Ukombozi wa Zanzibar wazidi kuimarika

Baraza la Katiba Zanzibar ambalo limeundwa chini ya taasisi tano kwa kushirikiana na Jumuiya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar (JUMIKI) iliyojumuisha taasisi zote za dini ya Kiislamu hapa Zanzibar leo wamefanya mhadhara juu ya kutoa elimu ya uraia, kwa kwanza kulia ni Kiongozi wa Jumuiya ya Maimam Ustadh Farid Hadi, Mjumbe wa Baraza la katiba Wakili Awadh Ali Said, Mwenyekiti wa baraza la katiba Pro. Abdul- Shareef, Amiri wa Uamsho Mselem Ali na Sheikh Suleiman Al Kindy ambaye ni Mjumbe wa Jumuiya ya Uamsho

 

Kwa upande wa Zanzibar kumezaliwa hasara nyingi kubwa zikiwemo Kupoteza mamlaka yake ya kutambulika duniani kama ni nchi, ambayo mamlaka hayo yamo mikononi mwa Tanzania Bara (Tanganyika), na kutokuwa na mamlaka ya kuhudhuria vikao vya Kimataifa mfano UN,AU,CW, East Africa Community nk. Hasara nyengine ambayo Zanzibar inaipata ni kupoteza uwezo wake wa kufunga mikataba ya Kimataifa, pia kutokuwa na mamlaka ya kujiamulia ni nchi gani au Taasisi gani ingependa kuwa na mahusiano nayo au kutokuwa na mahusiano nayo ambapo mambo hayo ndio msingi mkuu na chachu ya mafanikio katika nchi yoyote duniani na ndiyo yanayopelekea kuifanya nchi kutambulika kuwa ni nchi kamili , kinyume chake ni kuwa na nchi dhaifu isiyotambua ulimwengu ukoje na unakwendaje.

Toleo No 1 23 March 2012

MIAKA 48 YA MUUNGANO WA TANGANYIKA NA ZANZIBAR, WAZANZIBAR NA MAONI YAO.

Na Suleiman Al Kindy

Utangulizi

Imetulazimu kutoa mawazo haya kwa kuzingatia ibara ya 18(1) ya Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 tolea la 2010, inayosema kama ifuatavyo-:

Bila ya kuathiri sheria ya nchi, kila mtu yuko huru kuwa na maoni yoyote na kutoa nje mawazo yake, na kutafuta kupokea na kutoa habari na dhana kupitia chombo chochote,bila ya kujali mipaka ya nchi,na pia ana uhuru wa mawasiliano yake kutoingiliwa kati.”

Katika miaka yote 48 ya umri wa muungano wa nchi mbili zilizokuwa huru, (Jamhuri ya Watu wa Zanzibar na Tanganyika), hakuna shaka ya kwamba Zanzibar imekuwa ikiendelea kulalamika na kuonesha kwa vitendo juu ya kutoridhishwa kwake na muundo na mfumo wa muungano huo, pamoja na usimamiaji wake na utekelezaji wake.

Kwa msingi huo,hayo ndio yaliyozaa Muungano ambao ni kero kwa Wazanzibari walio wengi., ni wazi kwamba kuna kila dalili, kasoro na matendo yaliyowazi mengi yaliyojaa shaka inayotulazimu tuamini kuwa kuna dhamira ya makusudi ya kuifikisha Zanzibar pale pasipo takiwa na Wazanzibari walio wengi.

Miongoni mwa mambo yaliyo na athari mbaya na machungu sana na matendo yaliyowazi na yaliyojaa shaka kwa nchi ya Zanzibar na Wazanzibari wenyewe, ni pale siku chache tuu baada ya Muungano huo tumeiona Tanganyika ikihaulisha Mamlaka yake kwa serikali ya Jumhuri ya Muungano,na Zanzibar nayo ikisalimisha mamlaka yake kwa Jamuhuri ya Muungano hiyo hiyo ya Tanzania katika namna ambayo Wazanzibari tunaamini kuwa ni mbinu na hila za kuipokonya Zanzibar mamlaka yake (Soverenity), na hapo ndio ukawa mwanza wa safari ya kuvunjwa nguvu za kimamlaka kwa nchi ya Zanzibar.

