Aliyechoma Quraan ashindwa kufika mahakamani

PAMOJA na kuwasilisha rufaa ya kupinga adhabu aliyopewa katika kesi ya uchomaji moto msahafu pamoja na juzuu za dini ya Kiisilamu, hatimae kijana Ramadhan Handa Tuma ‘ameingia mitini’ mahakamani. Mkata rufaa huyo ambaye ni mwanafunzi katika Chuo cha Mafunzo kwa muda wa miezi 18, ameshindwa kufika mahakamani jana kwa ajili ya usikilizwaji wa rufaa yake hiyo.

 

Upande wa mpinga rufaa hiyo Aziza Idd Suweid, Mwanasheria wa serikali kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) ulikuwa upo tayari kwa ajili ya usikilizwaji, lakini ilishindikana kutokana na mkata rufaa kushindwa kuhudhuria katika kikao hicho.

 

Rufaa hiyo nambari hiyo nambari 4/2011 kutoka katika kesi ya jinai nambari 432/2010, ameiwasilisha mahakamani hapo tokea Oktoba 10 mwaka jana, mbele ya hakimu Nassor Ali Salim wa mahakama ya mkoa Vuga.

 

Katika kikao kilichopita, rufaa hiyo ilishindwa kusikilizwa kutokana na hakimu Nassor kushindwa kufika mahakamani hapo kutokana na sababu zilizokuwa nje ya uwezo wake.

 

Katika rufaa hiyo, Ramadhan Handa Tuma ambaye ni mkaazi wa Mombasa wilaya ya Magharibi Unguja, anapinga hukumu na adhabu iliyotolewa na mahakama ya wilaya Mwanakwerekwe, wakati alipokuwa akikabiliwa na kesi ya kufanya kitendo kinachoweza kuleta uvunjifu wa amani pamoja na kukashifu dini.

 

Katika kesi hizo, mahakama hiyo ilimtia hatiani na kumpa adhabu ya kulipa faini ya shilingi 200,000 kwa kosa la kufanya kitendo kinachoweza kuleta uvunjifu wa amani, pamoja na kutumikia Chuo cha Mafunzo kwa muda wa miezi 18 kwa kosa la kukashifu dini.

 

Adhabu hizo zilitolewa Febuari 21 mwaka jana, na hakimu Khamis Ali Simai na kufahamisha kuwa, endapo atashindwa kulipa faini hiyo atalazimika kukitumikia tena Chuo hicho cha Mafunzo kwa muda wa miezi sita na kuongeza kuwa adhabu zote hizo zitakwenda sambamba.

 

Hakimu Khamis Ali Simai, ambaye hivi sasa ni hakimu wa mahakama ya mkoa Mwera, alimtia hatiani mkata rufaa huyo chini ya kifungu cha 219 cha sheria za mwenendo wa jinai (CPA) namba 7/2004 sheria za Zanzibar.

 

Ramadhan hakuridhika na maamuzi hayo ya mahakama, na kulazimika kuwasilisha rufaa mahakama ya mkoa ya kupinga maamuzi hayo.

 

Katika kesi ya msingi kwa mujibu wa mahakama, Ramadhan Handa Tuma alifanya kitendo kinachoweza kuleta uvunjifu wa amani, chini ya kifungu cha 74 (1) (b) cha sheria namba 6/2004 sheria za Zanzibar.

 

Imefahamishwa kuwa Novemba 16 mwaka jana mahala hadharani kwa makusudi na bila ya halali alichoma moto msahafu pamoja na juzuu za dini ya Kiisilamu kitendo ambacho kingeweza kuleta uvunjifu wa amani kwa jamii ya Kiisilamu.

 

Sambamba na shitaka hilo pia alihusika kuikashifu dini hiyo ya Kiisilamu, kwa kuchoma moto vitabu hivyo kitendo ambacho ni kosa kwa mujibu wa kifungu cha 117 na 27 cha sheria namba 6/2004 sheria za Zanzibar.

 

Matukio yote yalitokea Mombasa wilaya ya Magharibi Unguja, saa 2:30 usiku wa Novemba 16, 2010.

 

Kesi hiyo ilifikishwa mahakamani hapo kwa mara ya kwanza Novemba 18, 2010, na kwa muda wote huo hadi kutolewa kwa hukumu hiyo mshitakiwa huyo alikuwa rumande kwa kile kilichoelezwa kwa usalama wa maisha yake.

Advertisements

4 responses to “Aliyechoma Quraan ashindwa kufika mahakamani

  1. uyo mtu inabidi apatiwe adhabu kubwa sana endapo akipatikana
    kwani anaonekana hataki kabisa amani ipate kudumu ndani ya zanzibar

  2. Ningeliomba waandishi kuwa makni katika kuripoti hbari nyeti na nzito zenye kubeba hisia za kiimani hasa katika dini yetu hii ya kiislamu kwani kosa hupelekea mtu kuhesabiwa ili kuipa heshima Qur’an isngelipaswa kuandikwa sentesi hii “alichoma moto msahafu pamoja na juzuu za dini ya Kiisilamu” na hii “kwa kuchoma moto vitabu hivyo”. Muandishi sema tu alichoma Qur’ani bila ya kutufanyia usanii hakuna kitu kinachitwa juzuu ya kiislamu.

  3. Huyu ilibidi kitu cha kwanza kuchapwa viboko visivopunguwa 20. Unguja tijuayo sisi hapo zamani ni kuwa
    kitovu cha dini tukufu ya Kiislamu katika Africa ya mashariki.

  4. Huyu Ramdhan ni mtu mwendawazimu ambaye hajui ” Ukiristo wala Uislamu”. Huyu ni muuza njugu kama wenzake na watu wasiandike wakamkuza. Awachiwe amalize muda wake jela kisha atahama kwa kuwa hataweza kuishi tena. Na akirudi bara atasaidia kupunguza Influx ya walevi na wazururaji wa usiku ambao wanaharibu heshima ya nchi hii.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s