Ripoti ya Utafiti wa vyombo vya habari

Utafiti umeonyesha kwamba asilimia 61 ya wasikilizaji na watazamaji wa ZBC wana mtazamo chanya na asilimia 39 wana mtazamo hasi kuhusu ZBC. Wale wenye mtazamo chanya wamekiri kwamba utangazaji wa umma ni muhimu lakini wametaka hatua za haraka zichukuliwe ili nao wasije wakawa na mtazamo hasi. Wale wenye mtazamo hasi wamesema ZBC imeendelea kuwa sauti ya seriakli wakati vituo binafsi vya utangazaji vimekuwa sauti ya wananchi wanyonge. Wafanyakazi 33 (49%) wana mtazamo hasi kuhusu ZBC na 18 (23%) wana mtazamo chanya. Wafanyakazi 22 (28%) hawakujibu swali. Wafanyakazi wenye mtazamo hasi kuhusu ZBC wanaamini ufinyu wa bajeti na msukumo wa kisiasa ndiyo matatizo sugu yanayoathiri utendaji kazi wa ZBC. Wamedai kwamba ZBC ina wafanyakazi wenye uzoefu, weledi na moyo wa dhati kulitumikia shirika kuhakikisha linafanya kazi vizuri, lakini wanaamini seriakli imeshindwa kuwawezesha kuifanya kazi hiyo na hivyo kuwavunja moyo. Wafanyakazi hao, kwa ujumla wao, wanakiri kwamba jinsi shirika linavyofanya kazi hivi sasa ni utangazaji wa dola na ndiyo maanda wana mtazamo hasi kuhusu ZBC kufanyia kazi ya utangazaji wa umma.

UTANGAZAJI WA UMMA ZANZIBAR KATIKA ZAMA ZA UTANGAZAJI WA USHINDANI

Na Samwilu Mwaffisi

1.0: UTANGULIZI

Katika nchi nyingi za Afrika kusini mwa jangwa la Sahara mfumo wa utangazaji wa umma umekuwa ukichukuliwa kimakosa kwamba ni sawa na mfumo wa utangazaji wa dola. Ukweli ni kwamba hii ni mifumo miwili ya utangazaji iliyo tofauti kabisa. Hivyo ni muhimu kuanzia mwanzo kabisa ya mazungumzo yetu tukakumbushana tofauti ya mifumo hii ili tuweze kujenga msingi imara ya majadiliano yetu.

Kwa ufupi – utangazaji wa dola uko moja kwa moja chini ya dola na ni sehemu ya utawala wa dola. Kwa sababu hiyo utangazaji wa dola unasimamiwa moja kwa moja na wizara ya serikali kuu. Dola inatumia mfumo huu wa utangazaji kutekeleza maslahi yake ya kisiasa na mengineyo..

Jukumu kubwa la utangazaji wa umma ni kutoa huduma kwa umma na hivyo inawajibika kutekeleza maslahi ya umma katika vipindi vyaka. Shirika la utangazaji wa umma huanzishwa na serikali, lakini huachiwa Bodi huru ya wakurugenzi ambayo inawajibika kuhakikisha shirika linatoa huduma kwa umma kupitia vipindi vyake.

Tuliouita utangazaji wa umma hapa Africa wakati wa mfumo wa chama kimoja na hata sasa chini ya mfumo wa vyama vingi vya siasa, unatekelza maslahi ya serikali iliyopo madarakani.Hii ni sababu ya msingi inayofanya watu wengi kuona utagazaji wa umma ni sawa na utangazaji wa dola. Ndiyo maana nimeanza kwa kukumbushana tofauti ya mifumi hii miwili ya utangazaji.

Mwanzoni mwa miaka ya 1990 kulitokea mapinduzi ya kisiasa katika nchi nyingi za Afrika ambayo yalizifanya nchi hizo kuachana na mfumo wa siasa ya chama kimoja na kuzingatia mfumo wa vyama vingi vya siasa. Miongoni mwa matunda ya kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi vya siasa ni serikali zetu kuruhusu vyombo binafsi vya habari kuanzishwa. Kwa vyombo vya habari vinavyomilikiwa ba serikali wito ulitolewa kubadilisha mfumo wa utangazaji wa dola na kuzingatia mfumo wa utangazaji wa umma. Serikali za Africa ziliitikia wito huo na kukubali kwamba utangazaji wa dola ubadilishwe na kuwa utangazaji wa umma.

