Ibada ya Ijumaa Kuu

Father Michael Hafidh, akiongoza Ibada ya Ijumaa Kuu katika Kanisa la Mkunazini, na kuhudhuriwa na waumini wegi wa madhehebu hayo walioko katika Visiwa vya Zanzibar kitaifa imefanyika katika Kanisa Kuu Mkunazini leo mchana na kughudhuriwa na Askofu Mstaafu John Ramadhani. Ibada kama hiyo imefanyika katika makanisa mengine ya hapa Zanzibar.

 

WAKRISTO nchini wametakiwa kutunza utulivu na maelewano yaliopo kwani ndani ya utulivu inapatikana amani na maendeleo katika nchi na katika ngazi ya familia. Kauli hiyo imetolewa na Padri Stanley Nicholaus Lichinga wa katika Kanisa Kuu la Anglikana liliopo Mkunazini Mkoa wa Mjini Magharibi Zanzibar wakati wa mahubiri ya Pasaka yaliofanyika na kuadhimishwa na wakristo wote duniani ambapo wazo kuu lilikuwa ni kufufuka kwa Bwana Yesu.

Akitoa ujumbe katika mahubiri yake Padri Lichinga alisema amani, utulivu, umoja na umezungumzwa sana katika vitabu vitakatibu na kutakiwa wakristo wote kufuata nyayo za bwana Yesu ambaye alikubali kujitolea kwa ajili ya wakristo wote ulimwenguni na kwa kuwasamehe dhambi zao.

Padri Lichinga alisema ni vizuri wakati wakaristo wakisherehekea siku hiyo ya pasaka wakristo wakazingatia maneno yalioandikwa katika biblia na kutayafakari kwa kutafuata na kauchana na vitendo vyote viovu ambavyo vinakwenda kinyume na mafundisho ya biblia ambavyo mwisho wake vinapelekea uvunjifu wa amani.

Akinukuu Yohana ya 20, mstari wa 19 Padri Lichanga alisema “Ikawa jioni siku ile ya kwanza ya juma pale walipokuwepo wanafunzi, milango imefungwa kwa khofu ya Mayahudi akaja Yesu akasimama katikati akawaambia amani iwe kwenu (Asalamu Alaykum)”. Yohana 20:19

Akitoa salamu za kwanza za Bwana Yesu Padri Lichinga aliwaambia wakristo kwamba salamu ni kutakiana kheri na na amani juu ya mwengine kwa asalamu alaykum ambapo alinukuu Yohana ya 20:19ambapo alisema salamu inazaa umoja katika mtu binafsi, katika ndoa na katika familia nzima kabla ya kusambaa katika jamii nzima.

Padri Lichinga alisema jamii taifa na dunia nzima inahitaji amani na upendo kwani ndnai ya umoja na amani ndipo inapopatikana ufumbuzi  wa matatizo mengi na pia kuweza kukabiliana na utulivu unaotakiwa.

“Ndani ya umoja tunapata ufumbuzi wa matatizo yetu mengi na pia tubakiwa na utulivu kwa hivyo tunapaswa sote tuwe na amani kama alivyosema Bwana Yesu ili tubakie katika nchi yetu tuwe na amani ndani na nyumba zetu, ndani ya familia zetu lakini pia ndani ya jamii yetu na ndnai ya nchi yetu amani itawala” alisema Pardi huyo.

Katika mahubiri yake ambayo yaliwakusanya wakristo kutoka sehemu mbali mbali Padri Lichinga aliongeza kuwa utulivu unatoa nafasi ya maendeleo katika nchi na nje ya utulivu kunakuwa ni vurugu ambalo halitakiwi kuwepo katika taifa lolote na kuwataka wakristo kuacha kufanya vitendo vya vurugu kwani haviwezi kusaidia katika jamii wala nchi.

“Utulivu unatoa nafasi ya maendeleo nje ya utulivu ni vurugu tupu, kisiasa, kijamii na kifamilia na pia kiroho” alisisitiza kuwaeleza waumini hao katika kanisa kuu l;a Mkunazini ambapo kanisa hilo limejengwa tokea wakati wa utawala wa kifalme hapa Zanzibar.

Naye Father Emmanuel Masoud akitoa mahubiri katika liliopo Mbweni alisema waumini wa kikristi wanapaswa kufuata maelezo na kusoma Biblia kwa mazingatia ili kuacha vitendo viovu vinavyofanyika na badala yake kurejea katika kitabu kitukufu kwa kufuata maelezo ya kitabu hicho.