Kitendo hicho cha Tanganyika kuhaulisha mamlaka yake kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kimezaa faida mbili kubwa kwa Tanganyika na kusababisha hasara nyingi kwa Zanzibar.

Faida ambazo Tanganyika imezipata ni kama zifuatazo ,Kwanza kuivunja nguvu Zanzibar za Mamlaka, Pili kujikweza na kujipatia maguvu ya kimamlaka ndani ya Katiba ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

(a) Maamlaka ya Raisi wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

ndani ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Kwa mfano katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Ibara ya 33(2) inasema kama ifuatavyo-:

Raisi atakuwa mkuu wa nchi , kiongozi wa Serikali na amiri jeshi Mkuu’

Ibara ya 34 (1) pia inasema kama ifuatavyo-:

Kutakuwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano ambayo itakuwa na Mamlaka juu ya mambo yote ya Muungano katika Jamhuri ya Muungano,na pia juu ya mambo mengine yote yahusuyo Tanzania Bara (Tanganyika)”

Ibara ya 34 (2) inasema kama ifuatavyo-:

Mamlaka ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano yatahusu utekelezaji na hifadhi ya katiba hii na pia mambo mengineyo yote ambayo Bunge lina mamlaka ya kuyatungia Sheria”

Pia ibara ya 34(3) inasema kama ifuatavyo-:

Mamlaka yote ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano juu ya mambo yote ya Muungano katika Jamhuri ya Muungano,na pia juu ya mambo mengineyo yote yahusuyo Tanzania Bara,yatakuwa mikononi mwa Raisi wa Jamhuri ya Muungano”

Ndugu msomaji, ukiitizama ibara ya 33(2) utagundua kuwa maaana yake ni kwamba huyo Rais ndiye mwenye maamlaka mengineyo yote ya Tanzania Bara (Tanganyika), pia soma kwa makini ibara ya 34(1) (2) na (3), hapo ndipo utagundua kuwa Tanzania Bara (Tanganyika) ipo na ina maguvu kamili ya ndani ikiwemo kuiamulia Zanzibar juu ya mambo yake ya ndani, na nje ya nchi, kwa kumpata Rais aliye amiri jeshi Mkuu na ambaye atasimamia mambo yote ya Tanzania Bara (Tanganyika) kwa maana hiyo kwa nini tusiamini kuwa Tanzania Bara (Tanganyika ) ndio Jamhuri ya Muungano yenyewe?, tumekokotwa kwa mtindo huu kwa muda wa miaka isiyopungua 48.

Kwa upande wa Zanzibar kumezaliwa hasara nyingi kubwa zikiwemo Kupoteza mamlaka yake ya kutambulika duniani kama ni nchi, ambayo mamlaka hayo yamo mikononi mwa Tanzania Bara (Tanganyika), na kutokuwa na mamlaka ya kuhudhuria vikao vya Kimataifa mfano UN,AU,CW, East Africa Community nk.

Hasara nyengine ambayo Zanzibar inaipata ni kupoteza uwezo wake wa kufunga mikataba ya Kimataifa, pia kutokuwa na mamlaka ya kujiamulia ni nchi gani au Taasisi gani ingependa kuwa na mahusiano nayo au kutokuwa na mahusiano nayo ambapo mambo hayo ndio msingi mkuu na chachu ya mafanikio katika nchi yoyote duniani na ndiyo yanayopelekea kuifanya nchi kutambulika kuwa ni nchi kamili , kinyume chake ni kuwa na nchi dhaifu isiyotambua ulimwengu ukoje na unakwendaje.

Hapo ndipo utapoona kwa ubainifu wa mambo yalivyo kama tulivyonukuu maandiko ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano, ibara tulizotangulia kizielekeza zinaonyesha wazi na kubainisha upamoja wa mamlaka hizo juu ya mambo yote ya Muungano katika Jamhuri ya Muungano na pia mambo yote yanayohusu Tanzania Bara( Tanganyika).

Ndugu msomaji, hivyo utaona kuwa upamoja wa mamlaka hizo ambazo ziko mikononi mwa Rais wa Jamhuri ya Muungano ni kwa kiwango gani Tanganyika inafaidika kupitia upamoja huo.

