Uvumi wa vyandarua wasambazwa

Watoto hawa wawili wakitoka kuchukua vyandarua hapo jana katika vituo vyao ambapo wananchi kadhaa jana wamejitokeza lakini leo uchukuaji huo umekuwa ukisuasua baada ya kuenea kwa uvumi kuwa vyandarua hivyo vina madhara na kusababisha vifo

Mradi wa Malaria Zanzibar unaofadhiliwa na Mashirika ya Global Fund pamoja na Marekani umeingia matatani baada ya kuwepo uvumi kwamba vyandua wanavyogawa kwa wananchi vinasababisha watu kupoteza maisha na wengine kuzimia baada ya kuvitumia. Uvumi huo umekuja siku moja baada ya hatua ya serikali kugawa vyandarua hivyo kwa wananchi huku wanaovumisha wakiwemo baadhi ya viongozi wa dini wakisema kwamba vyandarua hivyo vinasababisha ukosefu wa uzazi, kuvuruga akili na kupoteza maisha.

Uvumi huo umeanza kusambaa jana jioni katika baadhi maeneo yakiwemo Kisiwani Pemba na baadhi ya miskiti ya hapa Unguja leo nyakati za asubuhi baada ya sala ya alfajiri baadhi ya Maimamu wamesimama kuwatahadharisha na kuwataka wananchi wasende kuchukua vyandarua hivyo hivyo kusababisha khofu kwa wananchi walio wengi. Wakati hayo yakitendeka huko misikitini baadhi ya wananchi wamekuwa wakisambaza uvumi huo kwa njia za simu kuwahamasisha watu wasende kwa madai kwamba wapo watu wamezirai na wengine wamefariki dunia baada ya kuvitumia vyandarua hivyo.

Vyandarua hivyo ni sehemu ya juhudi za serikali ya Zanzibar za kutokomeza Malaria hapa nchini ambapo mradi huo ulianza mwaka 2005 kwa msaada wa Marekani na Shirika la Afya Duniani (WHO). na kabla ya mradio huo kulikuwa na mradi ya Kataa Malaria ambapo umesaidia sana kupunguza vifo vinavyotokana na Malaria.
Meneja wa Mradi wa Malaria Zanzibar, (Zanzibar Malaria Control Programme) Abdallah Suleiman aliwaambia waandishi wa habari kwa njia ya simu kwamba wamepokea uvumi huo lakini hakuna ukweli wowote hadi sasa wa vifo baada ya kufanya uchunguzi wa kina.


“Tumepata taarifa hizo ambazo ni za upotoshaji kwa sababu kabla ya ugawaji wa vyandarua tulikuchua tahadhari zote kuhakikisha kwamba vyandarua hivyo havina madhara kwa binaadamu…lakini baada ya kupata taarifa ya leo asubuhi tumefuatilia katika sehemu mbali mbali kufahamu kama kuna ukweli juu ya hivyo vifo lakini tumeshindwa kuthibitisha uvumi huo maana hakuna mtu aliyethibiika kwa kufa kwa matumizi ya vyandarua” alisema Meneja huyo.

Inawezekana baadhi ya watu katika matumizi wakawa wamepata matatizo madogo madogo mfano kama muawasho hivi kidogo lakini matatizo makubwa kama hivyo kufa au kuzimia hatujapata taarifa hiyo kwa kuwa kabla ya matumizi tulizingatia sana suala la usalama wa vyandarua hivyo. Lakini tunatoa wito kwa wale waliokuwa hawajenda kuchukua baada ya kupata taarifa hivi za uvumi basi tunawaomba waende wakachukue vyandarua vyao wasiogope na mtu yeyote ambaye atapata matatizo asiache kutuarifu na kwenda kuripoti katika taasisi zinazohusika.


Tokea jana na leo wananchi mbali mbali Unguja na Pemba wamejitokeza kwa wingi kuchukua vyandarua katika maeneo mbali mbali ambapo wanatakiwa kuvitumia kwa ajili ya kujikinga na mbu wanaoeneza Malaria. Harakati za matayarisho kwa ajili ya ugawaji wa vyandarua zilianza mwezi uliopita na nyumba zote zaidi ya 250,000 kuhakikiwa na kupata makisio ya vyandarua zaidi ya 600,000 vitakvyogaiwa kwa wananchi.


