ZFA msijitete -Maalim Seif

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akizungumza na wadau wa mpira wa miguu Zanzibar huko hoteli ya Bwawani.

Makamu wa Kwanza wa Rais Maalim Seif Sharif Hamad amewataka viongozi wa chama cha soka Zanzibar (ZFA) kuacha kujitetea na kusikiliza na kumaliza mogogoro kati yao na wadau wa michezo. Maalim Seif ameyasema hayo juzi katika kikao cha pamoja kilichowakusanyisha wadau wa michezo wakongwe na chipukizi, viongozi wa ZFA na wizara inayoshughulikia suala la michezo katika hoteli ya Bwawani Mjini Unguja ambapo aliwataka ZFA kusikiliza maoni ya wadau na kuyafanyia kazi badala ya kuanza kujitetea.

Makamu huyo wa kwanza alikiri kuwepo kwa matatizo ndani ya uongozi wa ZFA na kusema kwamba kwa kuendelea kuendeleza migogoro soka ya zanzibar haitaweza kuinuka hadi hapo viongozi watakapojipanga vyema na kutafuta mipango endelevu ya kuendelez amichezo zanzibar.

Aidha aliliagiza Baraza la Michezo Zanzibar (BTMZ) kukaa pamoja na ZFA kuandaa mkutano mkubwa wa wadau wote kwa lengo la kupitia upya katiba kwani inaonekana kuna kasoro katika katiba na utendaji wa kazi za chama hicho cha soka ambacho kinategemea na wadau katika kuinua soka nchini.

“Baada ya kusikiliza pande zote naona kuwa ZFA kuna matatizo lakini katiba yetu pia ina matatizo, lakini ZFA msiwe mnajitetea sana chukueni maoni na myafanyie kazi kwa hivyo baraza itisheni mkutano wa wadau mpitie katiba na kama nkuna kasoro zirekebishwe na kama mkiona hazifai basi muandike katiba mpya” alisema Maalim Seif.

 

Maalim Seif Sharif Hamad ameitaka ZFA kufanya kazi za ziada ili kuhakikisha kuwa soka la Zanzibar linarejea katika hadhi yake ya asili kwani Zanzibar imekuwa wasindikizaji wa michezo mbali mbali ukiwemo mchezo wa soka, na kutaka juhudi za makusudi zichukuliwe ili soka la wanaume na wanawake liweze kurejea katika hadhi.

Ni lazima Zanzibar ijipange ili kurejesha soka na kuvutia wanasoka wazalendo, badala ya kushabikia soka la Ulaya na kuliwacha la hapa nyumbani alisema Maalim Seif.

Katika mkutano huo uliowashirikisha wadau wakongwe na chipukizi Maalim Seif aliahidi kuliendeleza suala hilo na kwa yale ambao ana uwezo nayo atayachukulia hatua na kwa yale ambao yapo nje ya uwezo wake atakaa na wizara husika na yaliokuwa makubwa atayawasilisha kwa rais wa Zanzibar Dk Ali Mohammed Shein.

Katika mkutano huo ZFA imeshutumiwa kukosa mvuto kwa wadau wa soka na kushauriwa kujiuzulu ikiwa ni kutoa nafasi kufanyika kwa uchaguzi mwengine ili uongozi uliopo madarakani ukae pembeni kwa ajili ya kunusuru soka isije kupotea kama ilivyopotea michezo mengine hapa Zanzibar.

Shutuma nyengine kwa ZFA ni viongozi wake kutokuwa na elimu ya kutosha ya kuendeleza soka, kushindwa kusimamia majukumu yao na kuacha soka la Zanzibar kuporomoka ikiwa pamoja na kuendeleza malumbano yasio na tija katika sekta hiyo ya michezo ambapo wadau hao walisema ZFA haiwezi tena kujisafisha kwa wadau wa michezo kutokana na doa la muda mrefu la kuendeleza migogoro.

 

Wadau mbali mbali wa mpira wa miguu wanaume na wanawake wamekishutumu chama cha ZFA kuwa kimepoteza mwelekeo na kutaka uongozi wa chama hicho uwajibishwe ili kutoa nafasi ya kuendeleza michezo nchini.