Kwa maaana hiyo Katiba hiyo moja ni ya Muungano na ndio yenye mamlaka ya Tanzania Bara (Tanganyika) ambayo Tanzania Bara (Tanganyika) ndio yenye mamlaka na Katiba hiyo.

(b) Mamlaka ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

ndani ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Katika ibara ya 64(1) inasema kuwa:-

Mamlaka yote ya kutunga sheria juu ya mambo mengine yote yahusuyo Tanzania Bara (Tanganyika) yatakuwa mikononi mwa Bunge”

Ndugu msomaji tunatakiwa tufahamu ya kuwa mamlaka hizo mbili (Bunge na Rais) ndizo zinazosimamia na kutekeleza kuitendaji kwa wizara zote za Tanzania Bara ( Tanganyika).

Vile vile ikumbukwe kuwa mamlaka hizo ndizo zinazotambulika kuwa ni kiwakilishi cha nchi duniani, Rais ndio mamlaka pekee inayowakilisha vikao vyote vya juu vya kimataifa (rejea ukurasa no 3 hapo juu).

Ibara ya 63(3) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inasema kuwa-:

Kwa madhumuni ya utekelezaji wa madaraka yake Bunge laweza-:

(e) “Kujadili na kuridhia mikataba yote inayohusu Jamhuri ya Muungano na ambayo kwa masharti yake inahitaji kuridhiwa”

Mamlaka haya ya Bunge ni sawa na mamlaka aliyonayo Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (rejea ukurasa no 2-4 hapo juu).

Hizo ndizo mamlaka zinazosimamia na kutekeleza kiutendaji mambo mengineyo ya Tanzania Bara (Tanganyika).

Kwa uchanganuzi huu ni kwa nini tusiamini kuwa Tanzania Bara (Tanganyika) ni nchi ndani ya Tanzania na pia ni nchi nje ya Tanzania kwa sababu ina sifa za kisheria ndani ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayotoa fursa ya kuzipa mamlaka hizo mbili kuu (Bunge na Raisi) kusimamia mambo yake.

Kwa kigezo cha kukosa sifa hizo ndio kuliifikisha Zanzibar kubainishiwa hadharani kwamba “Zanzibar si nchi”, hili ndio tamko la mwanzo la Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, hivyo ukijiuliza ndugu msomaji unapoambiwa Zanzibar si nchi maaana yake ni nini kinyume chake? je inamaanisha ni Mkoa? au Jimbo? jawabu zuri unalo wewe ndugu msomaji.

Kisha ikafuatia kauli ya pili kuwa “Zanzibar ni nchi ndani ya Tanzania lakini si nchi nje ya Tanzania”, hivyo duniani kuna utaratibu wa kuwa na nchi ndani ya nchi? au Wazanzibari tumependelewa? Je tutamini vipi kuwa kauli hizo mbili kuwa hazina lengo na dhamira ya majibu ya masuala tuliyoyauliza hapo juu?

Viongozi hao wamejiamini na kukinai kwa uhakika juu ya matamshi yao hayo kwa kutokuwa na shaka wala wasiwasi na kauli hizo, kwa sababu Zanzibar zamani kabla ya leo ilishapotezewa vigezo na sifa hizo ndani ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, huku tukiiona Tanzania Bara (Tanganyika) ikikweya juu ya mabega ya Jamhuri ya Muungano kikatiba kutekeleza malengo yake yote ya kitaifa na kimataifa.

Ndugu msomaji mimi na wewe tutakubaliana ya kwamba Serikali ya Muungano haina utaratibu unaokubalika Kisheria wa kuwakutanisha katika vikao vya pamoja vya walioungana (Tanganyika na Zanzibar) vitakavyojiamulia kila upande kipi kiongezwe na kipi kipunguzwe kwa makubaliano ya nchi huru zilizoungana, hilo halijawahi kutokea katika historia ya Muungano huu kwa sababu halina miguu ya kusimama kisheria.

Sasa hapo ndipo yanapozuka masuala yafuatayo katika vichwa vya Wazanzibari;

 1. Je ni kwa vielelezo gani ambavyo vinaweza kutufanya sisi Wazanzibar kwamba tuamini kuwa kero za Muungano pamoja na utata uliojaa wingi wa matukio kwamba hivyo au hayo hayakupangwa kwa makusudi?

