Mfuko wa Maendeleo ya Jimbo Zanzibar

Hamza Hassan Juma Mwenyekiti Kamati ya Kusimamia Ofisi za Viongozi Wakuu wa Kitaifa ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar

Mhe Spika, kazi yetu ya uwakilishi ni ngumu sana kwani aliyeko nje humlaumu alieko huku ndani lakini miezi miwili tu akiingia humundani utamkuta analalamika kuwa anamaombi mengi lakini uwezo wa kuyatumia unakua ni mdogo, kwa hiyo waheshimiwa wenzangu tujitahidi kufanya kazi zetu kwa bidii ili kuiondoa hali hii na njia pekee ya kuliondoa tatizo hili ni kuibua miradi mikubwa ya kiuchumi hapa Zanzibar, tuendelee kushikamana kutafuta vianzio vipya vya mapato ikiwemo utafutaji na uchimbaji wa mafuta hapa Zanzibar, ili rasilimali hiyo ije kuwasaidia Wazanzibari wote kwa ujumla na Inshaallah Kwa uwezo wa Allah atatuwezesha kwa uwezo wake, pia tujitahidi kisimamia ukusanyaji wa mapato hapa Zanzibar ili yasivuje ili Mfuko wetu Mkuu wa Fedha za Serikali upate fedha za kutosha ili Serikali yetu iwe na uwezo wa kuwahudumia wananchi wetu kwa ujumla.

TAARIFA YA KAMATI YA BARAZA LA WAWAKILISHI YA KUSIMAMIA OFISI ZA VIONGOZI WAKUU WA KITAIFA JUU YA MSWADA WA SHERIA YA KUANZISHA MFUKO WA MAENDELEO YA JIMBO ZANZIBAR PAMOJA NA MAMBO MENGINE YANAYOHUSIANA NA HAYO.

 

 

UTANGULIZI

 

Mheshimiwa Spika, awali ya yote napenda kuchukua fursa hii kumshukuru Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa kutujaalia kwa mara nyengine kukutatana mbele ya Baraza lako tukufu tukiwa wazima na wenye afya njema ili kujadili mambo mbali mbali yanayohusu maendeleo ya Nchi yetu pamoja na mstakabali mzima wa wananchi wetu, likiwemo suala la kujadili na kupitisha miswada mbali mbali ukiwemo mswada uliopo mbele yetu. Mswada wa Sheri ya Kuanzisha Mfuko wa Maendeleo ya Jimbo Zanzibar na Mambo mengine yanahusiana na hayo.

 

Mheshimiwa Spika, aidha, napenda kuchukua fursa hii kukushukuru wewe binafsi kwa kuniruhusu kusimama mbele ya Baraza lako tukufu ili niweze kuwasilisha Muhtasari wa Taarifa ya Kamati ya Kusimamia Ofisi za Viongozi Wakuu wa Kitaifa ya Baraza la Wawakilishi, juu ya Mswada uliokwishaainishwa hapo juu.

 

Mheshimiwa Spika, Pia napenda kuchukua fursa hii kwa niaba ya Kamati kutoa mkono wa pole kwako wewe binafsi, wajumbe wa Baraza, wananchi wa Jimbo la Bububu na familia ya marehemu Salum Mtondoo aliyekuwa Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi na Mwakilishi wa Jimbo la Bububu, ambaye alifariki tarehe 15/03/2012 na kuzikwa tarehe 16/03/21 kijijini kwao Bumbwini Misufini na tunamuomba Mwenyezi Mungu amlaze mahala pema peponi Amin.

 

Mheshimiwa Spika, pia napenda kuchukua nafasi hii, kwa niaba ya Kamati kutoa shukrani za dhati kwa Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais kwa kutuwasilishia mbele ya Kamati Mswada huu na kuweza kuujadili kwa kina na uwazi.

