Polisi Pemba adaiwa kubaka

Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, Inspekta Said Mwema

Mahakama ya Kijeshi Kisiwani Pemba jana imesikiliza tuhuma za Askari Polisi John Joseph Bundala anayedaiwa kumbaka Mwanafunzi wa miaka 17 na kumsababishia maumivu makali. Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kusini Pemba Hassan Nassir amesema mahakama hiyo imesikiliza tuhuma zinazomkabili mfanyakazi wao na kisha kukusanya ushahidi wa kina kabla ya kupandishwa katika mahakama za kiraia kwa mujibu wa taratibu za ofisini yake.
Mtuhumiwa huyo mwenye miaka 30 ni muajiriwa wa jeshi la polisi katika kituo cha Mkoani Pemba anashutumiwa kumbaka binti huyo (Jina limehifadhiwa) ambaye ni mwanafunzi wa darasa la tisa aliyekuwa akifanya kazi nyumbani kwake. Hassan Nassir amesema walikuwa wakisubiri ushahidi wa kutosha ndipo wamfikishe katika vyombo vya sheria na ikithibitika kuwa ametenda kosa hilo hatua ya kwanza ni kufukuzwa kazi.
Kwa mujibu wa taarifa za mama mzazi wa mtoto huyo Bi Asha Ali Salum amesema, mwanawe ni mwanafunzi na alimgundua baada ya kumuona akimwgika damu nyingi jamboa ambalo awali alikuwa ameficha kutokana na woga.  Bi Asha amesema mwanawe aliogopa kumueleza kutokana na kupigiwa simu na Askari aliyefanya kitendo hicho kumtaka asimtaje jina kwa kuogopa kuhatarisha kazi yake ya upolisi.
Akizungumza kwa upande wake Afisa Mdhamini wa Maaendeleo ya Vijana Wanawake na Watoto, Bi Mauwa Makame Rajab alisema bada ya kupokea taarifa za tukio hilo walianza kufuatilia hatua kwa hatua kwa kuwashirikisha viongozi wa wilaya na masheha na wakagundua kweli tukio hilo limefanyika.  “Nilipopata tu taarifa hizi kuwa kuna mtoto kabakwa basi moja kwa moja nikawatafuta wahusika mkuu wa wilaya na sheha tukafuatilia na kwenda kituoni na nikakuta tayari limeripotiwa na nikasema tuone kama tayari hatua zimechukuliwa kwa hivyo suala hili hatuwezi kuliwacha hivi hivi tu likapita kwa sababu serikali imetuagiza kufuatilia masuala kama haya ili yakomeshwe kabisa” alisema Bi Mauwa.
Alisema mbali ya kwenda kituo cha polisi kuweka ripoti ambapo alikuta tayari taarifa zimeshafika alifanya bidii ya kumtafuta mtuhumiwa na kuchukuliwa maelezo yake na msichana alipelekwa hospitali kwenda kufanyiwa utaratibu wa kuangaliwa ambapo madaktari walithibitishwa kuumizwa na kushauri kuanzishwa kutumia dawa za dharura za kuzuia maambukizi ya virusi vya ukimwi.
“Mtuhumiwa ni Askari wa kituo cha polisi cha Mkoani na alizungumza na mtoto huyo na kumtaka asimtaje kwa kuhofia kufukuzwa kazi ni dhahir tendo hili kalitenda.” alisema Afisa Mshamini huyo.  Bi Mauwa alisema jamii inapaswa kutambua kwamba hilo ni jambo baya na linatakiwa kukomeshwa katika jamii na kutoa wito kwa wananchi mbali mbali kutowaficha watu wanaotuhumiwa kufanya vitendo kama hivyo kwani vimekuwa vikinea katika jamii.
Hili ni tukio la pili kwa askari wa jeshi la polisi kukutwa na tuhuma kama hizi ambapo Pandu Ndame alidaiwa kumbaka mtoto katika kituo cha polisi cha Chwaka mwaka jana na kufukuzwa kazi baada ya kuthibitika kuwa alitenda kitendo hicho. Polisi huyo hakuwahi kushitakiwa katika mahakama kutokana na kukimbia nchini na kudaiwa kuhamia mikoa ya Tanzania Bara baada ya kutaka kushitakiwa katika mahakama ya kiraia.
Ndame alikuwa akichukua maelezo ya mtoto huyo ambaye alibakwa poribni wakati akitafuta nazi na baada ya kwisha kuchukua maelezo ya mtoto huyo naye alimbaka kwa mara ya pili ndani ya kituo cha polisi cha Chwaka.