Matokeo yake Serikali ya Mapinduzi Zanzibar mwaka 2000 iliruhusu kuanzishwa kwa vyombo binafsi vya habari, ikiwa ni pamoja na vyombo vya utangazaji wa radio na televisheni. Aidha katika kuitikia wito wa kubadilisha mfumo wa utangazaji wa dola kwenda utangazaji wa umma, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar mwaka wa 2010 iliunganisha Sauti ya Tanzania Zanzibar na Televisheni Zanzibar na kuunda Shirika la Utangazaji Zanzibar – Zanzibar Broadcasting Corporation – ZBC. Sera ya Utangazaji Zanzibar iko wazi kabisa kuhusu dhamira ya kuwa na utangazaji wa umma.

Kabla ya kuanzishwa kwa vituo binafsi vya utangazaji, ZBC, wakati huo STZ na TVZ- ilikuwa na ukiritimba katika utangazaji hapa visiwani. Lakini sasa shirika linakabiliwa na ushindani mkubwa kutoka ndani na nje ya Zanzibar. Hali hii ilinipa shauku ya kutaka kutathmini utendeji kazi wa Shirika la Utangazaji Zanzibar wakati huu wa ushindani katika utangazaji.Hususan, kuna maswali manne ambayo nilitaka kuyapatia majibu.

  1. Je, wananchi wa Zanzibar wanasikiliza ZBC kwa kiwango gani?

  2. Je, vipindi na mtiririko wa vipindi vya ZBC unakidhi matakwa ya wasikilizaji na watazamaji wake?

  3. Je, kuwepo vya vyombo vingi vya utangazaji Zanzibar, kumebadilisha mtazamo wa wananchi wa Zanzibar kuhusu ZBC?

  4. Utendaji kazi wa ZBC katika zama hizi za utangazaji wa ushindani ukoje?

2.0: Mbinu za utafiti.

Kupata majibu ya maswahili haya nilifanya utafiti Unguja na Pemba mwezi September 2011.Nilipeleka madodoso 500 kwa wasikilizaji na watazamaji wa ZBC walioko Unguja na Pemba. Katika madodoso 500, 490 (98%) yalirejeshwa, na kati ya hayo madodoso 297 (61%) yalitoka Unguja na 193 (40%) yalitoka Pemba. Aidha nilipeleka madodoso 100 kwa wafanyakazi wa ZBC walioko Unguja na Pemba. Unguja nilipeleka madodoso 50 na Pemba nilipeleka madodoso 50. Katika madodoso 100 yaliyopelekwa kwa wafanyakazi wa ZBC, 78 (78%) yalirejeshwa.

Nilifanya mahojiano ya ana kwa ana na waandishi wa habari na watangazaji 7 kutoka vituo viwili binafsi vya utangazaji – Zenzi FM na HITS FM, viongozi 5 kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo, Tume ya Utangazaji Zanzibar, ZBC na waandishi na watangazaji waandamizi.

Aidha nilifanya majadiliano na makundi matano – focus group discussions. Kundi la kwanza lilikuwa la wafanyakazi 6 toka ZBC- radio. Kundi la pili lilikuwa la wafanyakazi 7 wa ZBc- televisheni. Kundi la tatu lilikuwa la wafanyakazi 6 wa Zenji FM. Kundi la nne lilikuwa la wafanyakazi 8 wa ZSJMC. Baada ya kufanyia majadiliano na makundi haya manne nilikutana na kundi la watangazaji waandamizi 4 wa ZBC- radio kwa nia ya kutaka kuelewa zaidi na kupata ufafanuzi wa kina kwa taarifa nilizozipata katika makundi manne ya mwanzo.

