Naibu Waziri aangua kilio barazani

Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Bi Zahra Ali Hamad leo aliangusha kilio barazani akikumbuka mazowea ya Waziri wake, Ramadhan Abdallah anayeondoka wizara hiyo

NAIBU wa waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Bi Zahra Ali Hamad, jana ameangua kilio mbele ya wajumbe wenzake wa baraza la wawakilishi akikumbuka mashirikiano makubwa aliyopewa na waziri wake wa Elimu na Mafunzo ya Amali Ramadhan, Abdalla Shaaban. Zahra ameangua kilio kicho wakati akifanya majumuisho ya mswada wa  kuanzishwa kwa bodi ya vipimo na tahmini ya elimu Zanzibar na mambo mengineyo yanayohusiana na hayo katika kikao kinachoendelea Mjini hapa.

Naibu huyo alishindwa kuzizuia hisia zake na kuwaeleza wajumbe wenzake wa baraza hilo kwamba mbali ya kuwa ni waziri wake alikuwa alikuwa akimchukulia kama ni mlezi na mzazi wake kutokana na kumsaidia na kumuongoza katika utendaji wa kazi zake tokea kukabidhiwa wadhifa huo na Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohammed Shein.

Jana Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amewaapisha baadhi ya mawaziri ambao waliondolewa katika nafasi zao na kuhamishiwa wizara nyengine akiwemo  waziri Ramadhan Abdalla Shaaban ambaye alikuwa waziri wa Elimu na Mfunzo wa Amali na sasa kuhamishiwa wizara ya Ardhi Makaazi Maji na Nishati.

Juzi usiku baada ya kupata taarifa za uteuzi mpya Bi Zahra alishindwa kujizuwia muda mfupi baada ya kupata taarifa hizo ambapo wakati akitoka ndani ya kikao hicho kilichomalizika usiku alionekana akifuta machozi na kuinama chini huku akikimbilia ndani ya gari lake na kushindwa kuongea na wajumbe wenzake licha ya kuwa baadhi ya wajumbe wenzake kumbembeleza lakini alishindwa kujizuwia na kilio hicho.

“Ahhh siwezi kusema chochote naomba niende zangu tutazungunza kesho inshallah” alisema wakati akiingia ndani ya gari lake.

Baadhi ya wajumbe wenzake walisema kinachomlinza Naibu huyo ni kule kupewa fursakubwa na kuelekezwa katika utendaji wa kazi na waziri wake huku akikhofia waziri wake mpya ambaye ni Ali Juma Shamhuna anayejulikana kuwa ni miongoni mwa mawaziri wenye misimamo mikali ya kihafidhina.

Naibu huyo alisema waziri wake amemuongoza katika utendaji kazi zake na alikuwa akimkosoa pale ambapo alikuwa akikosea lakini zaidi kukaa naye kwa wema na kumuelekeza ndiko kunakomfanya ashindwe kujizuwia kutoa kilio hicho.

Alisema mafanikio aliyoyapata katika wakati wote akiwa kama naibu waziri wa elimu yanayotokana na ushirikiano mkubwa alioupata kwa waziri wake ambaye licha ya kuwa anaondoka katika wizara hiyo alkini hatasahau jinsi alivyojitahidi katika kuinua sekta hiyo muhimu katika taifa.

Akifuta machozi, Zahra aliwaomba wajumbe wa baraza la wawakilishi na Mawaziri kumpa mashirikiano makubwa katika kipindi hiki ambapo sekta ya elimu imepata mtihani mkubwa kutokana na baadhi ya wanafunzi kufutiwa matokeo na kusababisha kilio kikubwa kwa wananchi mbali mbali wa Unguja na Pemba.

Waziri wa wizara hiyo Ramadhan Abdalla Shaabani wakati akijibu hoja za wajumbe waliochangia mswada huo alisema jambo la kwanza ni kumshukuru naibu huyo na kumtakia kheri na mafanikio mema katika akzi zake akiwa na waziri mpya ambapo alisema jukumu kubwa ni kufanya kazi kwa bidii ambayo ndio dira ya mafanikio.