Advertisements

12 responses to “Polisi Pemba adaiwa kubaka

 1. WAMEZOEA KUBAKA HAO. WATU WANGAPI WALIBAKWA NA ASKARI WA VIKOSI 2001 PEMBA NA HAKUNA LILIOKUA? HUKO KENGEJA ASKARI POLISI WALIWABAKA WATOTO WAWILI WA FAMILIA MOJA PIA HAKUNA LILOKUA. HAPO WETE ASKARI POLISI ALIMBAKA NA KUMPA UJAUZITO MTOTO WA DARASA LA KUMI. ALIMUOA WIKI MBILI NA KUMUACHA NA HAKUNA LOLOTE LILE LILOKUA.INAONEKANA KUBAKA NI MCHEZO WAO WA KAWAIDA HAO. HAYA TUONE NA HILI BASI NINI KITATOKEA KAMA HATUKUAMBIWA MTUHUMIWA KAKIMBIA KUMBE KAHAMISHWA MAENEO MENGINE.

 2. tumechoka na vitendo vya askari wa jeshi la polisi kuwabaka ndugu zetu na hakuna lolote linalo fanyika hali hii itaendelea hadi lini?

 3. kwa hakika kitendo hichi ni miongoni mwa matendo ambayo vyombo vya ulinzi vya Tanzania wamezoea kuvifanya kwa kuwa wana uhakika hawafanywi kitu badala yake viongzi wao husema hakuna ushahidi au adhabu inayotolewa ni kupewa uhamisho ili akafanye tena sehemu nyengine kama ilivyo kwa huyu John ambaye alishawahi kufanya hivyo Kengeja na matokeo yake alihamishiwa Mkoani sasa tunasubiri kama atapelekwa Chake au Wete. ila sisi wananchi tuna imani kubwa na kamanda wa polisi wa mkoa wa kusini Pemba ila hatuna imani na OCD Mkoani ambaye tokeo hili amelifumbia macho kwa kipindi kirefu mpaka Kamanda wa Mkoa aliposikia na kulifanyia kazi Tunamuomba ALLAH amzidishie imani hiyo

 4. Huyo john kazowea kutuharibia ndugu zetu hapo mkoani, huu ni mpango wa kanisa kutuharibia watoto wetu kimaadili kisha kuwaritadisha. Wazanzibar tuifuatilie kesi hii kwa karibu mno haki itendeke! Salma na waandish wenzako mutusaidie haki itendeke! Zanzibar itadumu kwa nguvu za Allah

 5. mimi naona hakuna haja ya kesi, wala ushahidi mahakamani huyo askari ni kunyongwa tu, hilo litakua fundisho tosha kwa vikosi vya ulinzi, au wananchi wachukue sheria mikononi mwao jinsi gani wampe adhabu, lakini wananchi na waminia watafanya kweli tu, ya kukumu ya kwanza kumuingilia yeye kinyume na maumbile yake halafu watamua wakichukua sheria mikononi mwao