 2. Je ni hoja gani tunaweza kuelimishwa kwamba kero zote za Muungano ambazo ni mzigo mzito kwa Zanzibar zimetokea kwa bahati mbaya?

 3. Je tunatakiwa tuamini kuwa haya na mengineyo yote yanayolalamikiwa na Wazanzibar ni dhana potofu au ni hakika?

 4. Je kama ni bahati mbaya au ni kasoro za Kisheria au kuna dhamira njema juu ya hayo ni sababu gani iliyosababisha kukosa ufumbuzi na utatuzi au kudhihirika kwa nia njema kwa muda wa nusu karne sasa ?

 5. Kwa nini walamikaji wa kimaslahi wa Muungano huu iwe ni upande mmoja nayo ni Zanzibar tu?

Wazee wetu wa hikima wanasema “Mwanadamu humgeuza paka akawa chui pindipo tu atapoamua kumfanyia madhara paka huyo ndani ya eneo la chumba kilichofungwa milango”,

Pia Wataalamu wa Saikologia wanasema kuwa kadiri mwanadamu utakavyo mkosesha haki zake huku akiwa ametambua kuwa unamkosesha haki yake hiyo inayomuwajibikia elewa kwamba atabuni mbinu za kutegua kwa kila kilichotegwa hata kama uteguwaji wake utamletea madhara.

Huu ni wakati wa kuirejeshea Zanzibar Mamlaka yake ili viongozi waliotuelimisha kuwa Zanzibar si nchi wawe na kauli na tamko moja tu lisilo kuwa na upungufu wala ufafanuzi utakaogeuza maana , ya kwamba “Zanzibar ni nchi nje ya Tanzania”’

Hilo linawezekana tukiamuwa kwa Umoja wetu Wazanzibar.

Kwa kulitambua suala muhimu la umoja Katiba ya Zanzibar inathamini suala hilo la umoja na kutuongoza kama inavyojieleza katika ibara ya 23(3)-

Watu wote watatakiwa na Sheria kulinda vizuri mali ya Zanzibar na kwa pamoja kupiga vita aina zote za uharibifu na ubadhirifu na kuendesha uchum wa Zanzibar kwa makini kama watu ambao ndio waamuzi wa hali ya baadae ya Taifa lao”

Pia ibara 23(4) inasema kuwa:-

Kila Mzanzibar ana wajibu wa kulinda,kuihifadhikudumisha uhuru,mamlaka,ardhi na Umoja wa Zanzibar”.

Pia ibara 9(a) inasema kuwa:-

Mamlaka ya kuendesha nchi ni ya Wananchi wenyewe ambapo nguvu na uwezo wote wa Serikali kufuatana na katiba hii utatoka kwa wananchi wenyewe”

Kwa mantiki pamoja na maoni hayo tunapenda kuwahimiza Wazanzibar kuwa kuigomboa Zanzibar kutoka katika mfumo ulio na Kero ni jambo linalowezekana ikiwa patapatikana umoja miongoni mwetu pamoja na kuamini kuwa kulizungumzia suala la Muungano wa Zanzibar na Tanganyika na kutoa mawazo juu ya kutatua matatizo ya Muungano kwa nguvu za Hoja ni wajibu wa kila Mzanzibar na kufanya hivyo ni kukuza Demokrasia


Advertisements

8 responses to “Ukombozi wa Zanzibar wazidi kuimarika

 1. Pingback: Ukombozi wa Zanzibar wazidi kuimarika·

 2. Aslam aleikum,
  Ndugu waandishi au wenye mtandao kinachotakiwa hapa ni habari ni nini kimezungumzwa na sisi uliopo mbali tufahamu sio picha. Picha haitusaidii kitu wala haina faida yoyote kama hakikuelezwa kilicho zungumwa.

