Hutuba ya ofisi ya makamo wa kwanza juu ya utafiti

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Dk Omar Dadi Shajak akitoa hutuba katika uzinduzi wa ripoti ya utafiti wa vyombo vya utangazaji Zanzibar katika Hoteli ya Ocean View

Naomba nimalizie kwa nasaha zifuatazo kabla ya kufanya hiyo kazi niliyotakiwa kuifanya, ripoti hii imetuonyesha hali halisi tulivyo, hivyo niwaombe watendaji wenzangu wa shirika la utangazaji la Zanzibar, kwanza, kutengeneza ramani ya utekelezaji (road map) kulingana na matokeo ya utafiti huo ili kukabiliana na udhaifu ulioonyeshwa na kupambana na changamoto zilizotolewa. Pili, katika kuyaangalia mapendekezo yaliyotolewa na kuyafanyia kazi lazima muyaangalie kwa kutafsiri mazingira ya Zanzibar na utamaduni wa Wazanzibari. Si kila zuri linalofanywa na vyombo vya habari vya nje kuwa litakuwa zuri kwa mazingira ya Zanzibar kwa sababu tu ya visingizio vya ushindani. Mimi kama mimi msimamo wangu ni kuandaa vipindi vinavyopendwa na umma na vinavyoheshimu maadili ya kizanzibari, vinavyotoa taarifa za ukweli zilizofanyiwa uchunguzi na bila kuegemea upande wo wote wa siasa na unaoheshimu dini zote, unaoheshimu makundi yote ya watu na kuamini kwamba binaadamu sote tuko sawa na ni maumbile tu yaliyotufanya tuwe ama mwanamke au mwanamme, ama una ulemavu kwa sasa au huna. Tatu, Prof. MacKinon, profesa na mtaalamu wa masuala ya mawasiliano kutoka Chuo Kikuu cha Oxford, amesema ‘New time calls for new Thinking’ (Zama Mpya huhitaji mawazo mapya) na Rais wetu Dr. Ali Mohd Shein anatwambia ‘TUBADILIKE’. Kwa hiyo basi, Zama Mpya zinahitaji mawazo mapya.Tubadilike. Endelea kusoma hutuba hii

HOTUBA YA MGENI RASMI KATIBU MKUU OFISI YA MAKAMU WA KWANZA WA RAIS DR. OMAR D. SHAJAK KATIKA UZINDUZI WA RIPOTI YA UTAFITI WA VYOMBO VYA UTANGAZAJI VYA UMMA ZANZIBAR 15 MACHI, 2012 ZANZIBAR OCEAN VIEW

Ndugu Viongozi wa Baraza la Habari Tanzania

Ndugu Wanahabari na wadau Mbali mbali wa Tasnia ya Habari

Ndugu wageni Waalikwa

Mabibi na Mabwana

As sallam alaykum,

Ndugu Wanahabari,

Awali ya yote, napenda kuchukua nafasi hii kumshukuru Mwenyezi Mungu, mwingi wa rehma kwa kutuwezesha kukutana hapa, tukiwa na furaha na afya njema.

Ninapenda kuchukua nafasi hii, kutoa shukrani zangu za dhati kwa uongozi wa Baraza la Habari Tanzania kwa kunipa heshima hii ya kipekee ya kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa Ripoti hii ya Utafiti juu ya Utendaji kazi wa Vyombo vya Utangazaji vya umma katika zama zenye ushindani mkubwa.

Aidha, ninaomba nichukue nafasi hii kulishukuru Baraza la Habari la Tanzania kwa kuweza kudhamini kufanyika kwa utafiti huu. Wazo lao lilikuwa ni hatua moja ya maendeleo kwa tasnia ya habari kwani, kufanya utafiti ni njia kuu ya kuweza kujitambua uwezo wako, udhaifu wako na changamoto zinazokukabili ili utumie matokeo ya utafiti huo kuweza kujisahihisha kwa udhaifu uliougundua na kujipanga kukabiliana na changamoto na kufanya yaliyo bora zaidi. Kwa umuhimu wa utafiti, ndio maana Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ikaamua kuanzisha Idara za Mipango, Sera na Utafiti kwa Wizara zake zote na kuzitenganisha na Idara za Uendeshaji na Utumishi ili kutoa nafasi kwa UTAFITI kupata mtazamo unaostahiki.

Ndugu wanahabari,
Naomba pia nichukue nafasi hii kumshukuru sana Bwana Samwilu Mwafisi kwa kuweza kukamilisha kazi aliyopewa na Baraza la Habari na leo hii tupo hapa kuweza kuzindua Ripoti hii. Juhudi zake binafsi, taaluma yake, uwezo wake na uvumilivu mkubwa umemuwezesha kukamilisha kazi hii. Tunamshukuru na kumpongeza yeye na wasaidizi wake wote waliomsaidia katika kufanya utafiti huu.

Ndugu Wanahabari,
Nilipoambiwa kuwa nimeteuliwa rasmi kuzindua ripoti hii juzi, niliipokea heshima hii kwa mikono miwili lakini nikahisi nimepewa kazi kubwa ya kuzindua ripoti ambayo sijaisoma na kwa hiyo nikalazimika kuchukua juhudi maalum wa kuipitia ijapo kwa haraka haraka. Nilichojifunza yaliomo katika Ripoti hii hayakuwa mageni kwangu kwa bahati niliyoipata ya kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ambayo imesimamia vyombo hivi viwili STZ na TVZ ambavyo leo vimeunda shirika moja kwa vipindi viwili vyenye jumla ya miaka kumi(1995-2000 na 2005-2010).
Nimekuwa mshiriki katika kipindi hicho ndani ya safari ndefu ya ZBC, ni hakika safari yake imekuwa shwari pale upepo ulipotulizana na imekuwa ikikumbana na dharuba (turbulences) pale upepo ulipobadilika kama zilivyo safari zote. Mathlan, mwaka 1995 katikati TVZ iliishiwa nguvu kabisa na kuwa chumba cha watu mahututi na ndipo mwaka 1996 ikapata uhai tena pale ilipopata msaada mkubwa wa Serikali ya Japan. Hivyo, sikushangaa nilipoona watoa majibu (Respondants) hasa wale waliopo ndani ya chombo chenyewe wakionyesha udhaifu wa vitendea kazi uliopo.

