Mwili wa Marehemu Mtondoo waagwa

Baadhi ya wajumbe wa baraza la wawakilishi wakiongozwa na Katibu wa Mufti wa Zanzibar, Sheikh Fadhil Suleiman Soraga katika dua maalumu ya kumuombea aliyekuwa Mwakilishi wa Jimbo la Bububu (CCM) Salum Amour Mtondoo aliyefariki dunia leo katika Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja Zanzibar. Mwili wa Marehemu uliwasilishwa katika ukumbi wa baraza la wawakilishi kwa ajili ya kuagwa na kuombewa dua. Mwenyeenzi Mungu amlaze mahali pema peponi inshaallah

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein, leo ameongoza mazishi ya marehemu Mheshimiwa Salum Amour Mtondoo, aliyekuwa mwakilishi wa Jimbo la Bububu, Mkoa wa Mjini Magharibi Zanzibar.Viongozi mbali mbali wa Vyama, Dini na Serikali wakiwa pamoja na wananchi na wanafamilia walihudhuria katika mazishi hayo, ambapo Makamu wa Kwanza wa Rais Alhaj Maalim Seif Sharif Hamad nae alihudhuria.

Alhaj Balozi Seif Ali Idd pamoja na Rais mstaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi nae alihudhuria katika mazishi hayo yaliofanyika saa nne asubuhi huko kijijini kwao marehemu Bumbwini Misufini, Wilaya ya Kaskazini B, Mkoa wa Kaskazini Unguja ambapo maiti aliondokea nyumbani kwake Bububu baada ya kusaliwa katika msikiti Utapoa Bububu.
Mheshimiwa Salum Amour Mtondoo alifariki dunia jana tarehe 15/3/2012 kwenye hospitali ya MnaziMmoja, ambako alikuwa amelazwa akipatiwa matibabu.
Mheshimiwa Mtondoo alizaliwa tarehe 14/12/1962 Bububu, Wilaya ya Magharibi, Zanzibar na kupata elimu yake ya msingi na Sekondari katika Skuli ya Bububu kuanzia mwaka 1969 hadi 1979.
Akisoma risala fupi baada ya mazishi hayo, Kaimu Katibu wa Baraza la Wawakilishi Yahya Khamis alieleza kuwa katika shughuli za ajira rasmi, marehemu aliwahi  kufanya kazi ya Usimamizi wa Kiwanda cha kutengenezea nguo cha COTEX kuanzia mwaka 1983 hadi mwaka 1985.
Alieleza kuwa nje ya ajira rasmi, marehemu alifanya kazi za Ujenzi katika Ushirika wa Bait-El-rs Building Brigade (BBB) hadi mwaka 1986 hadi mwaka 1992. Vile vile, aliwahai kufanya kazi za biashara kuanzia mwaka 1992 hadi mwaka 1020.
Katika shughuli za kisiasa, marehemu amewahi kushiriki nyazifa mbali mbali katika Chama Cha Mapinduzi zikiwemo Ujumbe wa Kamati ya Siasa ya Tawi na Ujumbe katika Jumuiya ya Wazazi Wilaya na Mkoa.
Mheshimiwa Salum alichaguliwa kuwa Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi wa Jimbo la Bububu katika Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar uliofanyika Octoba, 2010 ambapo  katika Baraza la Wawakilishi alikuwa mjumeb wa Kamati ya Mawasiliano na Ujenzi na aliitumikia Kamati hiyo hadi muda wote wa Uwakilishi wake.
Katika kipindi cha kifupi cha kazi yake ya Uwakilishi, Marehemu alifanya kazi nzuri ya kuwatetea wananchi wa Jimbo lake pamoja na wananchi wote wa Zanzibar, na aliifanya kazi hiyo kwa moyo wake wote, uadilifu na mashiruikiano makubwa kwa wananchi na Wajumbe wenziwe wa Baraza la Wawakilishi
Kaimu Katibu Mkuu huyo alieleza kuwa ni dhahiri kuwa Baraza la Wawakilishi, Chama Cha Mapinduzi, Wananchi wa Jimbo la Bubu na wananchi wote wa Zanzibar kwa jumla wameondokewa na mtu muhimu aliyesaidia katika kuleta maendeleo ya Taifa.
Wengine waliotoa salamu zao kwa niaba ni Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi, Zanzibar Vuai Ali Vuai ambaye alieleza kuwa kifo cha Marehemu Mtondoo kimeacha pengo kubwa katika CCM, ambapo alikiri kuwa Chama hicho kimeondokewa na mtu muhimu ambaye bado walikuwa wakimuhitaji na kuahidi kuwa Chama kipo pamoja nae.
Nae Spika wa Baraza la Wawakilishi Pandu Ameir Kificho akitoa salamu za Baraza la Wawakilishi alieleza kuwa marehemu Mtondoo alikuwa kiungo muhimu cha Baraza hilo kwani alikuwa akifanya kazi zake kwa umakini na mashirikiano ya makubwa.
Waziri wa Nchi Afisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mhe. Mohammed Aboud, akitoa salamu za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar alisema kuwa  Marehemu Mtondoo ameacha pengo kubwa ambalo si kwa wananchi wa Bububu pekee bali ni pengo kwa Zanzibar nzima na kueleza kuwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar iko pamoja na wafiwa.
Nao wanafamilia walitoa shukurani zao kwa viongozi wote pamoja na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na wananchi wa Jimbo la Bububu kwa mashirikiano makubwa waliyoyapata katika kipindi chote cha msiba huo wa mwanafamilia yao. Marehemu ameacha vizuka watatu na watoto 10.
Advertisements

2 responses to “Mwili wa Marehemu Mtondoo waagwa

  1. Hapa sasa tunaondoka kwenye utamaduni wetu wa kiislamu, hizi issue za kuaga ni katika mila za kikafiri kwenye uislamu hakuna sehemu iliyotajwa kitu kuaga ila tunachotakiwa ni kuhudhurika kwenye mazika kama ni haki ya mwislamu kwa muislamu mwenzake tumezowea kuona haya kwa Watawala wetu Tanganyika sasa mimi nina wasiwasi kuwa hii itakuwa ni some sort of justification ambazo tunawawekea vizazi vyetu kuona ni mila zetu kumbe no ila ni kwa wachache kukumbatia ukoloni wa Tanganyika na kuacha mila zetu adhimu za kistaarabu naomba masheikh wapinge hili kwa kuepusha hatari huko twendako.

  2. he, Kupinga tuuuu kila kimachofanywa na serikali au CCM.
    Tubadilike. Hivi s utamaduni wetu waislamu wa Zanzibar kusoma Maulid ya mfunguo sita. Mbona sasa wamejitokeza watu wanayapnga na hawasemwi.

    Kubali mabadiliko. Usibaki kwenye zama za mawe,

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s