Wolfgang Dourado afariki dunia

Jaji wa Mahkama Kuu Zanzibar, Wolfgang Dourado na aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa mwanzo Zanzibar baada ya Mapinduzi ya 1964 amefariki dunia nyumbani kwake Vuga na mazisihi yake yatafanyika kesho katika kanisa la minara miwili Shangani Zanzibar

Jaji wa Mahkama Kuu ya Zanzibar na aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa kwanza wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar mara baada ya Mapinduzi ya mwaka 1964 Wolfgang Dourado  amefariki dunia nyumbani kwake Vuga  mjini Zanzibar. Kwa mujibu wa taarifa za ndugu wa marehemu Dourado wamesema kifo chake kimetokea nyumbani kwake akiwa na famili yake leo nyakati za mchana.

Kwa muda mrefu Dourado alikuwa akisumbuliwa na maradhi mbali mbali ambayo yanatokana na utu uzima wake.

 Bonyeza hapa CV Dorado 1  na Bonyeza hapa CV Dorado 2

Hadi anafariki dunia jaji Dourado alikuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Zanzibar akiongoza  Mahakama ya Kazi ya Zanzibar.

 

Dourado aliwahi pia kuwa Mwanasheria Mkuu wa kwanza wa Zanzibar mara baada ya mapinduzi ya mwaka 1964 na baadaye kuzaliwa kwa taifa jipya la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

 

Hata hivyo katika kipindi cha uhai wake Dourado alikuwa miongoni wakosoaji wa mkataba wa Muungano kati ya Zanzibar na Tanganyika ulioasisiwa na Marehemu Mzee Abeid Amani Karume na Mwalimu Nyerere.

Aiendelea na wadhifa wake hadi kifo cha hayati Karume mwaka 1972 ambapo mabadiliko mbali mbali yalifanyika na kuja kwa wanasheria mbali mbali wakuu katika kipindi cha rais mstaafu Alhaji Aboud Jumbe akiwemo Bashir Swanzi kutoka Ghana pamoja na Damian Lubuva ambaye kwa sasa ni Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).

 Mara baada ya kifo cha hayati Karume, Dourado alikuwa mwendesha mashtaka mkuu wa kesi ya kifo cha hayati Karume ambapo watu kadhaa walitiwa hatiani na kuhukumiwa kifo wakiwemo wanasiasa maarufu.

 

Dourado katika uhai wake aliwahi kushika nafasi mbali mbali za uongozi katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu pamoja na Idara ya Mahakama Kuu ya Zanzibar akiwemo mjumbe wa kamati mbali mbali na tume za kurekebisha muundo wa Mahakama ya Zanzibar.

 

Kufuatia kuundwa kwa Mahakama ya kazi ambayo lengo lake kubwa kusikiliza malalamiko yanayotokana na ajira katika utumishi wa Serikali na sekta binafsi Dourado aliteuliwa na rais mstaafu Amani Abeid Karume kuongoza mahakama ya kazi.

 

Dourado alizaliwa Septembar 20 mwaka 1929 na kusoma katika shule mbali mbali za Unguja ikiwemo St. Joseph ya Zanzibar katika mwaka 1939-1946.

Na baadaye kwenda Uingereza katika shule ya Royal London School of Economic katika mwaka 1962-1963.

Baada ha hapo alipata kazi katika serikali ya Kikoloni tangu mwaka 1947 hadi alipostaafu mwaka 1985 ambapo pia alipitia katika ngazi mbali mbali za uongozi akiwemo katibu mkuu katika wizara tofauti.

 

Nyadhifa nyengine alizoshika katika serikali ni pamoja na Mwanasheria Mkuu wa kwanza wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar mnamo Febuari mwaka 1964.

 

Aidha katika mwaka 1977 aliteuliwa kuongoza Shirika la Bima la Zanzibar, na kuwa meneja mkuu wa kwanza, na baadaye kuongoza taasisi ya kuangalia muundo wa sheria mbali mbali za nchi, ikiwemo za mahakama kuu.

Nyadhifa nyengine alizoshika wakati wa uhai wake ni kuwa mjumbe katika kamati mbali mbali katika sekta ya sheria ikiwemo kuwa mjumbe wa tume ya rais iliyokuwa ikitazama suala la mfumo wa chama kimoja au mfumo wa vyama vingi mwaka 1991.

 

Mwili wa Dourado anatazamiwa kuzikwa kesho katika makaburi ya Mwanakwerekwe Mjini Zanzibar kabla ya kufanyiwa misa katika Kanisa la Minara Miwili Shangani. Marehemu amewacha mke mmoja na hakujaaliwa kupata mtoto wakati wa uhai wake.

 


Advertisements

4 responses to “Wolfgang Dourado afariki dunia

  1. This style is incredible! You undoubtedly know how to maintain a reader amused. Between your wit and your videos, I was almost moved to start my own weblog (properly, almostHaHa!) Great job. I actually loved what you had to say, and a lot more than that, how you presented it. Too cool! 314012

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s