Aidha wadau hao wamesema kuwa sababu za kufa kwa mchezo mpira wa miguu ni kunatokana na chuki, ubinafsi na ubaguzi na majungu kwa viongozi wanaosimamia mchezo huo jambo ambalo linachangia kutia sumu kutika mafanikio ya soka nchini.

 

“Katika Vyama vinavyosimamia soka kumetawaliwa na mambo haya ambayo yanaifanya Zanzibar isifike mbali kisoka kutokana na ubinafsi wao”, alisema Mwenyekiti wa ZFA
Wilaya ya Mjini Hassan Haji Hamza maafuru Chura.
Alisema Zanzibar kuna wataalamu wengi wa mchezo huo lakini wanashindwa kutumiwa
kutokana na sababu fulani ambazo wanazijua wenyewe viongozi na hivyo soka ya Zanzibar kushuka na kutoonekana ya maana kwa washabiki.

Walisema wakati umefika kwa ZFA kuondoka madarakani kwa sababu wameshindwa kuendeleza soka na badala yake wanaendeleza migogoro huku wakitoa mifano ya viwanja vya mipiga kugeuzwa vigae vya kuchezea karata na kutafunia nyuju.

“Hakuna mpira hapa Zanzibar leo hii ukenda pale uwanja wa Mao tzetung watu wanakwenda kula njugu tu maana ukimuuliza lile pa limefungwa na nani hajui au mtu anaytoka pale muulize bao ngapi atakwambia ahhhh hata sijui …” hiyo ndio hali halisi alisema watu wanakwenda pale kwa mazowea tu na sio kutizama mpira.

Mwanasheria wa ZFA Taifa, Abdallah Juma alisema kuwa ili soka la Zanzibar liendelee ni lazima katiba ya chama hicho ifanyiwe marekebisho kutokana na kuwa imepitwa na wakati.

Alifahamisha kwamba katiba inayotumiwa na chama hicho kwa sasa haifai kuendelea kutumiwa kutokana na kupitwa na muda, jambo ambalo linahitaji kupatiwa ufumbuzi kama kweli wana nia thabiti ya kuendeleza na kukuza mchezo huo.
Hata hivyo, alisema kwamba viongozi wa chama hicho wanahitaji kujiuzulu kutokana na upeo wao wa kufikiri kuonekana kufikia kikomo.

Makamu wa ZFA Pemba, Ali Mohammed yeye alitupia lawama waandishi wa habari na kuwataka waache kuibomoa ZFA katika vipindi vyao vya radio, televisheni na magazeti ambapo alisema wamekuwa wakiitangaza vibaya licha ya kuwa inafnaya vyema kazi zake.

“Waandishi wengine wao kazi yao kuiandika vibaya tu hii ZFA kwa kweli inasikitisha maana utaona vyommbo vya habari kila ukisikiliza na kusoma habari zao utaona nondo, misumari basi hakuna jengien kila siku wanaisakama ZFA, na tumeitisha kikao na waandishi wa habari tukasema tunapiga mstari hatutaki tena migogoro lakini bado wanaendelea” alisema Mohammed.

 

Makamo huyo alisema licha ya shutuma hizo lakini chama hicho kinafanya vizuri na hawawezi kujiuzulu. Amesema iwapo watakuja viongozi wengine wanaweza kufanya mabaya zaidi kuliko hayo yanayoshutumiwa kufanywa na uongozi uliopo.

Akijibu shutuma hizo Makamo wa ZFA taifa, Alhaji Haji Ameir alisema wamepokea changamoto hiyo na kuahidi kuzifanyia kazi kwa umakini ili kuendeleza mchezo wa soka nchini.

 

 

 

 

 

 

 

Advertisements

One response to “ZFA msijitete -Maalim Seif

  1. Nakubaliana na Mwanasheria kuwa Katiba ya ZFA inahitaji kufanyiwa marekebisho. Mimi naona kuwe na ZFA taifa tuu na wasi ongeze utitiri wa ofisi ambazo ni vichekesho tuu kuwepo kwake. Angalia Ofisi za ZFA Wilaya ya Mjini na Wilaya ya Magharibi- ivo kweli mtu aliye serious ataamini kuwa wanatumia ofisi hizi wanajukumu la kuendesha soka.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s