Alisema iwapo wakristo wote watafuta kitabu cha Biblia dunia inaweza kuishi kwa amani kabisa bila ya kutokezea matatizo kwani tayari Biblia umeweka muongozo mzima wa maisha ya wanaadamu kuishi vipi katika ulimwengu huu.

Kwa upande wa Kanisa kuu la Katoliki la Minara Miwili liliopo  Mji Mkongwe, Askofu Mkuu wa Zanzibar, Augostino Shao alisema bado kumekuwepo na ubaguzi hapa Zanzibar unaoendelea ambao unapaswa kukomeshwa kwa nguvu zote.

“Katika mazingira yetu ya kiswaini kuna watu, sitaki kujidanganya kwamba wanasukumwa kwa dini zao, ila labda niseme wanasukumwa kwa itikadi za ubaguzi wenye misingi wanayoijua wao wenyewe. Wanafanyabiashara wengi katika kisiwa chetu wamefikia hatua yav kuwa na bei tofauti za watu wa dini au mahali Fulani na mara nyingine hauzi” alisema Askofu Shao.

Alisema kero kubwa zaidi ni kwa magari ya kubeba mzigo, ambapo alisema hayo ni kama yamewekewa sheria na wanayoyahodhi au labda wanaotoa leseni ya kwamba yasibebe mizigo ya watu Fulani ambapo alisema yeye anafanya biashara lakini amekuwa akihudumia watu wote.

Askofu huyo alisema biashara sio dini, siasa, au ukabila ila ni huduma kwa wote hivyo serikali inahakikisha kwamba wanapewa leseni ya kufanya huduma hiyo kwa kuzingatia kila mtanzania anaheshimu usawa wa binaadamu wote.

Akizungumzia uhuru wa kutoa maoni Askofu Shao alisema haki hiyo ipo kikatiba lakini Zanzibar hivi sasa kumeibuka tena lugha za kejeli na matusi juu ya imani za watu wengine ambapo kuna baadhi ya wanaojiita viongozi wa dini wanaotumia sehemu za ibada na viwanja vya siasa kukashifu imani za watu wnegine na kutoa matamshi ya kuharibu mali za wengine.

“Kashifa na matusi haya yanatangazwa wazi mbele ya vyombo vya usalama, lakini hakuna hatua inayochukuliwa. Wengi tunafahamu, kwamba uongo unaporudiwa na kutangazwa mara nyingi, hudhaniwa kuwa ukweli wa maisha, lakini madhara yake ni makubwa kwa wale wanaotishiwa. Tunaomba vyombo vya usalama vishughulikie haya, kwani sheria bila ya usimamizi sheria hiyo haina meno” alisema Askofu Shao.

Askofu Shao alisema mfufuko wa ni matumaini ya vijana wenye uwezo wa kufanya kazi wapete ajira lakini ajira hazipatikani kwa kisingizio cha wawekezaji ambapo alisema ni jukumu la serikali na vyomvo vyake kuhakikisha kwamba vipaumbele vya shughuli za ufanisi wao ni kwa wananchi wake na sio wageni.

“Tunaomba serikali zetu ziwe makini zaidi kwa ajira za wageni. Inasikitisha kuona yanayofanyika katika kivuli cha uwekezaji. Si rahisi kumwona Mtanzania Roma au China anauza ice cream, au anfanya kazi ambazo ni za ujuzi mdogo za raia wa nchi ile. Tunaomba uchunguzi wa kina ufanyike katika hoteli za kitalii, na viwanda tulivyomilikisha wageni. Hali ilivyo kamwe haitoi matumaini kwa wasomi wetu” alisema Askofu Shao.

Alisema mfufuko ushindi dhidi ya maovu kwa njia ya kifo msalabani Yesu aliondoa giza la dhambi na kwa ufufuko wake ameleta mwanga wa kuona milele na hivyo mwaliko wa kuishi kweli.

Alisema ufufuko wa kristo ni ufunguo wa ukweli kwa wanyonge na sababu za kueleza sababu kuu za kufufuka kwa Yesu ni kuwakomboa wanaadamu waliogandamizwa kwa maovu ya dini, siasa, uchumi, ukabila na utaifa ambapo ushindi wa maovu hayo ulionekana pale Kristu aliyedhaniwa ameishia kaburini alipofufuka kutoka wafu.

Askofu Shao alisema Kristu hakuishia utandawazi wa zama hizi lakini yote aliyofundisha na kutenda kamwe hayajapitwa na wakati kutenda kwa haki, amani na upendo kwani mamba hayo hayapitwi na wakati.

 

 

 

 

 

 

Advertisements

2 responses to “Ibada ya Ijumaa Kuu

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s