 

Mheshimiwa Spika, pia napenda uniruhusu niwashukuru kwa dhati, Wajumbe wa Kamati yetu kwa mashirikiano na michangoyao muhimu waliyoitoa katika kuujadili kwa kina Mswada huu siku ya Jumatano ya tarehe 21/03/2012. Naomba niwataje Wajumbe wa Kamati yetukama ifuatavyo:-

 

1. Mhe. Hamza Hassan Juma             –         Mwenyekiti

2. Mhe. Mwanajuma Faki Mdachi    –         M/Mwenyekiti

3. Mhe. Ali Salum Haji                      –         Mjumbe

4. Mhe. Mgeni Hassan Juma              –         Mjumbe

5. Mhe. Mohammed Haji Khalid       –         Mjumbe

6. Mhe. Salma Mohammed Ali          –         Mjumbe

7. Mhe. Ussi Jecha Simai                 –         Mjumbe

8. Ndg. Rahma Kombo Mgeni           –         Katibu

9. Ndg. Ramadhan Kh. Masoud        –         Katibu

 

 

Mheshimiwa Spika, Utakumbuka kwamba chimbuko la Mswada huu lilianza mwaka 2002 wakati katika vikao mbali mbali vya bajet suala hili lilijitokeza mara kwa mara, Mhe Spika, hili halikuja bure bure tu, sababu kubwa ya Wajumbe wako kudai Fedha za Mfuko wa Maendeleo ya  Jimbo ilikuwa ni ham kubwa ya wananchi wetu wa Zanzibar kutaka kujiletea maendeleo katika majimbo yetu lakini uwezo wao unakuwa mdogo, na wananchi wetu wao kimbilio lao ni kwa Wawakilishi wao na wao mara nyingi, hawajui kama hali za Wawakilishi wao zinakuwa dhaifu kwani wanabeba majukumu makubwa majimboni yaliokuwa ya maendeleo na ya watu binafsi ambayo ndio mengi zaidi , kwani kutokana na hali ngumu za maisha kwa wananchi wetu kimbilio lao kubwa linakuwa ni kwa Wawakilishi wao, na wanapokujia na shida zao wao hawajui unacho au huna.

 

Mhe Spika, ukiangalia Wajumbe wako kila mmoja anaongoza watu zaidi ya elfu ishirini katika Majimbo yao na kila anaekwama wakatimwengine hata chejio basi kimbilio lao ni kwa Mwakilishi wao , Mhe Spika hii sio kama tunawasimbulai wananchi wetu bali ndio hali halisi ilivyo na tunawahakikishia wananchi wetu waliotuchagua kuwa hatununi wala hatukasiriki tunafurahi sana kila wakija kutueleza shida zao kwani tunaamini kila anaekuja kukueleza shida yake basi amekukinai na anakuthamini lakini mara nyingi uwezo wa kuwasaidia watu wote wanaotujia tunakuwa hatunao, lakini kila tunapokuwa nacho tunajitahidi kwa kadiri ya uwezo wetu kuwasaidia.

 

Mhe Spika, kutokana na mapenzi tunayowapenda watu wetu waliotuchagua, yeyote ikiwa amekaa siku tatu hajaendewa na wananchi wake kumuelezea shida zao, basi huwa hapati usingizi kwani huhisi labda wameshaanza kumchoka basi ni yeye mwenyewe tu hujipeleka na kujipishapitisha mitaani alau apate kuelezwa shida japo moja kwani haya ndio maumbile ya kazi yetu, kwa hiyo tunawaomba wananchi wetu msichoke kutujia na shida zenu na pale mnapokosa basi  wala msikasirike kwani hakuna alie kamilika.

 

Mhe Spika, kazi yetu ya uwakilishi ni ngumu sana kwani aliyeko nje humlaumu alieko huku ndani lakini miezi miwili tu akiingia humundani utamkuta analalamika kuwa anamaombi mengi lakini uwezo wa kuyatumia unakua ni mdogo, kwa hiyo waheshimiwa wenzangu tujitahidi kufanya kazi zetu kwa bidii ili kuiondoa hali hii na njia pekee ya kuliondoa tatizo hili ni kuibua miradi mikubwa ya kiuchumi hapa Zanzibar, tuendelee kushikamana kutafuta vianzio vipya vya mapato ikiwemo utafutaji na uchimbaji wa mafuta hapa Zanzibar, ili rasilimali hiyo ije kuwasaidia Wazanzibari wote kwa ujumla na Inshaallah Kwa uwezo wa Allah atatuwezesha kwa uwezo wake, pia tujitahidi kisimamia ukusanyaji wa mapato hapa Zanzibar ili yasivuje ili Mfuko wetu Mkuu wa Fedha za Serikali upate fedha za kutosha ili Serikali yetu iwe na uwezo wa kuwahudumia wananchi wetu kwa ujumla.

