TUME YA MABADILIKO YA KATIBA

Rais Kikwete akitangaza majina ya wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba leo. Katika hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam katika hafla iliyoshuhudia ni Makamu wa Rais Dkt Mohamed Gharib Bilal, Waziri Mkuu Mizengo Pinda, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Iddi na Waziri wa Sheria na Katiba Mama Celina Kombani na badhi ya wahariri wa vyombo vya habari mbali mbali.

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete leo ametangaza rasmi majina ya wajumbe walioteuliwa katika Tume ya Mabadiliko ya Katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Rais Kikwete ameyataja majina hayo mbele ya wahariri wa vyombo mbali mbali vya habari huko Ikulu Jijini Dar es Salaam. Tume ya mabadiliko ya Katiba. Tume hiyo aliyoitangaza leo, Rais Kikwete alisisitiza kwamba kuanza kazi itatangazwa rasmi mara baada ya wajumbe wote kujulishwa uteuzi wao na baadae kuapishwa. Ila kisheria tume inatakiwa iwe imekamilisha kazi ndani ya miezi 18

 

TUME YA MABADILIKO YA KATIBA

(Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Sura 83,

Toleo la 2012, Vifungu 5, 6 na 7)

______________________________

UONGOZI WA JUU

1.

Mhe. Jaji Joseph Sinde WARIOBA

– Mwenyekiti

2.

Mhe. Jaji Mkuu Mstaafu, Augustino

RAMADHANI

– Makamu Mwenyekiti

WAJUMBE KUTOKA TANZANIA – BARA

1.

Prof. Mwesiga L. BAREGU

2.

Nd. Riziki Shahari MNGWALI

3.

Dr. Edmund Adrian Sengodo MVUNGI

4.

Nd. Richard Shadrack LYIMO

5.

Nd. John J. NKOLO

6.

Alhaj Said EL- MAAMRY

7.

Nd. Jesca Sydney MKUCHU

8.

Prof. Palamagamba J. KABUDI

9.

Nd. Humphrey POLEPOLE

10.

Nd. Yahya MSULWA

11.

Nd. Esther P. MKWIZU

12.

Nd. Maria Malingumu KASHONDA

13.

Mhe. Al-Shaymaa J. KWEGYIR (Mb)

14.

Nd. Mwantumu Jasmine MALALE

15.

Nd. Joseph BUTIKU

WAJUMBE KUTOKA TANZANIA – ZANZIBAR

1.

Dkt. Salim Ahmed SALIM

2.

Nd. Fatma Said ALI

3.

Nd. Omar Sheha MUSSA

4.

Mhe. Raya Suleiman HAMAD

5.

Nd. Awadh Ali SAID

6.

Nd. Ussi Khamis HAJI

7.

Nd. Salma MAOULIDI

8.

Nd. Nassor Khamis MOHAMMED

9.

Nd. Simai Mohamed SAID

10.

Nd. Muhammed Yussuf MSHAMBA

11.

Nd. Kibibi Mwinyi HASSAN

12.

Nd. Suleiman Omar ALI

13.

Nd. Salama Kombo AHMED

14.

Nd. Abubakar Mohammed ALI

15.

Nd. Ally Abdullah Ally SALEH

UONGOZI WA SEKRETARIETI

1.

Nd. Assaa Ahmad RASHID

– Katibu

2.

Nd. Casmir Sumba KYUKI

– Naibu Katibu

Advertisements

21 responses to “TUME YA MABADILIKO YA KATIBA

 1. AT LEAST IT SOUNDS PALLATABLE. WISH ALL THE BEST FOR THE INTEREST OF ZANZIBAR AND ZANZIBARIS. i’M CONFIDENT WITH THOSE PEOPLE ON BOARD ” ZANZIBAR WILL BE FREE ONCE AGAIN AFTER ALLMOST 48 YEARS OF TANGANYIKA DOMINATION” GOD BLESS ZANZIBAR AND ITS PEOPLE.

  • I am not especially on Zanzibar side and the Chairman Warioba, who was nominated to safeguard the interest of the ideology of Nyereism. Remember Warioba was against even the establishment of Zanzibar national flag. He was the one who came with the idea of inscrpting Union flag at the corner of Zanzibar flag. meaning Zanzibar is Tanzania(Tanganyika) colony.

   But the most dangerous man in the committee is Salim Mohammed Salim. He has no heart about Zanzibar and he is after one government. Let wait and see but we are finished

 2. ee mwaya mbona umewacha nafasi kubwa? au copy and paste?

  Happy Birthday, umekuwa mkubwa una miaka mingapi?

