Katibu wa Baraza la Wawakilishi aapishwa

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk.Ali Mohamed Shein,akimuapisha Yahya Khamis Hamad,kuwa Katibu wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar,jana baada ya kumteuwa
kushika nafasi hiyo,hafla ya kiapo ilifanyika Ikulu Mjini Zanzibar

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein leo amewaapisha Katibu wa Baraza la Wawakilishi Yahya Khamis Hamad na Luteni Kanali Mohammed Mwinjuma Kombo kuwa Mkuu wa Kikosi cha Valantia Zanzibar. Hafla hiyo ilifanyika Ikulu mjini Zanzibar na kuhudhuriwa na viongozi mbali mbali akiwemo Makamu wa Kwanza wa Rais Maalim Seif Sharif Hamad, Makamu wa Pili wa Rais Mhe. Balozi Seif Ali Idd, Spika wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Pandu Ameir Kificho, Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe.Omar Othman Makungu na Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman.

Wengine ni Waziri wa Nchi Afisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Mwinyihaji Makame,Waziri wa Nchi Afisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mhe. Mohammed Aboud, Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mhe. Abdalla Mwinyi Khamis, Meya wa Manispaa ya Mji wa Zanzibar, Mstahiki Khatib Abdulrahman Khatib, Wakuu wa vikosi vya Ulinzi na Usalama pamoja na viongozi wengine.

Viongozi hao waliteuliwa jana pamoja na viongozi wengineo ambapo kabla ya hapo Hamad alikuwa Mwanasheria wa Baraza la Wawakilishi ameteuliwa kujaza nafasi ya Ibrahim Mzee alieteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP).

Wengine walioteuliwa hapo jana tarehe 25 Machi mwaka huu, ni Abdulghani Himid Msoma kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Viwanja vya ndege Zanzibar na Saada Thani kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Elimu Zanzibar.

Tunawatakia kheri wateule hawa wapya inshaallah watafanya kazi kwa haki na uadilifu mkubwa.

Tafadhali weka maoni yako

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s