Mwakilishi wa Bububu afariki dunia

Mwakilishi wa Jimbo la Bububu (CCM) Marehemu Salum Amour Mtondoo

Mwakilishi wa Jimbo la Bububu (CCM) Salum Amour Mtondoo amefariki dunia jana katika Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja alipokuwa amelazwa. Spika wa Baraza la Wawakilishi, Pandu Ameir Kificho aliwathibitishia waandishi wa habari juu ya kifo hicho na kusema kwamba kifo chake wamekipokea kwa huzuni kwani kubwa.

Mtondoo ambaye alikuwa Mwakilishi kufuatia uchaguzi uliofanyika Octoba, 2010, alizaliwa tarehe 14/ 12/ 1962 huko Bububu , Wilaya ya Magharibi , Zanzibar ambapo alipata elimu yake ya msingi na Sekondari katika Skuli ya Bububu kuanzia mwaka 1969 hadi mwaka 1979.


Marehemu Mtondoo katika uhai wake aliwahi kufanyakazi ya Usimamizi wa Kiwanda cha COTEX mnano mwaka 1983 hadi mwaka 1985 na Baadae kufanyakazi za Ujenzi katika ushirika wa BBB 1986 hadi mwaka 1992. Mbali ya kazi hizo , Marehemu aliwahi kufanyakazi za biashara kuazia mwaka 1992 hadi mwaka 2010.


Aidha katika katika shughuli za kisiasa, Marehemu amewahi kushika nyadhifa mbali mbali katika Chama Cha Mapinduzi (CCM) ikiwemo mjumbe wa Kamati ya siasa ya Tawi na nafasi za ujumbe katika jumuiya ya wazazi Wilaya hadi Mkoa.


Mheshimiwa Salum Mtondoo alikuwa Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi wa Jimbo la Bububu , kupitia Chama cha Mapinduzi katika Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar uliofanyika Octoba, 2010.


Marehemu ameacha wake wawili (Vizuka) na watoto 10.

Tunamuomba Mwenyezimungu aijaalie familia ya Marehemu pamoja na wananchi wa Jimbo la Bububu, subira na utulivu katika kipindi hiki kigumu cha msiba. Mwenyezimungu aiweke roho ya Marehemu mahali pema peponi. Amin.


Huyo ni Mwakilishi wa pili kufariki katika kipindi tokea kumalizika kwa uchaguzi mkuu wa 2010 ambapo Agosti Mwakilishi wa Jimbo la Uzini (CCM) Mussa Khamis Silima alifariki dunia. 

Advertisements

5 responses to “Mwakilishi wa Bububu afariki dunia

  1. mungu amuhuhukumu kama alivyo itumikia zanzibar kama alishirikiaana na watanganyika kuiyumiza zanzibar yeye na mungu wake ikiwa alishirikiana na wazanzibar na uzanzibar na uisilam na waisilam kuitetea maslahi ya zanzibar basi mungu mpe kila mazuri na umstiri na umjaalie firdaus nuzulaa

  2. Inna lillah wa inna illayhi raj uun. Hakika kila nafsi itaonja mauti. Mwenyezi Mungu awape subra wafiwa na atuafikishe kutenda mema.

  3. kaka Abdulmajid< sio wakati wake wakuchanganya siasa hali yakua mwenzetu ametangulia mbele yahaki. hata kama labda ana mabaya si ustarabu kumuombea au kumsimanga maiti. MUNGU NDO MJUZI WA YALIYO JIFCHA NA YALIO KATIKA NIA ZA KILA MTU. YEYE NDO HAKIMU WA HAKI NA WALA HAFUNDISHWI NAMNA YA KUHUKUM. YEYE NDIO MREHEMESHAJI NA HUMREHEMU AMTAKAYE. Abdulmajid najua unauchungu wa zanzibar kama tulivyo wazanzibari sote. kutokana na mila na utamaduni wetu ak izanzibar na pengine hata kiislamu haipendezi kumuombea maiti dua mbaya.ni vizuri tukamuombea rehma kwa Mwenyezi Mungu na kumpunguzia ahdhabu. Maisha ya dunia ni mapito yaliojaa mitihani tele. Hakuna aliye na uhakika kua atakufa akiwa msafi. Hata wewe bwana Majid unaweza ukahilibika na maisha haya yadunia utakapopata nafsi na ukasahau kuwa ulikua wa mwanzo kutetea maslahi yanchi yako.Muhimu tumuombee nduguyetu mapumzikomema nasi MUNGU atume hatma njema.

  4. Hajui alitendalo huyo Abdulmajid,Zanzibar itaimarika kwa kufanya kazi kwa bidii kwa kila Mwananchi kutoa nguvu zake na mawazo yake kwa maslahi ya Taifa na sio kuendekeza Siasa chafu,Udini na vyenginevyo .Mungu amsafishie makaazi yake na amuwekee Nuru ya milele katika Kaburi lake Marehemu Salum Amour Mtondoo na Sie Tulionyuma yake Atuzidishie moyo wa Imani na Ibada zaidi Amin.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s