Mswada wa utalii wapita kwa tabu

Mswada wa sheria ya utalii jana umepita kwa tabu baada ya wajumbe kutofautiana juu ya mswada huo kuhusu suala la upendelezo la ajira kwa wazanzibari.Wakati wajumbe wasiokuwa mawaziri backbenchers wakitaka ajira katika sekta ya utalii ibaki kuwa ya wazanzibari kisheria, mawaziri wengi walitaka pendekezo la serikali kuwa ni ajira iwe ni ya mtanzania. Wakishangia mswada wa marekebisho ya sheria ya utalii ambao uliwasilishwa na waziri wa habari, utalii, utamaduni na mcihezo, Abdillahi Jihad Hassan ilibidi upite kwa kura kutokana na wajumbe hao kutokukubaliana katika kifungu hicgo kinachosomeka kuwa.

“Kifungu cha 23 b. (3) mtu yeyote anayefanya biashara ya utalii aliyeajiri mtu ambaye sio Mtanzania kutoa huduma iliyoelezwa chini ya kifungu cha (1) cha kifungu hiki lazima apate ruhusa ya maandishi kutoka kwa waziri baada ya kumthibitishia waziri kuwa hakuna mtu wa ndani (Zanzibar) wa kujaza nafasi hiyo.”

Kambi ya wajumbe wasio na wizara wakiongozwa na Mwakilishi wa Jimbo la Mji Mkongwe Ismail Jussa walitaka kifungu hicho kiwe na jina la mzanziabri badala ya mtanzania ili kutoa upendeleo maalumu kwa wazanzibari.

Waziri wa Habari, Utalii, Utamaduni na Michezo Abdillahi Jihad Hassan, Waziri wa Sheria na Katiba, Abubakar Khamis Bakari na Mwanasheria Mkuu Othman Masoud Othman wote kwa pamoja walitoa maelezo kwamba licha ya wao kutaka wazanzibari wawe na upendeleo katika sheria hiyo inayojadiliwa lakini sheria ya kazi inatamka neno mtanzania kwa hivyo kuwa na sheria nyengine inayotamka mzanzibari ni kuleta mgongano wa kisheria.

Mwanasheria Mkuu alikwenda mbali zaidi na kuelezea kuwa hali hiyo inaweza ikasababisha Tanzania bara wakatunga sheria ambayo itadhibiti wazanzibari na kwamba hivi sasa nchi za jumuiya ya Afrika Mashariki ambayo Zanzibar ni sehemu yake zinaelekea katia soko huria.

“Mheshimiwa Mwenyekiti sio kama hatutaki ibakie Zanzibar lakini kuwa na sheria mbili tofauti inaweza kuleta matatizo na sio lazima kuwa na sheria katika utekelezaji wake” alisema mwanasheria huyo.

Hali hiyo iliwalazimu wajumbe hao chini ya Mwenyekiti, Mgeni Hassan Juma aliyekuwa akiongoza kikao hicho kupiga kura ambapo wajumbe 47 waliokuwemo wakati huo walipiga kura ya ndio (Mtanzania) na hapana (Mzanzibari).

Baada ya kupiga kura kwa kuinua mikono wajumbe 40 wakatoka sare kwa wajumbe 20 kuunga mkono na wajumbe 20 kukataa na kupelekea mwenyekiti kuamua kuitisha tena kura kwa njia ya wajumbe kuitwa majina mmoja mmoja, ambapo wajumbe wengine saba kuongezeka.

Matokeo ya mwisho yaliosomwa na Katibu wa Baraza hilo, Yahya Khamis Hamad yaliipa ushindi upande wa serikali kwa wajumbe 22 kuunga mkono na 21 kukataa ambapo, wajumbe wawili waliharibu kura zao na wawili kuamua kukaa kimya.

Wakati wa kuchangia mswada huo wajumbe wengi walisema kwamba ajira nyingi zimechukuwa na wageni katika mahoteli na kuwanyima haki wazanzibari fursa ya kufanya kazi hata zile ndogo ndogo na kutaka serikali iweke sheria kali ya kudhibiti hali hiyo.

Mwakilishi wa Jimbo la Kitope (CCM) Makame Mshimba Mbarouk alitoa mfano wa Dubai na nchi za Ulaya ambapo ni vigumu kupata ajira kwa mtu asiyekuwa raia na kwamba serikali ya Zanzibar imekosa udhibiti hata vitambulisho vya mzanzibari vinapatikana kwa wageni kutoka nje ya Tanzania.

Alisema wageni kutoka nje ya Tanzania wamekuwa wakipewa vitambulisho vya mzanzibari mkaazi (ZANID) na kuvitumia vibaya vitambulisho hivyo mahotelini kwa kufanyia uhalifu jambo ambalo bado serikali imekaa kimya kuhusiana na suala hilo licha ya kuwa mara kwa mara matukio ya kihalifu kuripotiwa katika vyombo vya habari na polisi.

“Wageni kutoka Kenya wana vitambulisho vya mzanzibari wakati wananchi wa kitope katika jimbo langu watu wa makunduchi wanalilia vitambulisho hawapewi leo anakuja mgeni kutoka mbali napewa kitambusliho na anafanya kazi…wageni hawa watakuja kutuponza maana uhalifu umezidi sana kila siku utasikia huyu kanyongwa, huyo kapigwa, huyu kachinjwa” alisema kwa hasira mwakilishi huyo.

