NGOs zisizo na sifa tutazifuta

Mrajis wa Serikali Abdallah Waziri akizungumza na Asasi za Kiraia katika ukumbi wa baraza la wawakilishi leo katika maonesho ya asasi hizo

MRAJIS wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Abdallah Waziri amesema jumuiya zisizo za kiserikali (NGOs) zilizosajiliwa hapa nchini zisizotekeleza majukumu na malengo yake waliokusudiwa zote zitafutwa na serikali. Kauli hiyo imetolewa katika kongamano la asasi za kiraia katika ukumbi wa baraza la wawakilishi na kuwashirikisha wana taasisi hizo mbali mbali wanaofanya maonesho ya kazi zao chini ya jumuiya ya Angoza ambayo ni mwemvuli wa asasi za kiraia hapa Zanzibar na kufadhiliwa na The Foundation for Civil Society.

Waziri amesema idara yake itazitafuta asasi zote ambazo hazina muelekeo wa utendaji wa kazi zake na kwamba serikali haitasita kuzifuta kutokana na kuwa zimeshindwa kutekeleza wajibu wake.

Alisema baadhi ya taasisi zimekuwa wakosoaji wakubwa wa serikali lakini asasi zenyewe zinashindwa kujitathimini na kutekeleza majukumu yake kama yalivyoainishwa katika katiba za asasi hizo.

“Mimi nimeshakaa miaka 10 katika kiti hicho na nimeona mambo mengi sana lakini kuna NGOs hapa zinashindwa hata kufanya uchaguzi na viongozi wanachaguana wenyew ekwa wenyewe tu au wanajiweka wenyewe tu hawafanyi uchaguzi tena NGOs nyengine zina majina mazuri tu lakini tunasema tumeshaanza kuzifuatilia zile ambazo hazitekelezi wajibu wake kama NGOs tutazifuta” alisisitiza Waziri.

Aidha aliwaambia wana azaki hao kwamba ipo haja ya kujirekebisha na kutekeleza majukumu yao kama asasi za kiraia ili malengo yalioainishwa katika maombi ya asasi hizo yafikiwe na kuwanufaisha wana jumuiya hizo.

Hata hivyo alisema wapo baadhi ya watu wamekuwa wakifanya jumuiya hizo kama ni mali yao binfasi na kujipa uongozi ambapo baadhi yao huwa wanaweka uongozi wa kifamilia jambo ambalo halikubaliki katika utawala bora.

“Ni kweli kwamba zipo jumuiya nyengine zinaendeshwa kifamilia maana mshika fedha, mwneyekiti na katibu wote amma ndugu au mtu na mkewe na wanawe nadhani hilo haliwezi kuwa jambo zuri kwa hali yoyote” alisema Mrajis huyo.

Akitoa mada ya mapungufu yanayotokana na sheria ya jumuiya ya Namba 6 ya mwaka 1995 katika kongamano hilo Mwanasheria kutoka Jumuiya ya Wanasheria Wanawake Zanzibar (ZAFELA) Fatma Saleh kwa niaba ya Hamisa Makame alisema sheria ya jumuiya ipo kimya juu ya hadhi ya jumuiya ambapo chombo chochote kinachofanya kazi kisheria kinatakiwa kiwe na hadhi ya kisheria.

“Sheria ipo kimya kuhusiana na hadhi ya kisheria ya kushtaki na kushtakiwa kwajumuiya kama ilivyo kwa sheria nyengine kama zile za kampuni kwa kuipa hadhi hiyo mara baada ya kusajiliwa kwake” alisema.

Alisema ingawa sheria imetambua uwepo wa bodi ya wadhamini ambayo inapata hadhi hiyo baada ya kusajiliwa kwa mujibu wa ile sheria ya (Land perpetual Succession Degree, 1929)  utaratibu huo ni urasimu na jumuiya zimekuwa zikifanya kazi bila ya kusajili bodi hizo za wadhamini kitu ambacho kinapoteza muelekeo wa jumuiya.

