watoto wa marehemu wa Karume, Ali na Amani Karume wote kwa pamoja walisema kuna mengi ya kuigwa yaliowachwa na marehemu baba yao na kuwataka wazanzibari kuyaendeleza yale mema yote aliyotaanzisha.

Alisema leo ni fakhari kubwa kwamba Mzee wao ameshafariki lakini Zanzibar hivi asa ina serikali ya umoja wa kitaifa jambo ambalo Mzee Karume alikuwa akilipigia kelele sana na kuondosha ubaguzi kwa watu wote na kuweka misingi imara ya kiutawala.

Akizungumza baada ya kumbukumbu hiyo Makongoro Nyerere aliungana na watoto wa marehemu kusema kwamba misingi iliyowekwa na waasisi wa mataifa hayo mawili yanapaswa kuendelezwa kwani walikuwa na nia njema ya kuendeleza nchi hizo na ndio maana wakaungana kwa pamoja ili kutetea haki za wanyonge na kuondosha ubaguzi.

Vyama vya siasa navyo vimetoa taarifa kwa vyombo vya habari ambapo Chama Cha Wananchi (CUF) kimesema Mzee Karume wakati wa uhai wake alikuwa mwanamapinduzi hodari, mpenda mabadiliko, aliyejitolea kwa hali na mali katika kutetea maslahi na maendeleo ya Zanzibar na wananchi wake kwa ujumla hivyo kuna kila sababu ya wazanzibari kumuenzi na kumkumbuka kwa mema yake.

“Mzee Karume alikufa kishujaa, la msingi wakati huu wa kumbukumbu yake, ni kuendeleza ushujaa wake na mema yote aliyopigania katika kuyafikia maendeleo ya kweli ndani ya visiwa hivi vya Unguja na Pemba” alisema taarifa hiyo iliyosainiwa na Salim Bimani, Mkurugenzi wa Habari Haki za Binadamu Uenezi na Mawasiliano ya Umma.

Taarifa hiyo imesema itakuwa ni masikitiko makubwa kwa mustakabali wa Zanzibar na wananchi wake iwapo hapatakuwa na hima ya makusudi ya kulinda na kuenzi juhudi za viongozi waasisi, chini ya uongozi imara wa marehemu Mzee Karume ambaye alikuwa ni mkombozi wa wa wanyonge.

Naibu katibu mkuu wa chama cha NLD, Khamis Haji Muusa alisema katika taarifa ya chama hicho kwa waandishi wa habari kwamba Mzee Karume alikuwa na upeo mkubwa wa kuona mbali na ndio maana mambo mengi ya kimaendeleo aliyaanzisha wakati wa uhai wake kuliko hata nchi nyengine za afrika.

Alisema Marehemu Karume alikuwa ni mfano wa kuigwa na kwamba viongozi wate visiwani wanapaswa kumuenzi kwa kuyakumbuka mema yote aliyotenda na kusababisha Zanzibar kupiga hatua kubwa kimaendeleo kuliko nchi nyengine zote za Afrika mashariki na kusini mwa jangwa la Sahara.

Viongozi waliohudhuria katika shughuli hiyo ni pamoja na Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi, Makamu wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mohammed Gharib Bilal, rais mstaafu Zanzibar, Amani Abeid Karume, Makamo wa kwanza wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamadi na Makamo wa pili wa rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idd.

Wengine ni Spika wa Baraza la wawakilishi Pandu Ameir Kificho, mawaziri na manaibu mawaziri, viongozi wa vyama vya siasa na wananchi mbali mbali.

Advertisements

4 responses to “Khitma ya Mzee Abeid Karume

  1. NYERERE NDIE ALIYESABABISHA KIFO CHA KARUME ILI AIFANYE ZANZIBAR KUWA KOLONI LA TANGANYIKA. MUNGU AMUEKE NYERERE MAHALA PABAYA MOTONI – AMEEN. Wazanzibar hatuutaki muungano na makafiri wa TANGANYIKA.

  2. Baada kumshukuru Allah, Naomba Allah alimpe kila lenye kheri almar-hum Karume huko aliko.
    Na sisi waislam wa Znz tunatakiwa tujikaze tuikomboe nchi yetu tuwache uvivu.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s