3.0: MATOKEO

3.1: Utendaji kazi wa ZBC katika zama za ushindani a utangazaji

Matokeo ya utafiti yameonyesha kwamba kwa ujumla, watazamajii na wasikilizaji wengi – 256 (52.4%) wamesama utendaji kazi wa ZBC umeimarika na 220 (45%) wamesema umedorora. Lakini wafanyakazi 69 (89%) wa ZBC wamesema utendaji kazi wa ZBC umedororo na 9 (12%) wamesema umeimarika.

Utafiti umegundua kwamba wafanyakzi wengi wa ZBC wamevunjika moyo kutokana na kukosekana kwa motisha, ikiwemo mazingira mazuri ya utendaji kazi. Kwa mfano, walisema hawana vitendea kazi vya kutosha na vichaje viliopo sio vya kisasa, kukosekana kwa usafiri wa uhakika, mishahara duni, bajeti finyu na majengo ya zamani yenye samani chakavu.

Wafanyakazi wa ZBC wanaamini Serikali haina nia ya dhati ya kuigeuza ZBC kuwa shirika la utangazaji wa umma kweli. Wanaamini hivyo kutokana na walichodai kwamba serikali imeshidwa kuwawezesha kushindana na vyombo vya utangazaji vya ndani na nje ya Zanzibar.

Wafanyakazi wamedai kwamba watazamaji na wasikilizaji wengi wa ZBC wanadhani utendaji kazi wa ZBC umeimarika kwa sababu wanaangalia tu habari za kuaminika zinazotolewa na shirika hasa katika maswala ya kitaifa kama vile maafa.

3.2: Kiwango ambacho wa Zanzibari wanatazama na kusikiliza ZBC.

Utafiti umeonyesha kwamba wa Zanzibari wengi – 42% wanatazama na kusikiliza ZBC, ikifuatiwa na Zenj FM- 27.3% na Spice FM – 17%. Aidha wa Zanzibari wengi -44% wanapenda kutazama TVZ, ikifuatiwa na TBC1- 13%, Star TV – 11% na ITV- 5%.

Kwa vituo vya utagazaji vya Tanzania Bara, wa Zanzibari wengi 227 (26.3%) wanasikiliza TBC Taifa ikifuatiwa na Radio One – 139 (28.3%), halafu Radio Free Africa – 36 (7.3%). Kwa radio za nje ya Tanzania, wa Zanzibari wengi 257 (58%) wanasikiliza Idhaa ya Kiswahili ya BBC ikifuatiwa na Idhaa ya Kiswahili ya Radio Deutsche Welle 162 (36.3%) halafu idhaa ya Kiswahili ya Sauti ya Marekani- 25 (5.6%).

Ingawaje wa Zanzibari wengi wanasikiliza na kutazama ZBC, wafanyakazi wa ZBC wamekiri kwamba wengi wao ni watu wazima na wazee ambao wameridhika na weledi ya wafanyakazi wa ZBC kuzingatia utamaduni wa Mzanzibari. Aidha wamekiri kuwapoteza vijana ambao sasa wanasikiliza zaidi radio binafsi zinazotumia muda mwingi kutoa burudani ya muziki unaowavutia vijana.

Maofisa wa radio binafsi wamesema sio tu vijana wanavutiwa na muziki lakini wamechoshwa na ZBC ambayo bado inaonekana ni sauti ya serikali ambayo inaitetea wakati wote. Wamesema vituo vya radio binafsi vimekuwa wasemaji wa wananchi. Vinaokosoa serikali, lakini pale ambapo hapana budi wanisifia.

3.3: Vipindi na mtiririko wa vipindi vya ZBC kukidhi matakwa ya watazamaji na wasikilizaji.

Watazamaji na wasikilizaji 262 (53.4%) wa ZBC wamesema vipindi na mtiririko wake unazingatia matakwa yao lakini watazanaji na wasikilizaji 213 (44%) wamesema sio kweli. Wafanyakazi wa ZBC wapatao 59 (76%) wamesema ZBC inazingatia matakwa ya wasikilizaji na watazamaji wake. Lakini wafanyakazi 18 (23%) wamesema sio kweli.

Vipindi vinavyopendwa zaidi ni habari – 48%, michezo – 18% na muziki – 15%. Hata hivyo, wafanyakazi wamekiri kwamba ZBC ina vipindi vichache sana vinavyokidhi matakwa ya vijana na wazee wenye umri zaidi ya miaka 61.