Akitaja sifa za naibu wake alisema kwa muda wote ambao wamekuwa pamoja Zahra alijituma na kufanya kazi kwa umakini mkubwa huku akitoa mashirikiano makubwa na pale ambapo alikuwa akikosea alikuwa tayari kukosolewa bila ya kuweka kinyongo jambo ambalo alitaka naibu wake aendelee nalo.

“Nimefanya kazi na naibu waziri wangu huyu na hata siku moja sijawahi kufanya malumbano naye na ninamshukuru kwa usikivu wake na uvumilivu pale ambapo kulikuwa na kasoro ndogo ndogo tukielekezana lakini kwa mashirikiano tuliweza kufanya kazi kwa pamoja….na naamini kabisa tabia hii ataendeleana nayo kwa waziri mpya na pia kwa maafisa wake wengine” alisema Waziri Shaaban.

Advertisements

12 responses to “Naibu Waziri aangua kilio barazani

 1. Kilio chako pengine kinamaana nyengine ambayo haikudhihirika hadharani,pengine nikwamatokeo ya mitihani au kwa mgeni mpaya akiwa na silaha mkononi yenye jina la BAMIZA!!

 2. Namtakia mafanikio mema katika majukumu yake kwani ni kwel kwamba mazoea yana tabu tabia zikilingana asiwe na wac kwa uwezo wa allah bac hakuna linaloshindikana

 3. Haya ndio matunda ya umoja wa kitaifa, huko nyuma hayakuwepo hata kidogo, Allah aulinde umoja wetu inshallah.

 4. Nikweli kiasi ulie dada angu mana huyo ajae kiumbe msugu na mpenda madaraka hata ambiwe uwa mtoto wako yuko tayari sifa zote za ushetani anazo yeye.
  pole sana dada.

 5. Huyu jamaa kiasi alie kwa kuwa ajae hamjui. Watu wengi wanamjua kwa jinsi alivyoongoza jaribio la kukimaliza kizazi cha Wapemba wakati akiwa Wizara ya Nchi Mipango. Mtu aliyekataa Umoja wa Kitaifa kwa kura hapa 100%. Pole dada yangu! Nadhani adui ukishamjua si adui tena!

 6. TUMSIFU YESU KRISTO. Ni ukweli usiofichika kuwa WAZANZIBAR HAWAWEZI KUANZISHA NECTA YAO. Kwani znz hakuna wasomi, wazanzibar kazi yao ni kuimba kialabu na kufilana tu basi. WABUNGE WA ZANZIBAR HAWANAMCHANGO WOWOTE KATIKA MUNGE LA TZ. Mbunge anavaa kofia na suti anakaa kama shoga wa alabuni.

  • wewe uliyejiita Godfrey jifunze adabu za kuongea kwenye vyombo hivi. nakumbuka siku ulipolewa ukaanguka. Uliyfanyiw siyasemi kwani mimi naelewa Kiswhili na adabu zake. nakuasa ufute herufi za God kwenye jina lako kwni kuwepo kwake kunaashiria utukufu, kinyume kabisa- kwenda!

 7. DUH! Shamhuna. Dada ni lazima uliye WIZARA YA ELIMU IMEKUFA SASA. Hakika shule zote zitauzwa ili zifugiwe ng’ombe kama SHAMHUNA aliweza kuuza 200km za bahari ya znz hatoshindwa kuuza mjengo ya wizara ya elimu. Alipokuwa wizara ya habari TVZ ilikufa kutokana na kuuzwa vifaa.

 8. mama kulia ni lazima hakika umeumi huu ni msiba mkubwa katika wizara yenu. HUYU UNAELETEWA KASHINDA KILA MAHALI. HUYO NI MWIZI ANAIBA MPAKA VIOO VYA OFISI HALAFU ANAUZA. UKIEKA SIMU CHAJI HUIKUTI ANAIIBA NA KUIZA KAUZA BAHARI ASHINDWE NA NINI

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s