  Salma Khamis/

 3. Katika tathmini yangu, naona wazi kuwa tumepata nafasi ya kujisemea. Sasa kazi ianze na tuwe makini kwa tunachokitaka. Nimefurahi sana kuwaona baadhi ya watu fulani ndani kwani wengine wengi tumeusikia msimamo wao na hisia zaao juu ya zanzibar. Tuweni na mshikamano mmoja.

 4. Ehh nnyinyi mnafurahi, hamwajuwi watanganyika nyinyi. Mimi bado nna msimamo wa UAMSHO, Tume hii mwisho Chumbe…

  • Nakuunga mkono mia kwa mia. Wajumbe wenyewe. Mwenyekiti ni adui mkubwa wa Zanzibar na tunamjua na naibu wake ni mdini tu na ni yule alihusika na kuanddaa ule waraka wa makanisa kabla ya uchaguzi na kiongozi kidete wa kuusamabaza ukiristo Zanzibar.

   Ahmed Salim ambaye anaichukia Zanzibar kiasi kuwa hata nyumba Zanzibar hana na pamoja na kuishi Dar karibu sana na Zanzibar hupita miongo ndio atembee na hufikia hoteli
   Fatuma Said Ali pamoja na kuolewa bara hana mlahaka wa kisiasa na watu wa Zanzibar. Lake tumbo. Hafai kuiwakilisha Zanzibar

 5. Tumeanza alichokifanya Rais Kikwete ni kutangaza tume, sasa ni juu ya watu wote kujipanga kutoa maoni wanayohisi ni matakwa na mahitajio yao, sauti ya umma ikiwa kubwa tume haiwezi kubadilisha ukweli, naelewa sio watu wote waliomo kwenye tume kama ndio wale ambao watu wote wanawataka lakini wamo wanaoridhiwa na wengi na kweli ni watu bora.
  Tuwe makini hii ndio hatma ya miaka zaidi ya khamsini ya maisha yetu tumelia sana na tuliihitaji fursa hii kila sekunde ilipowadia, tuitumieni naelewa zipo changamoto nyingi kama Watanzania na Wazanzibar.

  Mungu ibariki Zanzibar na Tanzania.

  • @Massoud
   No no no no no no no no no no more Tanzania here.
   we are looking how to establish our NATION, Republic of Zanzibar.
   Ungana na UAMSHO ktk harakati za kuvunja muungano.
   Allah ibariki Zanzibar na watu wake.

 6. Waznzbari kwishaaa, Subirini kunyongwa na huku mkijiona furahini hivyo hivyo, Uamsho ni solution ya matatizo.

  Kikwete Tume yako mwisho Chumbe.

 7. Wazanzibar huu si wakati wa kufurahi wala kuhamaki wal kuwa na jazba ni wakati wa kuwa makini mno! Naanza kwenye uwongozi wa juu m/kiti na mwenza zanzibar haijawakilishwa ipasavyo! Huyu jaji Augostino Ramadhani ni nani kwa wazanzibari? Jee ni balozi mwema kwa wazanzibar. Tukiangalia wajumbe wengi wao kwa upande wangu sijui Cv zao. Ukitoa Awadh Ali Said ambaye msimamo wake uko wazi kwa znz hawa wengine ni watu maslah tu. Tanbihi kama mzanzibar nahisi jamii inahitaji kuiangalia tume hii kwa umakini hapana kulala hadi kieleweke!. Maoni ya ujumla kwanini wenyeviti wote wawili wawe wakiristo? Kwani hakuna muislamu awezaye kaz hii? Kuteuliwa Awadh kuna lengo za kuzuwia harakati za uamsho na vijana wa umoja wa kitaifa! AMKA Mzanzibar! Funua macho wajanja hawalali!

 8. mbona zanzibar katuekea dokta mmoja tu.
  Wao wamejiekea maprofesa na madokta.
  Tume ipo kisiasa zaidi, wajumbe wengi ni kutoka CCM hao, kwani ccm huu muungano wao peke yao?

 9. Tunamshukuru Mungu kwa kuunda timu hii, ninaamini kuwa watafanya kazi nzuri. Ushauri wangu kwa Wanzibar, tueni maoni yetu. Lakini nimeogopa suala la mtu aliyetoa maoni kuwa mwenyekiti na makomu wake ni wakristo. Kwanza ni haki yake kusema, lakini ana ajenda gani. Ni % ya waislamu katika tume hii? Je hakuna mkristo hata mmoja Zanzibar kama wajumbe?, nadhani ni vizuri kuafakari kabla ya kusema.

