Zanzibar waunda baraza la mitihani

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali
Mohamed Shein,akimuapisha Mhe,Ramadhan Abdalla Shaaban,kuwa Waziri wa
Ardhi.Makaazi,Maji na Nishati,katika hafla iliyofanyika Ikulu Mjini
Zanzibar jana,kabla Shaaban,alikuwa Waziri wa Elimu na Mafunzo ya
Amali

Wajumbe wa baraza la wawakilishi wamepitisha mswada wa sheria wa Kuunda baraza la Mitihani Zanzibar. awali Jina lililopendekezwa na waziri wa elimu wakati wakiwasilisha mswada ilikuwa ni Kuanzisha Bodi ya Vipimo na Tathmini ya Elimu Zanzibar. Waziri, pamoja na naibu wake Zahra Ali Hamad, pamoja na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Othman Masoud walijititajihidi kutetea jina la Bodi, lakini wajumbe wengi wa baraza khasa Backbenchers walifanikiwa kujenga hoja ya kuunda baraza la mithani Zanzibar ambalo majukumu yake hayatoingilia baraza la taifa la Mithani Tanzania (NECTA).
Japokuwa Baadhi ya wajumbe akiwemo Mwakilishi wa Jimbo la Chonga (CUF) Abdallah Juma Aballah Chonga walipendekeza Zanzibar ianze kutunga mithani ya Form 4 na kuacha kutegemea NECTA, Majukumu ya ‘baraza la Mithani Zanzibar’ yatakuwa ni kusimamia mithani ya Zanzibar (Darasa la Saba, na Form 2) pamoja na kufuatilia maendeleo ya elimu Zanzibar.  Wakichangia mswada huo Mwakilishi wa jimbo la Mji Mkongwe (CUF) Ismail Jussa Ladhu alisema wakati umefika kwa Zanzibar kuwa na chombo kinachojitegemea kitakachoshungulikia uratibu wa mitihani ya elimu ya juu hasa kwa kuzingatia umuhimu wa elimu nchini.
Jussa alisema mswada huo ni mzuri licha ya kuwa na kasoro madogo madogo ambazo zinapaswa kurekebishwa na alisema chombo hicho ni muhimu sana kwa sababu ndiyo kitakachoratibu shunguli za mitihani ya kuanzia kidatu cha kwanza hadi cha kumi na mbili.
Akizitaja kasoro hizo Jussa alisema kuna baadhi ya wadau ambao hawakushirikishwa katika mswaada huo na walipaswa kushirikishwa katika mchakato huo.
“Suala hili sio la Muungano na imefika pahala Zanzibar ianzishe mambo yake wenyewe kwani msiba mkubwa tulipata wa kufelishwa wanafunzi kati ya 3303 waliofutiwa matokeo zaidi ya 1000 wanatokea Zanzibar lakini waziri ameshindwa kutoa kauli yoyote kuhusiana na suala hilo, Wananchi wanauliza jee serikali ipo makini katika hili? Alihoji Jussa.
“Wananchi wa Zanzibar hivi sasa wanapoteza imani na wenzao wabara kutokana na mambo kama haya Mheshimiwa Spika.” alisema Jussa. Mwakilishi huyo aliwaambia wajumbe wa baraza hilo kwamba katiak suala la kuleta maelendeleo ya elimu nchini, serikali isione tabu kuzialika taasisi za elimu kutoka nje ya nchi kwa ajili ya kusaidia kuinyanyua elimu ya Zanzibar. Na kusisitiza kwamba nchi yeyote yenye maendeleo basi wananchi wake wanakuwa na elimu.
Mwakilishi wa Jimbo la Kwamtipura (CCM) Hamza Hassan Juma naye alisema ili kufuta machozi ya wananchi wa Zanzibar ni kubadilisha jina la mswada huu na sio kuzungukazunguka katika kutoa majina ta tahmini na viwango bali ni kusema moja kwa moja baraza la mtihani Zanzibar “Mheshimiwa Spika dawa kubwa ni wazanzibari kuunda baraza letu la mitihani basi hakuna jengine. Maana hawa wenzetu wamezowea kutubeza nakumbuka tulipotaka kuanzisha vyuo vikuu hapa kila majina wakitwita lakini jee tuwaulize leo kuna vyuo vikuu hakuna? Alihoji Hamza.
Alisema suala la kuundwa kwa baraza la mitihani Zanzibar haklina mjadala na wala halitaki kuzungukwa zungukwa kwani Zanzibar ina watalamu wake wa kila aina hivyo hakuna haja ya kuwa na kigugumizi katika hilo. Alisema katika suala hilo la elimu elimu ya form 4 Zanzibar kamwe haijakiuka katiba bali imetekeleza kwa vitendo azma yake ya kuinua kiwango cha elimu kwa wananchi wake, kwa kuwa rasilimali ya nchi yeyote ni elimu basi ni kurekebisha mitaala na sera za elimu.
kufuatia malalamiko ya hivi karibuni ya wanafunzi kufutiwa mitihani, baadhi ya wajumbe wa baraza la wawakilishi walipendekeza zanzibar ijitegemee katika kutunga mithani yake na kuachana na NECTA, lakini waziri na mwanasheria mkuu wakajibu kuwa Zanzibar kujitoa ktk NECTA ni kinyume cha sheria, halafu haiwezi kuwa ni suluhisho la matatizo ya mithani.
“Kwa kweli wanafunzi wetu wamefanya udanganyifu mkubwa. kamati ya baraza la wawakilshi ilikwenda Dar es saallam katika ofisi za NECTA na kuthibitisha hilo, na kamati ya wazee ambao watoto wao wamekumbwa na mkasa wa kufutiwa mithani pia wamethibitisha. hata kama tukiamuwa kutunga mithani wenyewe, tusiruhusu udanganyifu,” Shaabani alisema.
