Timu ya Habari yapokewa na Naibu Waziri

Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Zanzibar Bi hindi Hamad Khamis akipokea Kikombe cha Ushindi Upande wa Netboll kwa msaidizi Katibu wa Timu ya Habari Spots Club ya Zanzibar Amina Kapenta baada ya kuwasili na kupokewa timu hio katika Bandari ya Zanzibar ikitokea Dar es salaam kulikokuwa na mashindano ya NSSF.

Timu za Wizara ya Habari,Utamaduni,Utalii na Michezo, Habari Sports na  Habari Queen, ambazo zilishinda michuano ya Kombe la NSSF jijini Dar es Salaam zimewasili leo Zanzibar na kupata mapokezi ya aina yake ambayo yaliongozwa na Naibu Waziri wa wizara hiyo Bi Hindi Hamad Khamis.

 

Mara baada ya kuwasili bandarini Zanzibar vikosi hivyo vililakiwa kwa ngoma aina ya Boso ambapo wachezaji wa timu hiyo kwa kushirikiana na viongozi wa Wizara hiyo walishiriki kusakata burudani hiyo ya ushindi.

 

Katika mchezo wa fainali kwa upande wa soka timu ya Habari Spots ilifanikiwa kuwatandika wenyeji wa michuano hiyo timu ya NSSF kwa jumla ya mabao 4-0 katika uwanja wa Sigara-Chang’ombe ambapo kwa upande wa netiboli Habari Queen waliwagonga kinadada wa TBC kwa magoli 30-10

 

Akielezea siri ya mafanikio ya ushindi huo, Kocha wa Habari Queen Amina Kapenta amesema ushindi wao ulitokana na juhudi na matayarisho ya muda mrefu ambayo waliyafanya kabla na wakati wa mashindano hayo.

 

Kwa upande wa Soka, Mwenyekiti wa timu hiyo, Issa Ahmada amesema nidhamu ya wachezaji na moyo wa kujituma ndiyo iliyokuwa silaha pekee ya kuweza kupata ushindi huo wa kishindo.

 

NSSF ilianzisha mashindano hayo tokea mwaka 2004 ikiwa ni mwaka wa tisa hivi sasa na imepanga kuyaboresha zaidi mashindano hayo kwa kuyafanyia katika mikoa mbali mbali ambapo kuna wanachama wake.

 

Huu ni mwaka wa pili mfululizo kwa timu ya Habari Queen kunyakua kombe la NSSF ambapo kaka zao Habari Sports ni mara yao ya kwanza kuchukua Kombe hilo tokea kuanza kushiriki katika mashindano hayo.

 

 

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s