Zaidi ya billioni moja zatolewa kwa waathirika wa MV. Spice

Watu walioathirika katika ajali ya Mv. Spice Islander ambao umeuwa mamia ya watu

ZAIDI ya shilingi billioni moja zimekusanywa hadi kufikia Machi 15 mwaka huu kufuatia ajali ya meli ya Mv. Spice Islander iliyouwa watu 1,529 katika visiwa vya Zanzibar.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais, Mohammed Aboud Mohammed aliwaambia wajumbe wa baraza la wawakilishi jana wakati akijibu suali la msingi lililoulizwa na Mwakilishi wa Jimbo la Ziwani (CUF) Rashid Seif Suleiman aliyetaka kujua ni kiasi gani cha fedha kilichokusanywa hadi sasa kwa ajili ya kuwafariji watu waliopata ajali ya meli hiyo.
Alisema fedha zilizokusanywa ni 1,271,581,288.15 ambazo zinatoka katika mashirika na watu mbali mbali walijitokeza kutoa ikiwemo madawa, sanda, sabuni, mashuka na mabusati kwa ajili ya kukalia wakati wa tukio la ajali hiyo mbaya iliyowahi kushuhudiwa hapa Zanzibar. Waziri Aboud alisema thamani halisi ya vitu haikupatikana kwa vile baadhi ya vitu vilivotolewa vilitumika moja kwa moja katika maeneo ya matukio hata hivyo madawa na vyakula vilikuwa na thamani ya shilingi millioni kumi na moja na lakini tano (11,500,000).
Serikali iliamua kugawa misaada yote iliyowasilishwa katika ofisi husika na kisha kugaiwa kwa wahusika wa maafa hayo ambapo utaratibu wa ugawaji wa fedha hizo umeshapagwa na karibuni serikali inatarajia kutoa tangazo rasmi la kuzigawa fedha hizo kwa wahusika, waliopatwa na ajali hiyo.  Kwa upande wa chakula Waziri Aboud alisema hakikuwa cha kutosha kuweza kugaiwa kwa wahusika wote na imeamuliwa chakula kigaiwe katika vituo vya watoto yatima na wazee wasiojiweza Unguja na Pemba na madawa na mashuka yatapelekwa wizara ya afya kwa ajili ya kugaiwa katika hospitali ambapo tayari zoezi hilo la uchukuaji vifaa hivyo limeshafanyika.
Akijibu suali la mwakilishi huyo aliyetaka kujua idadi kamili ya watu waliopoteza maisha aktika ajali hiyo Waziri Aboud alisema “Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa ripoti ya tume ya rais iliyochunguza ajali hiyo watu waliopoteza maisha elfu moja mia tano na ishirini na tisa (1529) na walionusurika walikuwa watu 941 hivyo inaaminika kuwa jumla ya watu wote waliokuwemo katika ajali ile ni watu 2470 kwa mujibu wa taarifa ya tume ya uchunguzi” alisema.

Advertisements

2 responses to “Zaidi ya billioni moja zatolewa kwa waathirika wa MV. Spice

  1. SAWA TUMUOMBE MUNGU ATUEKE HAI IKLI TUONE KWELI WALIOFIKWA NA MAAFA WATASAIDIWA ANGALAU KUPEWA RUZUKU HAIKUWA UGAWAJI WA VYANDARUA VYA MSAADA TU ULIGAIWA KWA KUZINGATIA ITIKADI YA SIASA JEE WPINZANZI 10 VYANDARU 2 NA CCM 1 VYANDARU 10.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s