“Kuna haja kubwa ya sheria kurekebishwa ili mara jumuiya inaposajiliwa iwe na hadhi ya kisheria kama vile ilivyo kwa kampuni na si kupata uwezo huo kwa kutumia sheria nyengine. Mapungufu hayo pia yanaonekana kwenye sera ya jumuiya kwa kuonesha bayana. Hivyo kuna haja ya sheria ya jumuiya kurekebisha ili iweze kujitosheleza na kuenda sambamba na sera mpya ya jumuiya” alisema Mwanasheria huyo.

Miongoni mwa mapungufu mengine ni kukosekana kwa muda maalumu aliowekewa msajili katika kuisajili au kuikataa jumuiya iliyoomba usajili, “Kutokana na kuwa mrajis hajawekewa muda maalum wa kuikatalia usajili tokea kupeleka maombi jumuiya inaweza kupewa usajili baada ya mwaka au miaka miwili ambapo hiyo inanyima fursa mbali mbali za jumuiya kutokana na kukosa usajili ingawa inaendelea na shughuli zake” alisema Mwanasheria huyo.

Advertisements

4 responses to “NGOs zisizo na sifa tutazifuta

  1. Rafiki yangu Abdalla Waziri hili ni wazo zuri. Watu wengi hapa kwetu tunaona NGO ni mwajiri mbadala na ndo mana kila mtu anaanzisha yake hata NGO yenye malengo sawa na ya kwake ipo. Angalia NGO za UKIMWI zilivyojaa eti tu kwa kuwa hii ni nyimbo ya Wafadhili. Katika hawa wanaondesha hakuna aliyetayari kujitolea hata safari ya kwenda dar na kurudi. Katika miradi ya NGO hizi utakuta fungu la “Administrative costs” na katika hili mna mishahara ya Executives. Hapo nyuma tunakumbuka Ford Foundation iliipa ANGOZA pesa kwa ajili ya “Capacity Building” sehemu kubwa ikatumika kulipa mishahara na safari za viongozi. Watu ambao ndani ya nchi yao watumishi rasmi hawazidi dola 100,00 kwa mwezi walijilipa hadi dola 500.00. Rafiki Mrajisi ni vizuri pia ungalie Wafadhili wa miradi kwa kuwa nao hutumia NGO hizi kuendeleza ufisadi ambao kwao hauruhusiwi. Kuna NGO ambazo hata kama utendaji wao hauowani na taratibu lakini kazi zake zinataathira na watu wanafaidika nazo. Tahadhari iwepo tusichanganye mchele na chua.

  2. NI BORA BAADHI YA WAMILIKI WA NGO’S KUFUNGULIWA MASHTAKA MAHAKAMANI KWANI KUNA BAADHI YA NGOS ZINAPINGA KAULI YA SMZ YA KUENGEZA MISHAHARA NA KULIPA KWA WAKATI WAAJIRI WAO KWA MFANO SHULE YA AL-HARAMAIN KWAMCHINA ZANZIBAR INAWATESA WAFANYAKAZI SANA BILA YA SEREKALI KUZUNGUMZA CHOCHOTE UKIZINGATIA SMZ INAYOTAARIFA YA KUWA WAFANYAKAZI WA AL-HARAMAINI WANALIPWA MSHAHARA 100000/- KWA MWEZI TENA MSHAHARA UNACHELEWA MPAKA TAREHE 5 AU 10.

  3. SKULI YA ALHARAMAINI YA KWA MCHINA ZANZIBAR INAWALIPA WAFANYAKAZI WAKE KIWANGO KIDOGO CHA MSHAHARA TENA TAREHE 35 / 40 PIA HAIZINGATII ELIMU YA MUAJIRIWA WAFANYAKAZI WOTE WANALIPWA VIWANGO SAWA VVYA MSHAHARA BILA YA KUJALI VIWANGO VYAO VYA ELIMU.

  4. Hii lazima itokee kwa kuwa Waajiri hawana mwega wakati wa kutafuta ajira! Sijui hawa walipwao hivi ni walimu au wafagiaji! Kama ni Walimu basi walipofua wakati wa kusaini mikataba ! Mimi nafikiri Wizara ya Tumishi ingetayarisha Tepmlate ya Mkataba ambao Sekta isiyorasmi ingeifata !

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s