Zanzibar kupewa tunzo ya utalii

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Uwekezaji wa Miradi ya Utalii Zanzibar (ZATI) Abdulsamad Said Ahmed

 ZANZIBAR imefanikiwa kuwa mshindi wa kwanza wa tunzo ya Utalii nchini Russia kwa mwaka 2011, ‘Star Travel.ru 2011’. imeelezwa. Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari, Mkurugenzi Mkuu wa Kamisheni ya Utalii Zanzibar, Ali Khalil Mirza, amesema amepokea taarifa hiyo kutoka Ubalozi wa Tanzania nchini Russia, ikielezea Zanzibar kuchaguliwa kuwa mshindi wa tuzo hiyo, kama eneo lililo bora kwa shughuli za kiutalii barani Afrika.

Tuzo kama hiyo hushindaniwa kila mwaka kwa maeneo yalio bora zaidi kwa shughuli za kiutalii barani Afrika, ambapo watalii na waongoza watalii wa nchi hiyo hutembelea nchi mbali mbali.

Mirza alisema kuwa kinyang’anyiro cha mashindano hayo kiliwashirikisha maeneo 23 yalio bora zaidi kwa shughuli za kiutalii, isipokuwa nchi ya Misri haikushirikishwa ambayo haikushirikishwa katika mashindano hayo lakini haijaelezwa kwa sababu gani.

Mkurugenzi huyo alisema tayari tuzo hiyo imekabidhiwa kwa Ubalozi wa Tanzania nchini humo katika na kufanyika hafla maalum ilioambatana na kuanza kwa maonyesho ya Kimataifa ya Utalii ya nchi hiyo.

Mirza alisema ushindi wa tuzo huyo unatokana na msukumo mkubwa wa Ubalozi wa Tanzania nchini Russia pamoja na hatua ya Kamisheni hiyo ya Utalii kufanya ziara maalum ya kuutangaza utalii wa Zanzibar mnamo 2009. na kuelezea kwamba Zanzibar imepiga hatua kubwa katika sekta ya utalii ambapo kwa sasa ndio sekta inayotegemewa katika kutoa ajira nyingi kwa vijana na kuchangia pato la taifa.

Aidha Mkurugenzi huyo alisema makubaliano yaliofikiwa kati ya Kamisheni ya Utalii na Makampuni ya kutembeza watalii yamelifanya soko la Utalii nchini Russsia kuimarika, ambapo wastani wa watalii 300 hufika nchini kila mwaka tangu wakati huo.

Alieleza kuwa hayo ni mafanikio makubwa kwa soko la utalii nchini Russia kwa kuzingatia watalii wanaokuja ni wale wanaotumia zaidi, ambao hufikia katika Hoteli zenye hadhi za juu kama vile Plan Hotel,Lagema,Green of Zanzibar na The Residents na nyingi nyenginezo.

Aidha alisema Kamisheni yake ina matumaini makubwa kuwa ifikapo 2013 idadi ya wataalii kutoka nchi hiyo itaongezeka, hususan pale Shirika la ndege la Uturuki litakapoanza kufanya safari zake moja kwa moja hadi Zanzibar, hasa kwa kuzingatia watalii hao hivi sasa hutumia usafiri wa Shirika la Emirates, na kutembelea kwanza katika Mbuga za wanyama na hatimae kuja Zanzibar.

Mkurugenzi huyo alivitaja baadhi ya vigezo muhimu vinavyozingatiwa katika kumpata mshindi wa tuzo hiyo, kuwa ni pamoja na hali ya usalama, na amani kutawala katika nchi husika na kufikiwa kwa matarajio ya wageni, vivutio vya utalii ikiwemo michezo mbali mbali (pwani na ufukweni), huduma katika mahoteli pamoja na tamaduni za wenyeji wa nchi husika vyote hivyo huzingatiwa katika mashindano hayo.

Akizungumza na Gazeti hili Mwenyekiti wa Jumuiya ya Uwekezaji wa Miradi ya Utalii Zanzibar (ZATI) Abdulsamad Said Ahmed alisema Zanzibar inastahiki kupewa tunzo kama hiyo kwani ina vigezo vya aina zote katika kufikia ushindi huo.

Akivitaja vitu ambavyo vipo Zanzibar na vinawavutia watalii wengi na kusababisha kuja kuona ni pamoja na amani na utulivu uliyopo Zanzibar, historia yake, utamaduni na silka wa wazanzibari, fukwe zake, ukarimu na utunzaji wa mazingira ni miongoni mwa vitu vichache ambavyo vinachangia kuifanya Zanzibar kuwa ni mshindi na kuzipita nchi nyingi ambazo vinapata watali.

Alisema Zanzibar ina kisiwa cha misali ambacho nacho kimejaaliwa kuwa na vivutio mbali mbali ikiwemo utunzaji wa rasilimali za bahari kama vile kobe, matumbawe ya kila aina (coral reef) na nk.

Ahmed alisema nchini Ushelisheli au kisiwa cha Moritius ni kizuri lakini ukiacha fukwe na mambo machache ambayo yapo katika kisiwa hicho hakuna jambo jengine ambalo linaweza kuwavutia wawekezaji au watalii kwenda katika visiwa vivyo.

Mwenyekiti huyo alisema pia Tanzania Bara wana mlima wa kilimanjaro, Ngorongoro na Serengeti lakini ukilinganisha vivutio walivyonavyo haviwezi kuifikia Zanzibar kwani Zanzibar imejaaliwa kuwa na kila kitu katika fukwe zake.

Hata hivyo Mwenyekiti huyo alitoa wito kwa serikali kutizama na kuzifanyia kazi changamoto zilizopo ambazo ni pamoja hali ya usalama kwa wawekezaji na watalii, ukosefu wa umeme wa uhakika, matatizo ya maji, na kuhimiza usafi wa maeneo ya miji na vijiji ili hali ya usafi iweze kuwavutia wawekezaji na watalii zaidi. 

 

Advertisements

2 responses to “Zanzibar kupewa tunzo ya utalii

  1. The russian clients are comming. As mentioned most of them are staying at PLAN HOTELS ( Gemma Del Est, Neptune Pwani, Dream Of ZNZ, and Mapenzi Beach). I have personally heard mant Tour Operators in Zanzibar complain against the policy of these hotels. When I talked to them, they said that PLAN HOTEL policy in regards to Accomodation Rates they provide to Local Tour Operators is not goood and is aiming at Killing the Local Tour Operators. Amazingly, One Zanzibari company showed me an examplke of the contract rates his company is given by PLAN HOTEL , then he showed me an example of the rates one of European company is given, I was really shocked to see that a Zanzibar Company is given very high rates compared to the foreign company !!

    Most of the Zanzibari Tour Operators have been crying against this behaviour specifically by PLAN HOTELS but no one in the government is trying to help this local companies to get competitive rates !!

    Can any one in the government help these local companies please?

  2. WAZANZIBAR TUUNGANE KUDAI UHURU WA ZANZIBAR KUTOKA MIKONI MWA MKOLONI WA TANGANYIKA. Zanzibar bila ya kuwa huru haiwezi kuendelea milele.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s