Ndugu Wanahabari,
Kama nilivyotangulia awali kusema kuwa, utafiti unafanywa ili utusaidie kujiona tuko vipi au tuko wapi, udhaifu wetu, uwezo wetu na changamoto zinazotukabili. Nilipoipitia Ripoti hii yote hayo nimeona yapo. Vyomo hivi vilipoanzishwa pamoja na kwamba hilo wazo la ‘Public Broadcasting’ Vyombo vya Utangazaji vya Umma ni mawazo mapya (concept mpya) ambazo zimekuja miaka ya tisini(90’s) na vyombo vyetu hivi vilizaliwa kabla ya hapo lakini wakati vyombo hivi vinaundwa lengo lilikuwa ni kuitumikia jamii na sio vyenginevyo. Naomba nimnukuu Rais wa Awamu ya pili wa Zanzibar, Alhaj Aboud Jumbe Mwinyi katika hotuba yake katika ufunguzi wa kituo cha TVZ Januari,1974 kama alivyonukuliwa na N’gwanakilala, 1981

“I have stated time and time again that TV in
Zanzibar is an investment on development, a
tool by means of which our people can enhance
their own development. We in Zanzibar are
absolutely committed to education through
colour television. We must therefore create an
atmosphere conducive to development of the
education through the means we envisage”

Ndugu Wanahabari,
Wakati Serikali ikiwa imeshachukua juhudi kubwa ya ununuzi wa vifaa ili kuigeuza TBC TV kutoka katika mfumo wa analojia kuingia dijitali na TBC Radio kuweza kununuliwa mitando miwili mipya ya FM sambamba na mtambo mpya wa Masafa ya Kati na ule ukarabati mkubwa wa mtambo wa masafa mafupi Short Wave, mwanzoni mwa mwaka jana Serikali ya awamu ya saba ilitangaza kuunda Shirika la Utangazaji la Zanzibar kwa nia ile ile ya kutoa nguvu zaidi kwa vyombo hivi kuweza kufanya shughuli zake kwa misingi ile ile ya kuutumikia umma wa Zanzibar na si vyenginevyo.

Ninachokiona mimi na ambacho ninakiamini ni jinsi uongozi wa shirika utakavyojipanga na kuweza kuonyesha yale ambayo wananchi wanategemea kuyaona. Tuondoke na mawazo mgando ya kufikiria tu kuwa vyombo vya habari vimeanzishwa kuisifia serikali iliyopo madarakani. Serikali yenyewe wakati wote imekuwa ikijidhatiti kuutumikia umma iweje chombo cha umma kisiutumikia umma wenyewe. Chombo cha umma kinapaswa kuandaa programu zinazoisaidia jamii. Programu za mapambano dhidi ya janga la dawa za kulevya, programu za mapambano dhidi ya UKIMWI, programu za kujidhatiti na Mabadiliko ya athari za tabia nchi na uharibifu wa Mazingira, Programu za kuwafichua wanaowaficha watu wenye ulemavu na kuwakosesha haki zao za msingi ikiwemo elimu na kadhalika na kadhalika.

Ndugu wanahabari,
Naomba nimalizie kwa nasaha zifuatazo kabla ya kufanya hiyo kazi niliyotakiwa kuifanya, ripoti hii imetuonyesha hali halisi tulivyo, hivyo niwaombe watendaji wenzangu wa shirika la utangazaji la Zanzibar, kwanza, kutengeneza ramani ya utekelezaji (road map) kulingana na matokeo ya utafiti huo ili kukabiliana na udhaifu ulioonyeshwa na kupambana na changamoto zilizotolewa.
Pili, katika kuyaangalia mapendekezo yaliyotolewa na kuyafanyia kazi lazima muyaangalie kwa kutafsiri mazingira ya Zanzibar na utamaduni wa Wazanzibari. Si kila zuri linalofanywa na vyombo vya habari vya nje kuwa litakuwa zuri kwa mazingira ya Zanzibar kwa sababu tu ya visingizio vya ushindani. Mimi kama mimi msimamo wangu ni kuandaa vipindi vinavyopendwa na umma na vinavyoheshimu maadili ya kizanzibari, vinavyotoa taarifa za ukweli zilizofanyiwa uchunguzi na bila kuegemea upande wo wote wa siasa na unaoheshimu dini zote, unaoheshimu makundi yote ya watu na kuamini kwamba binaadamu sote tuko sawa na ni maumbile tu yaliyotufanya tuwe ama mwanamke au mwanamme, ama una ulemavu kwa sasa au huna.
Tatu, Prof. MacKinon, profesa na mtaalamu wa masuala ya mawasiliano kutoka Chuo Kikuu cha Oxford, amesema
‘New time calls for new Thinking’ (Zama Mpya huhitaji mawazo mapya) na Rais wetu Dr. Ali Mohd Shein anatwambia ‘TUBADILIKE’. Kwa hiyo basi, Zama Mpya zinahitaji mawazo mapya, Tubadilike.
Ahsante sana kwa kunisikiliza na sasa naomba nitamke rasmi kwamba Ripoti ya Utafiti wa Utekelezaji wa vyombo vya Utangazaji vya Umma katika zama zenye ushindani mkali, imezinduliwa rasmi.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s