Agakhan anyanganywa ardhi Mangapwani

Old Dispensary ni miongoni mwa majengo yalio chini ya Mfuko wa Agakhan, jengo hili lipo eneo la Mji Mkongwe wa Zanzibar

SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar imekiri kuufuta mradi wa Mfuko wa Agakhan kutokana na kushindwa kutekeleza makubaliano ya awali walioekeana kati ya pande mbili hizo. Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Fedha Uchumi na Mipango ya Maendeleo, Omar Yussuf Mzee aliwaambia wajumbe wa baraza la wawakilihi wakati akijibu masuali mbali mbali hapo jana katika kikao kilichoanza huko Mbweni Mjini Unguja.
Akiuliza swali lake la msingi Mwakilishi wa Jimbo la Kwamtipura (CCM) Hamza Hassan Juma alitaka kujua eneo la Mwangapwani linalomilikiwa na mfuko wa Agakhan lililokusudia kujenga hoteli kubwa ya kitalii pamoja na kiwanja cha michezo umefikia wapi kwa kuwa ni muda mrefu mradi huo umekwama.  Akijibu swali hilo Waziri Mzee alisema “Mheshimiwa Spika, mradi huu umefutwa tokea mwaka 2008 baada ya kusimamishwa mkataba wa kukodisha ardhi kutokana na mwekezaji kushindwa kutekeelza kama ilivyotarajiwa. Kwa maana hiyo mradi huo haupo tena” alisema Waziri huyo.
Mwakilishi huyo pia alitaka kujua jitihada zinazochukuliwa na serikali za kuukwamua mradi huo ambao ni tegemea kwa kuwa mbali ya hoteli lakini pia utajenga kiwanja cha mchezo wa Golf mchezo amabo hupendwa sana duniani hasa na watu matajiri.  Waziri Mzee alisema kutokana na kuwa mradi wenyewe umeshafutwa, na kwa kuwa wawekezaji hawakuomba kurejeshsewa kwa mradi huo, serikali haioni haja ya kufanya jitihada zozote za kuurejesha tena mradi huo.
Aidha alisema kwa sasa serikali inatafuta wawekezaji wengine ambao watapewa kuliendeleza eneo hilo kwa kuwekeza miradi mbali mbali.  Akijibu suala la wananchi watapewa jibu gani kutokana na mradi huo waliokuwa wakiutegemea Waziri Mzee alisema hivi sasa serikali imepokea maombi ya wawekezaji wengine kwa ajili ya kuliendeleza eneo hilo na kuona kuwa watakaopewa eneo hilo wataweza kutimiza matarajio ya wannchi wa Mwangapwani na Zanzibar kwa ujumla.
Katika upatikanaji wa ajira alisema maombi ya wawekezaji hao yatazingatiwa kwa kina huku akiwatoa khofu wananchi wa Mangapwani Mkoa wa kaskazini Unguja kutokuwa na shaka juu ya upatikanaji wa wawekezaji wapya ambao watatimiza azma yao hiyo ya kutoa ajira. Katika suali lake la Nyongeza Mwakilishi wa Kwamtipura alisema kwa kiasi kikubwa serikali ndio iliyokuwa haikutekeleza makubaliano hayo kati yake na mwekezaji jee ni kummnyanganya ardhi wakati serikali ndio mkosa.
Akijibu hilo Waziri Mzee alisema katika miaka 90 serikali ilikuwa na njaa kubwa sana ya wawekezaji hapa Zanzibar na Aghakgan ali[pojitokeza serikali moja kwa moja ikampa zaidi ya hekta 70 kwa kuwa ilikuwa na hamu ya wawekezaji.  Alisema lakini tokea miaka ya mwanazoni ya 90 alichokifanya mwekezaji huyo ni kuweka mkahawa katika eneo zima alilopewa licha ya serikali kusafisha na kutengeneza barabara ili kuwavutia wawekezaji lakini mwekezaji huyo hajaweza kuliendeleza eneo hilo alilopewa kwa chochote zaidi ya huo mkahawa.
“Baada ya kuona eneo tulilompa hekta 70 kashindwa kuziendeleza kwa kufanya chochote zaidi na (Restaurant) Mkahawa, Serikali imeamua kumpunguzia na ardhi na kumbakishia hekta 20 tu. Hivyo serikali imechukua ardhi yake kwa faida ya watu wake na serikali haitawacha kufanya hivyo kwa wawekezaji wengine” alisisitiza Waziri huyo.
Naye Mwakilishi wa Viti Maalumu (CUF) Mwajuma Mdachi katika suali lake la nyongeza alitaka kufahamu wawekezaji wengine wanaotaka kuwekeza wananatoka wapi.

Ambapo Waziri alijibu kwamba hana uhakika ya wawekezaji wapya wanapotoka na hana orodha ya wawekezaji lakini alisema ni wengi na kutoka sehemu mbali mbali. Hija Hassan Hija Mwakilishi wa Jimbo la Kiwani  (CUF) alitaka kujua iwapo hamu ya serikali kuwakaribisha wawekezaji kama ipo au imepungua Waziri alijibu kwamba hamu hiyo haijaondoka lakini tatizo lililo kwa sasa sio kutaka wawekezaji kwa kuwa wawekezaji wapo wengi bali tatizo lililopo ni ardhi.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s