Mahusiaono ya serikali na NGOs yaimarika

Mwenyekiti wa ANGOZA, Salama Kombo Ahmed akizungumza na waandishi wa habari Bwawani Zanzibar

Mahusiano kati ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Jumuiya zisizo ya kiserikali (NGOs) umeanza kuimarika kutokana na serikali kuanzisha mahusiano mazuri baina ya pande mbili hizo na kuondosha udhalilishaji (stigma) kwa taasisi hizo.

Hayo yameelezwa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Taasisi zisizokuwa za Kiserikali Zanzibar (Angoza) Bi Salama Kombo Ahmed katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika hoteli ya Bwawani Mjini hapa jana ambapo alisema licha ya kukabiliwa na changamoto kadhaa lakini hivi sasa uhusiano wao unaridhisha tofauti na siku za nyuma ambapo serikali ilikuwa ikiwaona kama ni wapinzania au wakosoaji wa serikali.

“Ni kweli kwa muda mrefu hatukuwa na mahusiano mazuri katika kuleta maendeleo kati yetu na serikali na kwa sababu mazingira yalikuwa yakichangiwa na hali ya kisiasa wakati wote tukihusishwa na kudhaniwa kama ni wapinzani kwa sababu tunaikosoa serikali lakini stigma ile sasa imeondoka na tumekuwa tukishirikiana vizuri na serikali ingawa tunataka mahusiano haya yaendelee na kuzidi” alisema Mwenyekiti huyo.

Alisema uhusiano uliopo sasa baina ya pande hizo mbili umeongeza nafasi ya Azaki kufikisha serikalini maoni juu ya haki zinazotarajiwa kutolewa na serikali kwa wananchi na kwa utaratibu huo wananchi watapata fursa muhimu ya kuwasilsiha maoni yao kwa serikali.

Akitoa historia ya asasi zisizo za kiserikali Bi Salama alisema asasi hizo zilikuwepo Zanzibar hata kabla ya mapinduzi na mfumo wa demokrasia ya vyama vingi, lakini hazikupewa fursa ya kutetea haki za wananchi kama ilivyo sasa ambapo wamekuwa wakifanya kazi zao bila ya kubughudhiwa.

“Azaki zilikuwepo kabla ya mapinduzi ya 1964, na tena azaki zilikuwa nyingi na zilikuwa nyengine ni za makabila lakini mfumo baada ya Mapinduzi ulipunguza ushiriki wa taasisi hizo katika masuala ya serikali kwa hofu kuwa zinawakilisha maoni ya upinzani, na kwa muda mrefu Zanzibar serikali ilikuwa na matazamo kutuona sisi ni wapinzani tu, lakini sasa mtazamo huo umeondoka” alisema Bi Salama.

Serikali unazidi kuimarika jambo ambalo linaleta faraja kwani serikali ikipokea maoni yanayowasilishwa na taasisi hizo huwa yanapokea maoni ya wananchi jambo ambalo ndio lengo la taasisi hizo.

Hata hivyo alisema kadri mfumo unavyobadilika, uhusiano baina ya Azaki na serikali unazidi kuongeza ushiriki unaotoa fursa kwa wananchi juu ya haki ya kujua masuala mbali mbali yanayogusa maslahi ya jamii.

Mwenyekiti huyop alisema kuimarika kwa uhusiano huo ni changamoto kwa asasi kuimarisha mfumo wa utoaji elimu ya umma ili kujenga uwezo wa jamii kujua umuhimu wa kudai haki, kama vile ya kupewa mamlaka ya kuhoji utendaji wa wawakilishi na wabunge wao na pia kufahamu fedha za bajeti zinazotengwa iwapo zinatumika vyema kama ilivyodhamiriwa.

“Azaki hatusemi kuwa zipewe uwezo wa kupiga kura ya kutokuwa na imani na wawakilishi au wabunge, tunataka uwepo mfumo unaoruhusu wananchi kueleza kutoridhishwa na utendaji wa mwakilishi au mbunge wao na kupendedekeza kuitishwa kwa uchaguzi mdogo katika jimbo lilanolohusika iwapo hawajaridhika na utendaji wa kiongozi wao na hilo linafanyika huko .”

Angoza imeandaa mdahalo utaojadili uimarishaji wa ushiriki mpana wa wananchi katika mchakato wa kuandaa, kusimamia na kufuatilia mipango ya maendeleo na bajeti ya serikali leo hii katika ukumbi wa baraza la wawakilishi.

Mdahalo huo umeandaliwa na Angoza kwa kushirikiana na Pasco na kugharamiwa na The Foundation for Civil Society na kwamba utafuatiwa na maonyesho na warsha itakayotoa fursa kwa wadau kujadili mchakato wa kuunda Katiba mpya.

Manufaa ya midahalo ya aina hiyo Bi Salama alisema imewezesha serikali ya Zanzibar kuharakisha utungaji wa sera ya serikali za mitaa ambayo sasa imo katika hatua ya mwisho kukamilika na kuwasilishwa katika vikao vya baraza la wawakilishi kujadiliwa.

Advertisements

One response to “Mahusiaono ya serikali na NGOs yaimarika

  1. HUU NI UONGO KWANI HADI LEO HII KUNA NGO’S ZINALIPA MSHAHARA 100000/- TENA TAREHE 15. SEREKALI HAISEMI KITU. USHAHIDI NI SHULE YA AL-HARAMIN ILOPO KWA MCHINA INANYANYASA WAFANYAKAZI NA SEREKALI HAIULIZI KITU MSHAHARA WANATOA KUANZIA TAREHE 10 NA KUENDELEA.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s