Alisema upo ushahidi wa kutoka kwamba watoto walifanya udanganyifu na kwamba ni lazima wazazi pamoja na waalimu waungane kupiga vita udanganyifu ili kupata wanafunzi wankaoweza kuwa wataalamu siku za baadae. Waziri alisema, katika hesabu za jumla, kati ya wanafunzi 3303 waliyofutiwa matokeo ya mithani, 2076 ni kutoka shule za zanzibar. “watoto wamefanya kosa, lakini adhabu ya miaka mitatu bila kufanya mithani ni mingi. nitazungumza na waziri mwenzangu wa elimu tanzania bara kuangalia uwezekano wa kupunguza adhabu hiyo.”
Amesema kuundwa kwa baraza la mitihani la Zanzibar sio suluhisho la kuepukwa kwa vitendo vya udanganyifu vinavyofanywa na wanafunzi katika mitihani yao.
“Mheshimiwa Spika hata kama Zanzibar itakuwa na Baraza lake la mitihani sio ufumbuzi wa tatizo hilo kwa sababu tatizo la udaganyifu wa mitihani ni la muda mrefu na vijana wetu wamepunguza kasi ya kusomea wanasubiri kuvuja mitihani ndio waanze kutafuta fedha wanunue” alisema Shaaban.
Waziri alisema wanafunzi 1,200 waliofutiwa mitihani yao hapa Zanzibar ni kutokana na kuthibitika kuwa wamefanya udanganyifu katika mitihani hiyo.
Alisema wanafunzi hao wamegundulika kuwa katika mtihani ya kiidato cha nne walifanya vitendo vya udaganyifu kwa kushirikiana na wasimamizi wa vituo wakati wa utahiniwa.
Waziri huyo alisema Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) lililazimika kufuta matokeo ya wanafunzi hao baada ya uchunguzi wa kina kufanyika jambo ambalo wizara yake nayo iliunda kamati maalumu ya kufuatilia suala hilo. Aidha Waziri Shaaban ambaye ameiaga wizara hiyo hapo jana alisema kwamba Wizara ya elimu ilichukuwa hatua kwa kulitaka baraza la mitihani la taifa Tanzania (NECTA) kuwasilisha ushahidi baada ya wanafunzi kufutiwa matokeo yao na serikali imelidhika na ushahidi wa Baraza hilo.
Aliwaambiwa wajumbe wa baraza la wawakilishi kwamba katika suala la mitihani kwa wanafunzi wa kidatu cha nne uthibitisho umepatikana kwamba wanafunzi walifanya udanganyifu na hivyo suala la kufutiwa matokeo limetokana na kasoro hiyo iliyotokea kwa udanganyifu huo.
Akitaja hatua za serikali katika suala hilo Waziri huyo alisema baada ya kutafakari kwa kina na kushauriana na wataalamu mbali mbali wa wizara yake serikali kupitia wizara ya elimu imeamua kuunda kamati ya kuchunguza kashfa hiyo ya udanganyifu na wasimamizi watakaobainika kuhusika na vitendo hivyo watachukuliwa hatua za kisheria.
Akitaja hatua ambazo serikali iemchukua ni pamoja na Wizara ya elimu na mafunzo ya amali kuchukua jukumu kusambaza mitihani ya kidato cha nne na sita na kusimamiwa katika vituo vya wizara badala ya kazi hiyo kufanywa na watendaji wa mikoa hapa Zanzibar.
Alisema licha ya kuwa wazazi wengi kuguswa na suala hilo lakini ni vyema wazazi hao wakachukua subra katiak jambo hilo kwani kuendelea kuwatetea wanafunzi ambao wamefanya vitendo vya udanganganyifu ni kutengeneza taifa dhaifu. Akizungumzia adhabu iliyotolewa na NECTA ya kuwazuwia wanafunzi kufanya mitihani miaka mitatu alisema adhabu hiyo ni kubwa na sasa wanapitia adhabu hiyo na kuangalia uwezekano wa kuweza kuipunguza kwani inaweza kuleta athari kubwa kwa wanafunzi.
“Ni kweli adhabu waliopewa wanafunzi kufungiwa kwa miaka mitatu wasifanye mitihani, adhabu hiyo ni kubwa lakini seriakli zetu zote mbili ya Zanzibar na muungano tumeanza kujadiliana kuangalia upya adhabu hiyo namna ya kutafuta utaratibu mwengine” aliwaambia wajumbe wa baraza hilo.
Mswada huo umepitishwa na wajumbe wa baraza la wawakilishi ambapo serikali imekubali kubadilisha jina la awali na kuitwa baraza la mitihani la Zanzibar ambapo awali jina lake lilikuwa Bodi ya vipimo na tathmini ya elimu Zanzibar jina ambalo lililalamikiwa na wajumbe wengi wa baraza hilo.
Moja ya kazi za Baraza hilo ni kusimamia mitihani ya shule ya msingi na mitihani ya kidato cha pili Zanzibar ambapo Waziri Shaaban alisema mitihani ya kidato cha nne na sita itaendelea kusimamiwa kama kawaida na Baraza la mitihani la Taifa Tanzania (NECTA).
Kwa mujibu wa mswada huo Baraza la mitihani la Zanzibar litafanya kazi ya kupima na kutathmini viwango vya ubora vya elimu ya maandalizi na msingi ili kuinua kiwango cha elimu cha Zanzibar. Waziri Shaaban alisema kwamba Wizara ya elimu na mafunzo ya Amali itaendelea kushirikiana na NECTA na Wizara yake haina mpango wa kujiondoa NECTA kwani wanafanya kazi pamoja.
“Mheshimiwa Spika Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar haina nia wala mpango wa ya kujitoa NECTA tutazidisha mashirikiano kwa kutumia uzowefu wao na utaalamu wao kuendeleza sekta ya elimu Zanzibar.”aliahidi Waziri Shaaban.
Kabla ya kupitishwa mswada huo wajumbe wakichagia muswada huo walishauri Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuanzisha Baraza lake la mitihani na kuchukuwa majukumu ya kusimamia mitihani yote badala ya kazi hiyo kufanywa na Baraza la Mitihani la taifa Tanzania NECTA ombi ambalo serikali imelikataa.