 

Mhe Spika, nimeamua kuyaeleza hayo kwa makusudi ili Serikali iweze kujua ni kiasi gani waheshimiwa tunavyosaidia Program ya kupunguza umasikini huko majimboni mwetu, Mhe Spika, hayo yote tunayakabili majimboni mwetu lakini kwa uwezo mdogo tuliokuwa nao inakuwa vigumu kuyamudu hayo yote, ndio maana Waheshimiwa wako wakawa wanahitaji alau kuwe na Mfuko wa jimbo ambao utawasaidia hasa kuweza kusaidia kwa yale mahitaji muhimu ya kijamii huko majimboni.

 

Kwa hiyo kwa muda wote huo Serikali ilikuwa haijaweka utaratibu maalum wa kumuwezesha Mwakilishi kupata fedha za uhakika kwa wananchi majimboni ingawa kulikuwa na fungu la miradi midogomidogo kupitia wizara ya Fedha, lakini kulikuwa hakuna utaratibu mzuri na wa uhakika kuzipata kama huu utaratibu unaoletwa na Serikali yetu kwa hivi sasa, kwa hiyo sio wajumbe wote walioweza kufaidika na fedha hizo napengine pia hata utaratibu wa kusimamia fedha hizo wakati mwengine unakuwa sio mzuri, lakini kupitia Sheria hii tutakayoipitisha tunaamini utaweza kutusaidia kuondoa baadhi ya kero ndogondogo majimboni mwetu   baada ya maelezo hayo machache sasa naomba kutoa maelezo ya mswaada huu.

 

Mhe Spika, tunaishukuru Ofisi yako ya Baraza la Wawakilishi mnamo mwaka 2008/2009 ilifanya ziara nchini Kenya kwenda kujifunza ni namna gani Mfuko huu umeweza kusaidia vipi wananchi wa Kenya, nakushukuru Mhe Spika, na mimi pia ulinishirikisha kwenda huko kujifunza na kwa kweli tukaona kuwa kumbe tumechelewa sana kutokuanzisha Mfuko huu, kwani tulipata nafasi ya kuongozana na Mbunge Jimbo la Naivasha kwenda kujionea kwa macho yetu Maendeleo aliyoyapata kupitia Mfuko huo ,kwa kweli yapo mengi sana lakini nitayataja machache kutokana na muda, kwa mfano katika jimbo lake tangu Uhuru wa Kenya ilipita miaka kama zaidi ya 30 jimbo lake lilikuwa na Shule za Sekondari hazikuzidi tano lakini baada ya kuanzisha Mfuko ndani ya miaka  sita waliweza kujenga Sekondari kiasi 15, kupitia fedha Mfuko wa Jimbo wameweza kujenga barabara za ndani nyigi katika maeneo mbali mbali ,amediriki hata kujenga Gereza la watoto ndani ya jimbo lake baada ya kutembelea Gerezani na kuona watoto wamefungwa pamoja na watu wazima wanaowazaa, pia sheria yao inawaruhusu kusadia malipo ya ada ya Shule kwa wale watoto ambao wamefaulu lakini wazazi wao hawakuwa na uwezo wa kuwalipia ada, pia wameweza kuwapatia fedha na kuwaanzishia miradi vijana ambao walikuwa wakikaa vijiweni (maskani) bila ya kazi na kuwapatia Tender kupitia baraza la mji ya kutengeneza Makalbi, Calvart na kujenga vikuta pembezoni mwa barabara. Kwa hiyo fedha zile zimewasadia sana wanchi wa majimbo yote ya Kenya, kwa fedha za Kenya wenzetu hupatiwa kiasi cha Kenya Shs 20 milioni kwa mwezi kwa Mfuko wa maendeleo wa Jimbo kwani wao wameweka asilimia 2 ya mapato yote ya Kenya ndio moja kwa moja huingia kwenye mfuko wa Jimbo kutoka mfuko mkuu wa Hazina wa Serikali ya Kenya, lakini kwa kua sisi ndio kwanza tunaanza na kutokana na makusanyo yetu kuwa madogo tunashukuru japo hiyo kwa kuanzia kwa shs milioni kumi sio mbaya sana ,lakini tunaiomba Serikali yetu kutokana na Mfumko wa bei ya vifaa hasa vya ujenzi hivi sasa hii pesa ni ndogo sana kwa hiyo tunaomba bajet ya mwakani ziongezwe alau kufikia milioni 20 kwa mwaka, tunajua hali ya Serikali yetu na safari ni khatua tunaamini kwa mashirikiano ya pamoja tutafikia mbali zaidi huko siku za mbele.