 3. a.aleykm?
  nakubaliya na wewe ndugu yangu mchangiaji wa mwanzo na nashauri kwa viongozi wa sheria na jumuia zote kutoa tamko ramsi juu ya serikali kwamba wazanzibar tunahitaji kura ya maoni kwanza juu ya muungano , tusiseme tu kila siku vitendo muhimu wakuuu wetu..
  Ahsanetini

 4. Inavyoonekana tatizo kubwa ni MUUNGANO WENYEWE. Ulilazimishwa kwa mizengwe bila ya ridhaa kwa kupitia elimu ndogo aliyokua nayo Karume pamoja na vitisho toka mataifa ya Magharibi kua angepinduliwa na aliowapindua. Dunia inakwenda mbele na sasa wananchi wanaona matatizo na kero juu ya Muungano wenyewe. UNAWEZA KUWAPUMBAZA BAADHI YA WATU KWA WAKATI FULANI TU LAKINI HUWEZI KUWAPUMBAZA WATU WOTE WAKATI WOTE. Tatizo la viongozi wetu wa upande wa Zanzibar ni wanafiki, wanajali maslahi yao binafsi zaidi hata kama nchi inachukuliwa na mfano mzuri ni suala la ukanda wa bahari wa EPZ jinsi lilivyotekelezwa. Kama tunaowategemea viongozi ndo wasaliti tutaendelea kua kolono la Tanganyika milele. Athari ziko waziwazi hasahasa Unguja na hali hii inaendelea. Nafasi za ajira za Muungano wanapewa wakoloni na tunaona. Hata mfagiaji au mpishi wa chai kwenye taasisi za muungano lazima atokee Tanganyika. Baya zaidi ni hayo mafuta yanayotegemewa kuchimbwa yatawafaidisha Mafisadi wa upande mmoja wa muungano kwani hivi sasa ukiangalia hilo shirika ambalo limepewa dhamana ya mafuta TPDC sio la muungano na hakuna hata mzanzibari mmoja na hao tunaowaita viongozi wa Zanzibar wamekaa kimya kwa sababu wao na watoto wao wanafaidika na hali hiyo. Watoto wao wote wanasoma shule na vyuo vya Ulaya ile waje kuendelea kututawala kama baba zao. Mifano iko wazi Malima, Makamba, Mwinyi, Nnauye, Kawawa nk. Nini tufanye? Mimi kwa uono wangu mfupi nahisi Wazanzibari wakati umefika kwa kila mmoja kusema SASA UKOLONI BASI na njia nyepesi ni kuwataka WAWAKILISHI wetu ambao wanaonekana kua makini kutaka Wazanzibari waulizwe kama wanautaka MUUNGANO au la na kama WATANGANYIKA nao watataka hilo au la shauri lao. Kama hili ni gumu basi itabidi tusubiri wakati wa Uchaguzi na kuanza mkakati wa kuvingoa vyama vyote vinavyounga mkono mfumo huu wa ukoloni kwa utaratibu wa kura. Suala la elimu juu ya masuala ya Katiba ni muhimu liendelee hasa kwenye maeneo ya mashamba ambako Wazanzibari wengi wamekua wakidanganyika kwa vitu vidogo kama kofia na fulana au kuambiwa Warabu watarudi tena kuwatawala. Hivi mwarabu gani mwenye shida ya kurudi nchi hii ambayo imejaa dhiki na mashaka ya kila aina? TUSEME BASI KWA MKOLONI.

 5. na mimi nakubaliana na wewe mia fil mia, ila nadhani umefika wakati taasisi zote ziungane then watuunganishe wananchi ili tuishinikize serikali yetu ikubaliane na msimamo wa wananchi wake badala ya kung’ang’ania misimamo ya kivyama, vyama havikuwepo, vipo na baadae vitaondoka ila Zanzibar itakuwepo mpaka mwisho wa dunia kwa hiyo nazishauri hizi jumuiya ziitishe hata maandamano ambayo tutabaki barabarani mpaka serikali ikubali kutuletea kura ya maoni juu ya muungano kwanza.

 6. NYINYI WAZANZIBALI WACHENI KUJIDANGANYA KUWA MUNA NCHI, ZANZIBAR SI NCHI BALI NI MKOA WA TANZANIA. Bila ya watanganyika zanzibar isingeripata uhulu kutoka kwa mwalabu, watanganyika ndio waliofanya MAPINDUZI ya kumuondoa mwalabu zanzibar. Kwahivyo, tunahaki ya kuwa na mateka wetu zanzibar. Shukulun sisi wanaume kuwapatia uhulu NYINYI KAZI YENU KUNYWA ULOJO NA KUFILANA TU HAMUWEZI KITU.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s