Meneja wa ZECO awekwa kiti moto mbele ya Dk Shein

Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohd Shein akibadilishana mawazo na Waziri wa Ardhi Makaazi Maji na Nishati, Ali Juma Shamhuna huko katika Uzinduzi wa Mradi wa Maji safi na salama huko Selem Mkoa wa Mjini Magharibi ikiwa ni Mfululizo wa Ziara ya Rais Katika Mkoa huo.

Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohammed Shein amemtaka Meneja wa Shirika la Umeme Zanzibar (ZECO), Hassan Ali Mbarouk kutoa maelezo ya kina mbele yake kutokana na kushindwa kuweka transfoma ya kusambaza umeme katika shule ya Kianga iliyopo wilaya ya Magharibi, Unguja.

 

Rais Dk. Shein aliyasema hayo leo katika uzinduzi wa mradii wa maji huko Selem, Mfenesini, Mkoa wa Kaskazini Unguja, ikiwa ni muendelezo wa ziara zake za kuitembelea miradi ya maendeleo  na  shughuli nyengine za kichama na serikali Unguja na Pemba, ziara iliyoanza leo rasmi.

 

Hayo yamefanyika jana katika ziara ya kutembelea maeneo mbali mbali katika mkoa wa Mjini Magharini ambapo Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Abdallah Mwinyi Khamis  alipokuwa anajibu risala ya kamati ya shule hiyo juu ya shule kutopata huduma ya umeme licha ya Dk Shein kutoa msaada wa shilingi milioni 3.6 za kununulia transfoma mwaka 2004.

 

Tukio hilo watendaji wakuu wa serikali kusemwa mbele ya hadhara ya watu linakuja siku chache baada ya Makamu wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad alipomsema Waziri wa Habari Abdilahi Jihad Hassan kwa kushindwa kutoa maelezo ya kina juu ya kuhamishwa wahariri wa wawili wa shirika la utangazaji zanzibar ZBC mbele ya wafanyakazi wa wizara hiyo hapo Bwawani juzi.

 

Katika risala ya kumkarisha Rais Shein katika uwekaji wa jiwe la msingi wa jengo la madarasa matano ya shule hiyo, mjumbe wa kamati hiyo, Chumu Ameir Juma alisema ingawa shule hiyo ilianza mwaka 2002 mpaka sasa bado inakabiliwa na tatizo ukosefu wa huduma ya umeme.

 

Chumu alisema kamati ya shule hiyo imeshangazwa na kitendo cha ZECO kushindwa kuweka transfoma shuleni hapo na badala yake kuipeleka katika eneo la kianga Kwaalhaarjiri, umbali wa kilometa moja kutoka mahali ilipo shule.

 

Mwaka 2004 uliahidi utaondoa tatizo la umeme katika shule hii na ukatoa fedha za kununulia transfoma, lakni mpaka sasa hatuioni,” aliema Chumu katika risala hiyo.

 

Alisema pamoja na tatizo la umeme, shule ya Kianga pia inakabiliwa na ukosefu wa huduma ya maji ambalo athari zake pia zinawagusa wakazi wapatao 5,000 wa Shehiya ya Kianga.

 

Baada ya kupewa nafasi ya kumkarisha Rais Shein kuweka jiwe la msingi wa jengo hilo , Abdallah Mwinyi Khamis alisema  kitendo cha ZECO kushindwa kutekeleza mpango wa weka transfoma kimemshangaza sana kwa sababu alishuhudia Rais Shein alipotoa shilingi milioni 3.6 baada ya uongozi wa shule hiyo kumwomba awaasaidie kuondokana na kero ya umeme.

 

Risala imenishtua sana , ningekuwa na presha nigeanguka kwa sababu nilishuhudia Dr Shein alipoombwa  transfoma mwaka 2004 akiwa Makamu wa Rais (Muungano)  na akatoa shilingi milioni 3.6 tukalipa ZECO,”  alisema.

 

Hata hivyo alisema alipofuatilia utekelezaji wa mpango wa kuweka transfoma hiyo shuleni  alishangaa kubaini tranbsfoma imewekwa walikojua wenyewe (ZECO) mbali na shule na kusababisha zihitajike nguzo 21 ili umeme uweze kufika katika eneo la shule ya Kianga.

 

 

 

Nilipowadadisi sababu ya kufanya hiyo, ZECO wakanipa jibu kwa Kiingereza kibovu  eti ,,, for technicola reasons we have placed it where there,s no people nearby,” alisema Abdallah akiwa na maana walimwambia transfoma haipaswi kuwekwa karibu na makazi ya watu.

 

Maelezo ya Mkuu huyo wa Mkoa, yalisababisha Rais Shein kumwita Meneja Mkuu wa ZECO, Mbarouk  mbele ya jukwaa kuu kutoa majibu ya malalamiko hayo.

 

Akifafanua Mbarouk alisema kampuni yake ililazimka kuweka transfoma mbali na shue kwa sababuhakuna nguzo zenye umeme mkubwa, lakini akaahizi kuanzia Jumatatu umeme utafikishwa shuleni hapo.

 

 

Rais Shein ambaye yuko katika ziara ya siku mbili katika mkoa wa Mjini Magharibi, baadaye alizindua mradi wa umeme uliojengwa kwa gharama ya shilingi billion 1.8  huko Mfenisini.

 

Dk. Ali Mohamed Shein,ameeleza kuwa Suala la upatikanaji maji safi na salama kwa wananchi wote wa visiwa vya Unguja na Pemba ni miongoni mmwa malengo makuu ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ya mwaka 1964.