 

Mheshimiwa Spika, sasa napenda kutoa maoni ya Kamati kwa kufanya marekebisho mbali mbali katika Mswada huu muhimu katika Maendeleo ya Jimbo na Taifa kwa ujumla. Marekebisho hayo yaliyofanywa katika mswada huu yamegawika  Kama ifuatavyo:-

 

 1. Marekebisho ya Mswada kwa kubadilisha maneno ili yaendane na maana halisi ya Mswada. Kwa mfano katika Sehemu ya Kwanza ya Mswada, Kifungu cha 2 katika tafsiri ya maneno, maneno “Katibu Mkuu” na “Mkurugenzi” tafsiri zao zimebadilishwa na kuandikwa upya.

 

 1. Marekebisho ya Mswada kwa kuongeza vifungu kwa lengo la kuviweka vizuri vifungu hivyo pamoja na mswada kwa ujumla. Kwa mfano, Sehemu ya Pili, Ukurasa wa 29 wa Mswada kimeongezwa kifungu cha 3(3) ambacho kinaelezea dhamana ya Mkurugenzi katika utekelezaji wa shughuli za Mfuko.

 

 1. Marekebisho ya Mswada kwa kurekebisha maneno ili yalete maana halisi iliyokusudiwa. Kwa mfano, Sehemu ya Pili, ukurasa wa 29, kifungu cha 7(1) neno “Risiti” lisomeke “ Mapato yote

 

 1. Marekebisho ya Mswada kwa kufuta baadhi ya vifungu vya Mswada kwa kuonekena kutokuwa na umuhimu na pia kutoathiri kwa kutolewa kwake. Mfano, Sehemu ya saba, ukurasa wa 37, kifungu 30(3) kimefutwa.

 

 1. Marekebisho ya irabu kwa baadhi ya maneno ili yaende sawa na mpangilio wa maneno mengine kwa mfano, Sehemu ya Kwanza, neno “Ola” limebadilishwa na kuwa “la”

 

Mhe Spika, naomba kuwaelezea waheshimiwa wote kuyaangalia marekebisho yote tuliyoyasambaza asubuhi hii ili kuona ni kipi tulichokirekebisha katika mswaada huu ili na nyinyi mpate kuongezea pale sisi tuliposahau.

 

Mhe Spika, kwa kumalizia naomba nimshukuru sana mhe Makamo wa Pili wa Rais pamoja na Waziri katika Ofisi yake kwa kutuletea mswaada huu muhimu kwa maendeleo yetu, pia kwa heshima zote tunaomba utupelekee shukrani zetu za dhati kwa Mhe Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza Mapinduzi kwa kusikia kilio chetu cha kutaka Mfuko wa Jimbo na kutukubalia na tunamuahidi kuwa tutajitahidi kuwasimamia watu wetu tutakaowakabidhi fedha hizo ili wazitumie vizuri na pia tunaahidi kumbukumbu zote za matumizi tutaziwasilisha Serikalini, pia nawaomba waheshimiwa wenzangu kujitahidi kusimamia vizuri matumizi ya fedha hizi kwani tukifanya vizuri basi Serikali  tunaamini itaongeza fungu hilo kila mwezi na pia tunawatahadharisha wajumbe wenzangu kuwa kuna kifungu katika Sheria hii kwamba jimbo lolote litakaloshindwa kufanya marejesho basi halitopatiwa fedha nyingine hadi hapo watakapopeleka marejesho hayo.