 10. kikwete ana nia ya kutumaliza wazanzibari.
  Tume iyo mimi binafsi sjaiwafik, kwa sababu kwanza imejaa ccm watupu, pili japokua wamo wazanzibari lakini hao wote wapo kwa ajili ya kujaza matumbo yao, na tatu hao jamaa inaonekana wamezaliwa tu zanzibar hawana uchungu ata kidogo na zanzibar.
  Shime wazanzibari wenzangu tuamke, siasa za kijinga tuachane nazo.
  Hawa jamaa wametudhamiria kuendelea kututawala, kutudhalilisha na kutukandamiza katika nyanja zote zikiwemo maadili, elimu na uchumi.
  Tukilifumbia macho jambo hili mjue ndo tumekwisha.
  Wabunge, wawakilishi na viongozi waliomo kwenye serikali zote 2 ambao ni wazanzibari hawaumii kwa haya tunayoyalilia bali wao ndo wanayapalilia halafu wanatujejea.
  Tufanye kitu kieleweke wazanzibari.

 11. A’alaykum Allah awape nguvu uamsho wafanye kazi ya Allah kwani kupigania nchi ni jihad. Na sisi tupo nyuma yao insha Allah.

 12. Hili Tume wala siliamini.
  Subiri niangalie kongamano la Bwawani na mhadhara wa Alabana, nitarudi baadae.

 13. BARUA YA WAZI KWA MH.WAZIRI WA SHERIA NA KATIBA TAIFA –
  WAZIRI WA SHERIA NA KATIBA –TAIFA, NDUGU:YAH,MAONI NA MAPENDEKEZO JUU YA MABADILIKO YA KATIBA HAPA NCHINI KWA MSWADA UNAOENDELEA KUJADILIWA KITAIFA HIVI SASA NA ULIOANDALIWA KWA AJILI YA KUIUNDA NA KUITAYARISHA TANZANIA MPYA KWA USITAWI WA WATANZANIA.
  Tafadhari rejea kichwa cha barua cha hapo juu,
  Ninayo heshima tukufu na thamani kubwa kwako,pamoja na furaha kubwa sana kukuandikia barua hii yenye mambo ya msingi ambayo mimi kama mdau wa maendeleo hapa nchini ningependa yachunguzwe na kutazamwa kwa umakini wakati wa zoezi zima la uundwaji wa katiba mpya hapa nchini ambalo ndilo tegemeo la kuwaletea watanzania mabadiliko na maendeleo, pamoja na utaifa wa kweli. kufanya hivyo ni kutekeleza wajibu na haki ya kushiriki kwa namna moja au nyingine katika zoezi zima la uundaji wa katiba mpya kwa maendeleo ya taifa. Ombi hili kwako linazingatia misingi ya haki ya kikatiba inayompa kila mwananchi nafasi ya kutoa maoni,na kujadili mustakabali wa maisha yake pasipo kuvunja sheria za jamii husika na zile za jamhuri ya muungano wa Tanzania,Nimeona ni busara ya wazi kutoa mapendekezo yangu juu ya mswada huu wa katiba mpya ili kuonesha ushiriki wangu katika zoezi hilo na kupendekeza mambo muhimu katika ujenzi wa katiba kwa ajiri ya manufaa ya kizazi cha leo na kesho.Nimezingatia kifungu namba 18-sheria za jamhuri ya muungano wa tanzania.
  Baadhi ya mambo ambayo napendekeza kujadiliwa pamoja na;
  1.Dhana halisi ya katiba, 2.Mambo ya msingi katika katiba yoyote ile, 3.Mambo ya msingi katika katiba kama chombo kinachoonesha mfumo wa serikali au utawala katika Taifa lolote duniani, 4.Mambo ya msingi katika katiba ya nchi zilizo endelea, 5.Mambo ya msingi kuwepo katika katiba ya nchi zinazoendelea, kama Tanzania 6.Mambo muhimu ya kuzingatia katika kujadili muundo wa katiba ya nchi mbili zilizo ungana, kama Tanganyika na Zanzibar, 7.Mambo muhimu ya kuangalia wakati tunajadili muundo wa katiba katika nchi iliyojiunga katika shirikisho la Afrika ya mashariki( EAST AFRICAN FEDERATION), 8.Mambo muhimu kuangaliwa katika muundo wa katiba ya nchi iliyo katika mfumo wa nchi iliyojikita katika siasa isiyofungamana na mfumo wa dini yoyote ile, wala upande wowote, 9. mambo ya msingi kuwepo wazi katika katiba ya nchi yenye mfumo wa utawala wa kidemokrasia,na 10.Uhusiano wa uchumi wa taifa na katiba inayoundwa liangaliwe kwa umakini mkubwa.