Advertisements

11 responses to “Zanzibar waunda baraza la mitihani

 1. “Mheshimiwa Spika Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar haina nia wala mpango wa ya kujitoa NECTA tutazidisha mashirikiano kwa kutumia uzowefu wao na utaalamu wao kuendeleza sekta ya elimu Zanzibar.”aliahidi Waziri Shaaban.
  Ama kweli aliyezoea kutawaliwa hawezi kujitawala. Hivi hii kuvuja kwa mitihani tu Mh Waziri haoni kua inatosha kua sababu ya msingi kujiondoa kuburuzwa na NECTA. Mh achana na mawazo mgando hayo huko NECTA elimu imekwisha wewe mwenyewe angalia ni watoto wa wakubwa gani ambao wanasoma chini ya NECTA? Kikwete UK, Makamba UK, Mwinyi Turkey kwanini kama NECTA kuna elimu watoto wao wanasomea nje? Haya lakini iko siku mtakuja jutia.

  • hatuna shida ya necta kwani tunaweza kujielimisha na kujiendesha wenye
   tuachane na mawazo mabovu kama kua hatuweze mpaka tuwezeshwe hii sio kweli
   wanzanzibar tunataka kila chetu necta tayari washapoteza muelekeo, wao wenyewe elimu
   washaishusha kiwango nchini kw kila siku kubadilisha mitaala na wanafunzi kufeli.
   wanzanzibar hatuyataki wala hatuyapendi haya mambo, tunataka tuone wanzanzibar wakiwa
   ni wasomi wa kweli na sio wa kuburuzwa,
   in order to do this we should trick together kuanzia juu sarekalini mpaka chini kw ushirikiano
   na raia wake

 2. Pingback: Zanzibar waunda baraza la mitihani·

 3. waziri kuitetea adhabu ya watanganyika ni upofu kwani yeye mwenyewe hajiulizin hata kama mtihani umepatikana ulitoka wapi?…wakurugenzi haohao ndo waliovujisha mitihani lakini panga wamefyekwa wanafunzi na kutaka kuwaonea wasimamizi sasa badala ya kuangalia vigogo wa baraza wenyewe ambao ndio chanzo cha udanyifu….HATUNA HAJA YA NECTA TUNAHITAJI KUJITAWALA HATA KIELIMU…ZINDUKA MZANZIBAR HUU NI UONEVU TUNAOFANYIWA……

 4. mke ni mke tuu hawezi kuwa mume, wazanzibar ss ni wake wa Tanzania bara tukitaka tusitake .Waswahili wanasema::”KIKULACHO KINGUONIMOOO”

 5. Jamani kama mpaka katika elimu pia lazima kuungano basi huo tena ni ulemavu wa kupita mipaka -heeeeeeeeee kazi kubwa hiyo lakini kama kweli basi na hao viongozi watoto wao wawaaache wasome izo shule tunazosomesha watoto wetu sisi walala hoi jamani this is toooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooomuch hii ni fedheha kubwa kwa wazanzibar ambao wana akili timamu huyu waziri wala hatufai.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s