 6. Jamani tuseme ukweli hii hali ya ubakaji imezidi siku hizi kama hakujachukuliwa hatua madhubuti basi hali itakua mbaya hapo baadae kwa sababu mtenda anakua huru na mtendewa pia mwengine anakua muoga wa kusema alicho fanyiwa ila akipatikana kama hawa kina john waadabishwe kwani itakua funzo kwa wengine au mtawaona wananchi wabaya kwa kujichukulia hatua mikononi mwao kwani sisi wananchi tunajua siku hizi kesi ikifika kwenye sheria hakuna liwalo kwahiyo tunakua na sisi hatuna imani na vyombo vya sheria. Nahisi kama viongozi wanachelea mtoto kulia wakae wakijua kuna siku watalia wao kwani dunia ni duara na maisha ni mzunguko!!!!!!!

 7. Pingback: Polisi Pemba adaiwa kubaka·

 8. Haya lazima yafanywe na polisi kwa kuwa Jeshi hili na taasisi nyengine za kiulinzi limeingia watu wasio waaminifu. Rafiiki siku moja alinambia mwenzake aliyecheza naye akakataa kusoma na akatumia udogo wake akiiba kuku aliajiriwa na kikosi kimoja cha SMZ. Ukisikia wafungwa wanatumia madawa ni kwa sababu akina huyu wamo. Mimi mwenyewe nimeshuhudiwa mara nyingi askari wa TPDF mwenye uniform ananunua bangi eneo la Mivinjeni Jangombe. Mtu kama huyu sidhani atakataa kutoa bunduki itumike kufanya uhalifu. Askari wengine nao hawasemeki- Polisi wa barabara ni mawakala wa waendesha dalala. Kuna vijana miongoni mwao wanasifika kwa kusaidia uhalifu wa barabarini uendelee. nenda darajani utasikia ” wewe mwite ——————- kama unakesi.” Mimi niligongwa na nakijana kwa kiburi alimpigia askari polisi akimtaka aje anisulubu kama Mesiah alivyosulubiwa. Kijana huyu pasi na kujua mimi niani alijiamini kama vile anahisa katika jeshi la polisi. Matatizo ya kimfumo pia yanachangi kufanya jeshi la polisi liwe hivi lilivyo! Ivo iweje mtu akae pahala pamoja pa kazi hadi aowe na watoto zake waolewe- ivo iweje askari akae mahali hata awe mwenjeji kiasi cha kujiami kuingia mitaani na kuharibu watoto kama huyu wa Mkoani. Ivo inakuwaje Askari azoane na wahalifu kiasi cha kumtumia kama wakala kama hawa kina ———— watumiwao na daladala mjini Unguja. Askari polisi wanaivunjia heshima nchi kwa ripoti za wageni nje zinaitaja nche yetu kama safe heaven ya wala rushwa na polisi ni miongoni mwao!. Mimi ningekuwa kiongozi wa Dola ninge tafuta mfumo mwengine wa kuajiri polisi lakni pia mfumo mwengine wa kuendesha jeshi hilo! Kuna watu ndani jeshi la posi ni wazuri na hawa wangekuwa wasahari wangu !

 9. Hivi kwanini kusiazishwe sheria ya kuwapiga risasi wabakaji na kwa huyu mtoto wa pemba kwa ufahamu wa haraka nimeona na mwanafunzi ila anafanya kazi za ndani kwa huyo kitangi cha ajabu ni kuwa wazee wa kiislamu walimruhusu vp mtoto wao kufanya kazi kwa mtu ambaye nahisi atakua si muislam kutokana na hilo jina lake umaskini wa watu wa pemba unawafikisha pabaya wito wangu serikali iboreshe hali za vipato vya wananchi wake

 10. Watu kama hawa hawafai katika jamii yetu. Wasifumbiwe macho. Heko viongozi wa jeshi la polisi kwa hatuwa muliochukuwa.

 11. Serikali chukueni sheria juu ya hawa waliopewa jukumu la kuwalinda raia lakini halafu wakawa wao ndio wanaowahujumu raia badala ya kuwalind a au wao hawajui majukumu yao.?

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s