Naye Mwakilishi wa Mji Mkongwe (CUF) Ismail Jussa alisema hata nchi za zilizoendelea zimeweka sheria kama hizo za kuwapa kipaumbele wananchi wake kufanya kazi kabla ya kuwapa wageni hivyo sio aibu kwa Zanzibar kuweka kiengele kinachomtambulisha mzanzibari katika ajira.

Jussa alisema haoni sababu yoyote ya serikali kukataa kuweka neno mzanzibari badala ya mtanzania hasa kwa kuzingatia suala hilo halileti mgongano wa kisheria kwa kuwa serikali ina haki ya kutunga sheria zake bila ya kuingiliwa na lolote.

Wakichangia mswada huo baadhi ya wajumbe walitishia sekta ya utalii ifutwe kutokana na kuendelea kuharibu maadili ya mzanzibari na kutafuta vyanzo vyengine vya mapato ya nchi kuliko kuharibu maadili ya nchi.

Walisema wamesema maadili ya mzanzibari yamepotea kabisa kutokana na sekta ya utalii kuachwa bila ya kushughulikiwa na kuwekewa mipango madhubuti ya kuweza kuendeleza utalii wenye kufuata mila, silka na utamaduni wa mzanzibari.

Baada ya kupitishwa mswada huo kwa kura Mwenyekiti wa baraza la wawakilishi ameakhirisha kikao hicho hadi jumanne baada ya kumalizika sherehe za pasaka.

4 responses to “Mswada wa utalii wapita kwa tabu

 1. Wawakilishi wafuatao mwisho wao ni 215, hawa hawana tofauti na Hamad Rashid wa wawi, na wanajali matumbo yao tu:-
  1. Abubakar Khamis : Huyu jamaaa siwakumuamini hata dakika moja, hana tofauti na Shamhuna na huyu kama Maalim Seif hatomchukulia hatua sisi hatuna imani naye kabisaa, alikuwa na msimamo mzuri ktk katiba baadaeghafla akabadilika tupata khabari kapewa fupa lililonona ndio maaana kanyamaza.
  Waznzbari ktk suala zima la katiba tusitegemee lolote jema kutoka kwa mwanaharamu huyu, ataiuza Znzbar kama Shamhuna alivofanya.
  2.Hamad Masoud: Fisadu mkubwa huyu, yaani hawa watu baaada tu ya kupata madaraka wamekuwa kama si Waznzbari tena wamekuwa Watanganyika, wanatuaibisha hiv hiv ndani ya baraza, Wallahi Mungu atawalaaani nyinyi.
  3.Juma Duni: Huyu jamaaa ni mkimya lakini khabari zake na udhaifu wake tumeuona jana na tukajua kama hatuna wawakilishi tuna watu wenye kujali matumbo yao.
  4.Mazrui: Hahahahaha… Eti mapembe baasi muhuni mmmoja huyu, yaaani hata haya hana anatubwaga hiv hiv waznzbari anathamini zaidi Watanganyika kuliko zanzibar .

  Ewe Allah wape laaana wanafiq hawa milele na wengine wasioipenda kheri Znzbar kama ulivo walaaani wanafiq kabla yetu.
  AAAAAmin.

  Na wewe Seif Sharifu, ikiwa umeridhika na huo umakamo wa kwanza, sawa nyamaza kama usiesikia na usieona haya wanayoyafanya wawakishi wako inshaaallah na wewe utapata unachokichuma.

  • Hongera kijana hawa Viongozi wametuangusha Wazanzibar ,wamesahau damu ilio mwagika kwa ajili ya kukilinda chama hicho kilowawezesha wao kudhaminiwa na kupata madaraka hayo. Nakumbuka Mnafiki Juma Duni Haji na wenziwe Kina Said Miraji 9/01/2001 walitwita Vijana wa Blue Guards Kilima hewa ofisi ya Wilaya ya C.U.F kupanga mikakati ya Maandamano ili kulinda heshima ya chama na kulani Matokeo ya Uchaguzi wa mwaka 2000. Nakumbuka Vizuri Juma Duni Haji akatwambia kuwa yeye anaweza kuishi popote hapa Duniani kutokana na Elimu aliyonayo lakini kajitolea muhanga ili ahakikishe Maisha ya Wananchi wa Zanzibar yanaboreka kwa kuhakikisha Tanganyika ina iwacha Zanzibar katika masuala Uchumi,Siasa na Zanzibar itapiga hatua Kiuchumi. Leo Juma Duni Haji anapinga Mzanzibar kupewa kipaumbele katika Ajira tena hapa hapa Zanzibar ?
   Mungu wetu Mtukufu warehemu wenzetu walotangulia mbele ya Haki,waliouwawa kwenye Mandamano

 2. hahahahahahahhaa mtume mbavu zangu mieee hahahahah kwikwikwikwi heheheh
  ostadh hamadi uko juu kaa wewe zaid ya msaniiii

 3. mm naungana maazo ya waliosema kua PASIWEPO HUO UTALII MAANA SIO SOURCE OF OUR INCOME KWA WAZNZ ila hawa jamaa hawana tabia ya kupitia ili kupata data za ukwelii
  na la IDS ni la kweli kuwa anapewa wasiostahiki ila ndio sera moja wapo ya ccm znz ili wapate kura ktk chaguzii zao sasa washaona kuwa zinwadhuru mfano mdogo uzini?

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s