  

Katika maelezo yake, Dk. Shein alisema kuwa Mipango na Sera mbali mbali zimekuwa zikipitishwa na kutekelezwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibatr, Awamu zote zilizopita ili kuhakikisha kwamba dhamira hii inafikiwa.

 

Alieleza kuwa katika Awamu hii ya Saba ya uongozi wake hatua zaidi zitachukuliwa na kufanya kila linalowezekana ili kuona  kuwa lengo hilo linatekelezwa.

 

Alisema kuwa uzinduzi wa  mradi huo umetokea katika wakati muwafaka kuhusu suala la maji ulimwenguni ambapo hapo kesho ni uzinduzi rasmi wa Wiki ya Maji Duniani.

 

Hata hivyo, naona nitumie fursa hii kusisitiza mambo matatu ya msingi likiwemo kuyatumia maji vizuri na kujiepusha na israfu, kuitunza miundombinu ya maji na kuwa waangalifu wa usalama wa maji pamoja na kuheshimu na kuvitunza vianzio vya maji yetu”,alisema Dk. Shein.

 

Aidha, Dk. Shein aliwapongeza wananchi kutokana na tokea kuanza kwa mradi huo wamekuwa mstari wa mbele na kutoa ushirikiano wa karibu na washirika wengine kupitia Kamati za maendeleo.

 

Pia, Dk. Shein alitoa shukurani kwa Jumuiya ya Ulaya (EU) kwa mchango wake mkubwa wa kifedha katika kufanikisha mradi huo ambapo mchango wa Jumuiya hiyo ni asilimia 71.5 fedha za kutekeleza mradi huo.

 

Pamoja na hayo alitoa shukurani kwa Jumuiya zisizo za Kiserikali hususan Jumuiya ya CHANGAMOTO, ANGOZA na ZAFFIDE  za hapa Zanzibar na Jumuiya ya FAI kutoka Uswisi na Jumuiya ya ACRA kutoka Itali kwa michango na jitihada zao madhubuti tokea mwanzo hadi kufikia hatua hiyo.

 

Dk. Shein pia, aliipongeza Uongozi wa Mamlaka ya Maji Zanzibar (ZAWA) na uongozi wa Mikoa yote pamoja na uongozi wa Wizara husika.

 

Mradi huo unalengo la kuzipatia maji safi na salama Sheihia 18 za Majimbo ya Mfenesini, Bumbwini na Kitope na maeneo ya jirani na zaidi ya wananchi 46.000 watafaidika na mradi huo. Huu ni mradi  wa aina yake na jumla ya Shilingi bilioni 1.8 .

 

Nao uongozi wa ACRA kutoka Itali ulitoa shukurani zao kwa mashirikiano mazuri yaliopata kutoka kwa Mamlaka ya Maji Zanzibar (ZAWA), na kueleza kuwa katika nchi 16 walizotoa msaada wao hapa Zanzibar ni nchi ya pekee waliopata mashirikiano mazuri na kuahidi kuendelea kutoa ushirikiano wao.

 

Mapema Dk. Shein alianza ziara yake asubuhi kwa kupata taarifa ya Mkoa wa Mjini Magharibi huko katika afisi za Mkoa huo ziliopo Vuga.

 

Baada ya hapo Dk. Shein alianza ziara yake katika Wilaya ya Magharibi Unguja kwa kuweka jiwe la msingi la jengo la madarasa matano ya Skuli ya Kianga na kueleza kuwa Serikali kupitia Wizara yake ya elimu italimaliza jengo hilo na kutoa shukurani kwa wananchi kwa mchango wao mkubwa wa ujenzi huo hadi kufikia hapo.

 

Aidha, Dk. Shein aliliagiza Shirika la Umeme  Zanzibar (ZECO) kuhakikisha kuwa ndani ya miezi mitatu tatizo la umeme katika kijiji cha Kianga, Jimbo la Dole liwe limepatiwa ufumbuzi kwani tayari alikwisha toa fedha taslim Tsh. Milioni 3.6 mnamo mwaka 2004, wakati akiwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania kwa ajili ya kununua transfoma.

 

Kwa maelezo ya wananchi na Mkuu wa Mkoa wa Majini Magharibi Bwana Abdalla Mawinyi transfoma hiyo iliwekwa sehemu ambayo haikuwa rahisi kwa skuli ya Kianga kupata umeme huo huku pia, wananchi nao wakikosa huduma hiyo kwa muda mrefu, ambapo Meneja wa Shirika la umeme alitakiwa kujibu hoja hiyo na kueleza kuwa umeme atahakikisha unafika siku ya Jumaatatu ijayo.

 

Pamoja na hayo, Dk. Shein aliwahakikishia wananchi hao kuwa juhudi za makusudi zitafanywa na serikali katika kuhakikisha wanapatiwa huduma za maji safi na salama huku akiutaka uongozi wa Jimbo uendelee kuwasaidia wananchi wa Kianga kumaliza ujenzi wa kituo chao cha afya huku akiahidi kusaidia utiaji umeme katika madarasa ya skuli hiyo.

 

Zaidi ya watu 46,000 kutoka Shehiya 18 za majimbo ya Bumbwini, Kitope na Mfenesini zitanufaika kwa kupata lita 250,000 za maji kwa saa kila siku. Miongoni mwa wafadhili wa mradi huo ni pamoja na Jumuiya ya Umoja wa Ulaya (EU).

 

 

 

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s