Rushwa hatutaivumilia- Jaji Mkuu

Jaji Mkuu wa Zanzibar, Omar Othman Makungu akiwa ofisini kwake Vuga Mkoa wa Mjini Magharibi

JAJI Mkuu wa Zanzibar, Omar Othman Makungu amesema Idara ya Mahakama haitowavumilia mahakimu na watendaji watakaojihusisha na vitendo vya rushwa na kuwanyima haki wananchi. Makungu alisema hayo wakati alipotembelea Magereza na vyuo vya mafunzo kwa lengo la kujitambulisha baada ya kuteuliwa na Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohammed Shein kukamata wadhifa huo mkuu.

Alisema vitendo vya rushwa vimeipotezea hadhi na heshima mahakama na hivyo kwa sasa juhudi zaidi zinapaswa kuchukuliwa ili kurejesha hadhi na heshima ya chombo hicho muhimu katika kuleta maamuzi sahihi ambacho ni tegemea la wananchi walionyimwa haki zao.

Alisema hakuna atakayeonewa lakini mahakama itafanya kazi na kuwachunguza wale watakaotuhumiwa kufanya vitendo hivyo kwa mujibu wa sheria.

“Mahakama ni chombo kinachotegemewa sana kutoa haki kwa wananchi kwa hivyo lazima watendaji wake wawe watu wasafi, waadilifu na wenye kutenda haki ili kurejesha imani kwa wananchi juu ya chombo hiki” alisema Jaji Makungu.

Alisema kwa muda mrefu Mahakama zimekuwa zikibebeshwa lawama ikiwemo kushindwa kutekeleza haki kwa watu wanaofikishwa katika taasisi hizo, mazingira ambayo yamewafanya watu kupoteza imani kwa taasisi hizo ambazo wajibu wake ni kutoa haki sawa kwa wote.

“Idara ya Mahakama haitowavumilia Mahakimu wanatakaobainika kujishungulisha na vitendo vya rushwa wakati wanapotekeleza wajibu wao…..tumedhamiria kujenga mazingira ya kutoa haki kwa mujibu wa sheria na kurudisha imani ya Mahakama kwa wananchi wote” aliahidi Makungu.

Alisema katika kuhakikisha mahakama inafanya  kazi zake vizuri imejipanga kuhakikisha kwamba rufaa zilizokatwa na wafungwa zinasikilizwa kwa wakati na ili haki iweze kutendeka  kwa lengo la kutoa haki na kupunguza mrindukano wa mahabusu, magerezani na waliowekwa rumande.

Mikakati mengine ambayo amedhamiria kuifanyia kazi ni pamoja na kuwaomba wajumbe wa baraza la wawakilishi kuongeza bajeti kwa vyuo vya mafunzo kwa kuwagudumia waliowekwa humo kwa dawa na vyakula.

Alisema Jaji Makungu kwamba bajeti inatengwa ni ndogo na haiwezi kukidhi haja kutokana na  watu waliomo ndani ni wengi hivyo idara hiyo inashindwa kutekeelza majukumu yake kwa ufanisi zaidi.

“Nitawaomba wajumbe wa baraza la wawakilishi waishawishi serikali kuongeza bajeti ya Idara ya Mahakama ili kuweza kutekeleza majukumu yake katika Taasisi zake mbali mbali lakini zaidi ni kwa ajili ya mahabusu kuweza kupata vyakula na dawa” alisema Makungu.

Aidha Makungu amesema Idara ya Mahakama inakusudia kujenga mahusiano mema na kuwa karibu na wananchi na kuondoa dhana iliopo kwamba Mahakama ni sehemu ya kutoa adhabu kwa wananchi.

‘Katika mpango kazi wetu tumeandaa Elimu kwa Vyombo vya Habari kupitia Redio na Televisheni vya kutoa Elimu ya Uraia kwa wananchi kuhusu haki zinazopatikana Mahakamani….tumebaini kwamba wananchi hawazijuwi haki zao zinazopatikana Mahakamani hapa lakini pia wananchi wamepoteza imani na chombo hiki muhimu” alisisitiza Makungu.

Jaji Mkuu yupo katika ziara ya kutembelea Magereza mbali mbali ya Unguja yaliopo Mjini na Vijijini kujionea hali halisi na mazingira wanayoishi wafungwa na mahabusu na kujuwa matatizo yao pamoja na kujitambulisha rasmi kwa wafanyakazi wa idara hiyo.

Kamishna Mkuu wa Vyuo vya  Mafunzo Zanzibar, Khalifa Hassan Chumu amesema yamekuwepo mabadiliko makubwa katika vyuo vya Mafunzo (Magereza) kwa lengo la kuimarisha Utawala Bora ikiwa pamoja na marekebisho hayo ikiwemo kuheshimu haki za wafungwa pamoja na mahabusu na kuweka mazingira mazuri katika sehemu wanazoishi ambapo kwa sasa wanapewa uhuru.

Kamishna huyo aliwataka wanafunzi hao waliowekwa rumande kuwa huru katika kutoa maoni na malalamiko mbele ya Jaji Mkuu naye atakuwa tayari kuwasikiliza ambapo baadhi yao walimlalamikia Jaji na kutoa maombi.

Katika risala yao wanafunzi hao walimuomba Jaji Mkuu kuendelea kuwaelimisha mahakimu ili watoe masharti mepesi na nafuu ya dhamana kwa watu wanaowekwa ndani kwani kufanya hivyo kutaepusha wao kuwekwa muda mrefu na keshi zao kusikilizwa kwa haraka na kutaka haki itendeke

Advertisements

2 responses to “Rushwa hatutaivumilia- Jaji Mkuu

  1. JEE MFUPA ULIOMSHINDA FISI JAJI MAKUNGU ATAUWEZA? LET US SIT AND WAIT TIME WILL TELL. IDARA INANUKA RUSHWA NA WALA RUSHWA KILA MMOJA ANAWAJUA ANZA KUFAGIA TU MH.

  2. Mheshimiwa Jaji nakupongeza kwa kukiri kuwa kuna manatatizo ndani ya Taasisi yako ambayo ni Moja wa Mihimili mitatu ya Dola. Haya yanayokea si ya kuvumilia kwa kuharibika kwa taasisi hii muhimi ni kuuwa Dola ambayo sote tunawajibu kuilinda.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s