 

Mheshimiwa Spika, naomba kuwashukuru wananchi wangu wa jimbo la Kwamtipura kwa kunituma kuwawakilisha katika chombo hiki kwa maslahi ya Wazanzibari wote,baada ya maelezo hayo, naomba niwashuru Wajumbe wote wa Baraza kwa kunisikiliza kwa makini na kwa niaba ya Kamati naomba waunge mkono Mswada huu kwa kuupitisha ili iwe Sheria itakayowaletea maendeleo wananchi wetu.

 

Mheshimiwa Spika, mwisho kabisa kwa mara nyengine naomba nikushukuru na kwa niaba ya Kamati na wananchi wa Jimbo la Kwamtipura naunga mkono hoja mia kwa mia.

 

 

 

Mhe Hamza Hassan Juma

………………………………..

Mwenyekiti

Kamati ya Kusimamia Ofisi za Viongozi Wakuu wa Kitaifa ya Baraza la Wawakilishi

Zanzibar.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

            

 

 

 

Advertisements

4 responses to “Mfuko wa Maendeleo ya Jimbo Zanzibar

 1. ALHAMDULILAH, ALLAH AMETURUZUKU BAADHI YA VIONGOZI WANAOJALI MASLAHI YA WANANCHI KAMA HUYU, WAZANZIBARI
  TUUNGANE
  KUCHIMBA MAFUTA YETU KWA MANUFAA YA NCHI YETU NA SIO NCHI NYENGINE
  WITO: VIONGOZI WA SMZ WAUNGANE KULETA MAENDELEO ZANZIBAR BILA YA KUJALI ITIKADI NA SERA ZA VYAMA VYAO.
  ZANZIBAR INAWEZA KUJIONGOZA WENYEWE BILA YA KUSIMAMIWA NA MATAIFA MENGINE. MAFUTA, UTALII NA KILIMO CHA
  KARAFUU NA NA NAZI NDIO UTI WA MGONGO WA MAENDELEO YA ZANZIBAR KWAHIVYO WAZANZIBARI TUWE WAKALI SANA NA
  WALE WOTE AMBAO WANATAKA KUFANYA UHARIBIFU WA MALI ZA ZANZIBAR

 2. YAARABI TURUZUKU AFYA NJEMA NA UWEZO WA KUCHIMBA MAFUTA YETU BILA YA KUPATA VIKWAZO KUTOKA KWA MAADUI WETU ABAO WANAJIFANYA MARAFIKI ZETU. KUMBE NDIO MAADUI ZETU WAKUBWA KATIKA KUDIDIMIZA UCHUMI WA NCHI YETU.
  YAARABI WAPE NGUVU WAWAKILISHI WETU WAWEZE KUITETEA NCHI YETU NA KUPAMBANA BILA YA HOFU NA MAADUI ZETU.
  YAARABI WAUNGANISHE VIONGOZI WETU WA SMZ WAWEZE KULITETEA TAIFA LETU KUWEZA KUWA HURU NA KUAMUA MBO YAKE YENYEWE BILA YA KUSIMAMIWA NA MAADUI ZETU AMBAO NI KIKWAZO CHA MAENDELEO YETU.
  EWE MZANZIBAR SHIRIKIANA NA VIONGOZI WAKO KULETA MAENDELEO YA NCHI YAKO.

 3. WITO:
  WAWAKILISHI WA SMZ CHUKUENI MFANO KUTOKA KWA MWAKILISHI HUYU KUZUNGUMZA MAMBO YA MSINGI NA SIO KULUMBANA BARAZANI UMOJA NI NGUVU UTENGANO NI UZAIFU. HAKIKA TUKIUNGANA MAADUI ZETU AMBAO WANAJIFANYA MARAFIKI ZETU WATASHINDWA KUIBA MALI ZA NCHI YETU. LAKINI TUKIFANYA WANAVYOTAKA WAO MAADUI ZETU DIVIDE AND RULE HAKIKA ZANZIBAR YETU ITAKUWA TEGEMEZI MILELE NA MILELE.
  MZANZIBAR UNGANA NA MWAKILISHI WAKO AMBAE ANAJALI MASLAHI YA WANANCHI WAKE KUITETEA ZANZIBAR DHIDI YA UKOLONI MAMBOLEO AMBAO NDIO KIKWAZO KIKUBWA CHA MAENDELEO YA ZANZIBAR.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s