ZECO yashutumiwa kwa rushwa

Mwakilishi wa Jimbo la Kiwani (CUF) Hija Hassan Hija

Mwenyekiti wa Kamati ya Maendeleo na Wanawake wa Baraza la Wawakilishi Hija Hassan Hija amekusudia kupeleka hoja binafsi ya ubadhirifu na rushwa unaofanywa katika shirila la umeme zanzibar katika kikao cha baraza la wawakilishi kitakachofanyika hivi karibuni.

Mwakilishi huyo amelishutumu Shirika la umeme Zanzibar (ZECO) akidai kuhusika na ubadhilifu, ufisadi na rushwa zinazotokana na uungwaji wa umeme kienyeji na watendaji wasio waminifu bila ya kulihusisha shirika hilo.

Kuali hiyo ameitangaza wakati akizungumza katika mkutano wake na waandishi wa habari huko katika ukumbi wa Idara ya habari (maelezo) Zanzibar ambapo alisema wafanyakazi wa shirika la umeme wamekuwa wakijiungia umeme kiholela na kuwepo kwa wafanyakazi walioajiriwa kwa ubaguzi akimaanisha ni watoto wa wakubwa na watendaji wa shirika hilo.

Hija alisema uchunguzi uliofanywa umebaini kuwepo kwa rushwa na ubadhirifu wa fedha za umma na ndio sababu iliyopelekea na kumsukuma kutaka kupeleka hoja binafsi kuliomba baraza la wawakilishi kuunda tume ya kuchunguza ubadhilifu huo.

“Hatuwezi kukubali fedha za umma zitumike ovyo hili ni jambo kubwa linalopaswa kuundiwa tume ya kuchunguza ili kubaini hasara za ubadhilifu uliopo katika shirika hilo ”alisema Hija.

Mbali ya ubadhirifu huo unaofanywa lakini pia kuna tatizo la utendaji mbovu wa watendaji amabo kwa kiasi kikubwa wanaonekana kuwa hawana uadilifu katika kazi zao na kusababisha matatizo na kuzorotesha ufanisi wa shirika hilo.

Alisema baadhi ya watendaji wamekuwa wakipoteza mapato ya serikali kutokana na ugawaji wa umeme ambapo mara nyingi imeonekana kuwa wanaofanya vitendo hivyo hawana uaminifu katika utendaji wa kazi zao.

Mwakilishi huyo ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya baraza la wawakilishi alisema ugawaji huo wa umeme unasababisha fedha kutoingia katika mfuko wa shirika hilo na badala yake fedha huigia katika mifuko ya watu binafsi.

Akizungumzia kero za wananchi wenye kutaka kuungiwa umeme Mwakilishi huyo alisema wateja wanalalamikia kutoa fedha zao za kutaka kuungiwa umeme lakini hucheleweshewe huduma hiyo kutokana na kuwa hawana uwezo mkubwa lakini wale wenye uwezo mkubwa hufanyiwa haraka huduma hiyo.

Akitaja jambo jengine ambalo hufanyika ndani ya shirika hilo mwakilishi huyo alisema ni jinsi taratibu za ajira zisivyozingatiwa ambapo watu ambao hufanyiwa usajili huachwa na kuchukuliwa watu mbao wahakuwemo katika usajili huo.

Suala la majenereta, Mwakilishi huyo alisema majenereta hayo yalionunuliwa kwa ajili ya kutoa huduma mbadala iwapo umeme utakatika lakini yamekuwa yakiitia hasara kubwa serikali kutokana na kuwa hayatumiki kwa madai kwamba yanapotumika hutumia mafuta ambayo ni ghali sana.

“Haya yale majenereta yaliyonunuliwa kwa gharama kubwa yamekuwa kama ni mapambo tu na ni mzigo mkubwa kwa serikali maana hayasaidii na yanatia hasara shilingi milioni mia taano kwa mwaka kwa ajili ya kufanyiwa (service) hili ni jambo la kushughulikiwa”alisema Mwakilishi huyi.

Hata hivyo Shirika hilo la umeme linakamiliwa na deni kubwa ambalo ni malimbukizo linalodaiwa na shirika la umeme la TANESCO.

“Ni matatizo makubwa ZECO linadaiwa fedha nyingi sana na TANESCO na haijulikani deni hilo la malimbukizo litalipwa lini” alihoji mwakilishi huyo.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s