  Ukifuatilia katiba za nchi yoyote inayosonga mbele kimaendeleo-utagundua kuwa mambo hayo yalizingatiwa-fuatilia katiba ya nchi ya AFRIKA YA KUSINI-(SOUTH AFRIKA.).Na hata mataifa mengine ya ulaya kama Marekani-hasa kipindi cha kufufua uchumi ili nchi ijitegemee.Hao walizingatia mambo kama hayo tuliyoyabainisha. Yote haya yakitazamwa kwa uyakinifu ndipo tuanze kujadili juu ya katiba iliyopo Tanzania na kuchambua kwa undani juu ya mapungufu ya katiba hii,baadaye tutajadili juu ya muswada na muundo wa katiba mpya ya Tanzania,likiwemo suala la muungano, umuhimu wake na jinsi ya kuulinda.
  Mambo mengine ya msingi ni mfumo wa serikali,utawala, pamoja na mamlaka ya Rais,Bunge na Mahakama katika katiba.Tjadili juu ya kuwepo au kutokuwepo kwa wakuu wa mikoa,wakuu wa wilaya, umiliki na haki ya kupewa nyumba na hifadhi kwa mtumishi yeyote wa umma, makatibu tawala na majukumu yao,suala la ushirikiswaji wa wananchi kutunga sera na kutoa maoni yao(mbunge asiruhusiwe kuingia kwenye mkutano wa bunge kabla hajaenda kukusanya maoni juu ya kero za wananchi katika jimbo lake,kigezo cha elimu kwa mtu kuchaguliwa kuwa mbunge ni jambo la muhimu(ni kutokana na unyeti wa kazi wanayoifanya wabunge kuwa inahitaji taaluma ya kutosha juu ya mambo muhimu ya kijamii,kisiasa na kiuchumi kwa ustawi wa jamii),idadi ya mawaziri iwe wazi ,sio kila rais anachagua mawaziri kulingana na busara zake,pia mawaziri wasichaguliwe kutoka miongoni mwa wabunge,ioneshwe wazi kiongozi akitumia madaraka ovyo juu ya hatua za kumchukulia,mawaziri washitakiwe kama watu wengine (hakuna kiongozi kuwa juu ya sheria),muda wa chama kutawala ujulikane,Pia suala la haki ya mfanyakazi wa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kujulikana wazi kikatiba ni jambo la msingi sana. Maombi haya natumaini yamekidhi na kufuata taratibu na sheria za nchi ya Tanzania, hayana dalili yoyote ya kuvuruga amani ya watu hapa nchini, ila ni sehemu tu ya kutimiza wajibu wa kuisaidia serikali kupata maoni na michango bora juu ya uundaji wa katiba itakayo kidhi mahitaji ya kila mtanzania aliyezaliwa katika nchi hii tajiri hapa Afrika na duniani kote.
  Kwa mswada huo ninaamini kwa dhati kuwa maombi hayo yatapewa nafasi ya pekee kutokana na unyeti wake kwa ajiri ya kuleta maedeleo ya Taifa letu.
  Mwisho ninakutakia utekelezaji mwema wa majukumu ya serikali na taifa.
  Imeandaliwa na mwanafunzi wa Sayansi ya Siasa, lugha na utawala- Duce.
  Emanuel Thobias(mwalyego G.T)
  Email,thobiasmwalyego@yahoo.com
  Call,0764524811/0786050406.
  15/04/2011

 14. Nawaonea huruma sana wazanzibari kwa maoni yao kwenye ukurasa huu. sasa mmepewa nafasi ya kuvunja muungano. FANYENI HIVYO KWA KUTOA HOJA ZENU. Acheni maneno ya kijinga. Kwani mkijitoa kwenye muungano mtapata cha zaidi nini. Kwa jinsi hulka za watu wa visiwani walivyo kujitenga na watanzania bara ni mwanzo wa dhiki kuu iliyokuwepo wakati ule wa ukoloni. hakuna la zaidi. hakuna sababu ya kuwatukana wajumbe wa tume. kinachofanya muwatukane ni wivu tu mioyoni mwenu kwamba kwa nini wewe hujachaguliwa. Kama mtu ni mwelewa jambo la kwanza ni kumpa ushirikiano yule aliyepewa majukumu halafu baadaye umhukumu kulingana na atakachokitenda kama ni tofauti na matarajio yaliyotazamiwa. Kwamba Warioba anasambaza ukiristo zanziba inaonesha wazi kuwa mzanzibari huyu anawaza ukiristo na hana uwezo wa kuchambua mambo kiyakinifu. ongeza bidii kujitambua mzanzibari punguza udini na ujima.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s