Zaidi ya dola za kimarekani millioni 3.5 zinatumika katika mradi huo ambao unakwenda sambamba na awamu ya saba ya upigaji wa dawa majumbani ili kuwauwa mbu wanaoeneza malaria. Mradi wa upigaji dawa majumbani, matumizi ya vyandarua na utumiaji wa dawa sahihi za kuuwa malaria zimesaidia kwa kiasi kikubwa Zanzibar kupunguza mambukizi ya Malaria kutoka asilimia 40 mwaka 2004 hadi chini ya asilimia 1 mwaka jana.


Zanzibar sasa imekuwa ukipigiwa mfano katika nchi mbali mbali hasa za Afrika baada ya kufanikiwa kupunguza Malaria kwa kiasi kikubwa ambapo pia imepunguza kwa kiasi kikubwa vifo vya akina mama na watoto walio chini ya umri wa miaka mitano vinavyotokana na Malaria.

Advertisements

5 responses to “Uvumi wa vyandarua wasambazwa

  1. Huu ni upotoshaji usio na msingi na anaefanya haya hawatakii mema Wazanzibari. Kuna saababu gani ya hao watu kutaka kutuua ? Tuacheni upumbavu kila mmoja anakubali jinsi Malaria ilivyopungua Zanzibar. Mnataka turudi kule tulikotoka kila siku kila nyumba kuna mgonjwa wa Malaria?

  2. Uvumi umeanza Pemba, ngome kuu ya CUF. Huko nyuma kwenye uwanja huuhuu walivumisha kuwa wanachama wa CUF wanabaguliwa kuandikisha vyandarua.

    Muwaone hawa, ndivyo walivyo.

  3. Lisemwalo lipo kama halipo basi laja……..Hakuna msaada usio na malengo isiwe tunatizama kupata tu je anaetoa anapata nini? au ndio sumu ya kutuuwa baada ya miaka kadhaa waje wachukue kisiwa kiurahisi, tuwe makini na misaada kama hii anaeathirika ni mwananchi wa hali ya chini na sio viongozi wetu sababu huenda hata wao wakatuuza wanachi wao kwa maslahi yao binafsi.

  4. Ulimwengu huu ni kumwomba Mungu atukinge nasi weyewe tujitahidi tu. Inaweza kuwa wanasayansi huko nje wana tafiti zao wanaendesha kwa madawa mbalimbali na ‘concentration’ mbalimbali. Kwa vile hawawezi kutumia watu wao kama ‘specimens’ hivyo sisi tunaweza kuchukua nafasi hiyo pale walipomaliza kujaribu dawa hizo kwa mapanya. Kinachokuja huku ndio kimefika, wanasayansi wetu ni butu na bubu. Kule Libya enzi za Gaddafi walikamatwa wakiwaambukiza ukimwi kwa makususdi wananchi, tena maasum-watoto wadogo. Pengine miongoni mwa malengo ni kuuonesha ulimwengu kuwa Uislam si kinga ya ukimwi. Hilo ni tawi moja la fikra.
    Katika tawi jengine tusisahau kwamba hii ni nchi ya majungu na uchakachuzi. wafanya biashara wa vyandarua wanaweza kueneza kampeni chafu kwa kuhofu kwamba biashara yao itakufa pale watu watapopata vyandarua vya bure. Wale wanaojishughulisha na vihospitali vya binafsi na maduka ya madawa wanaweza kuhofu iwapo watu watakuwa hawaugui watakosa pesa. Amini usiamini mchimba kaburi hufurahia akipata tenda nyingi ya kazi hiyo.
    Sasa, mimi na wewe tuwe macho huku tukijua kwamba hatari hizi mbili zimetukabili. Ukipata chandarua kioshe kwanza na kukianika hata mara mbili kisha kitumie. Wa billahi taufiq

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s