Kuhusu mtiririko wa vipindi, utafiti umebaini kwamba sio mzuri sana kwani kwa kiwango kikubwa hauzingatii muda. Wafanyakazi wametoa sababu nyingi zinazosababisha hali hii. Kwa mfano, ZBC ina lazimika mara kwa mara kubadili mtiririko wa vipindi vyake vya kila siku kutoa nafasi kwa vipindi maalumu vinavyohusu viongozi; kutokuwepo kwa vipindi; vipindi kuchelewa kutengenezwa; kukosekana kwa usafiri; uchache wa vitendea kazi na wafanyakazi; bajeti finyu ya uandaaji wa vipindi.

3.4: Mtazamo wa Zanzibari kuhusu ZBC kutokana na wingi wa vituo binafsi vya utangazaji.

Utafiti umeonyesha kwamba asilimia 61 ya wasikilizaji na watazamaji wa ZBC wana mtazamo chanya na asilimia 39 wana mtazamo hasi kuhusu ZBC. Wale wenye mtazamo chanya wamekiri kwamba utangazaji wa umma ni muhimu lakini wametaka hatua za haraka zichukuliwe ili nao wasije wakawa na mtazamo hasi. Wale wenye mtazamo hasi wamesema ZBC imeendelea kuwa sauti ya seriakli wakati vituo binafsi vya utangazaji vimekuwa sauti ya wananchi wanyonge.

Wafanyakazi 33 (49%) wana mtazamo hasi kuhusu ZBC na 18 (23%) wana mtazamo chanya. Wafanyakazi 22 (28%) hawakujibu swali. Wafanyakazi wenye mtazamo hasi kuhusu ZBC wanaamini ufinyu wa bajeti na msukumo wa kisiasa ndiyo matatizo sugu yanayoathiri utendaji kazi wa ZBC. Wamedai kwamba ZBC ina wafanyakazi wenye uzoefu, weledi na moyo wa dhati kulitumikia shirika kuhakikisha linafanya kazi vizuri, lakini wanaamini seriakli imeshindwa kuwawezesha kuifanya kazi hiyo na hivyo kuwavunja moyo.

Wafanyakazi hao, kwa ujumla wao, wanakiri kwamba jinsi shirika linavyofanya kazi hivi sasa ni utangazaji wa dola na ndiyo maanda wana mtazamo hasi kuhusu ZBC kufanyia kazi ya utangazaji wa umma.

4.0: MAPENDEKEZO

4.1: Uanzishwaji wa utangazaji wa umma wa kweli.

Wadau wa tasnia ya habari hapa Zanzibar waishawishi serikali ipitishe sheria itakayoifanya ZBC kuwa shirika la utangazaji wa umma ki kweli kweli. Wadau waitumie Sera ya Utangazaji Zanzibar kuhakikisha sheria inazingatia yaliyomo kwenye sera na serikali inaliachia shirika kujiendesha kama shirika la utangazaji wa umma.

4.2: Kugharamia uangazaji wa umma.

4.2.1: Wa Zanzibari wajadili na kukubaliana mfumo muafika wa kugharamia utangazaji wa umma ili mradi mfumo watakaokubaliana usiruhusu uhuru wa ZBC kuingiliwa.

4.2.2: Serikali iruhusu ZBC kubaki na fedha zinazotokana na matangazo pamoja na udhamini wa vipindi.

4.3: Uandaaji wa vipindi

Kazi muhimu kuliko zote ya ZBC ni uandaaji wa vipindi. Hivyo ni lazima Shirika litoe kipaombele kwa uandaaji wa vipindi. Lazima shirika liandae vipindi vya aina mbalimbali, vinavyolenga watu wa makundi mbalimbali na vyenye maudhui mbalimbali.

4.4: Kuimarisha mazingira ya utendaji kazi.

SMZ imarishe mazingira ya kufanyia kazi kwa : kukarabati majengo; kitao vitendea kazi vya kutosha na vya kisasa; kuwapa usafiri wafanyakazi kwenda kuandaa vipindi, kuwapa motisha.

5.0: Pendekezo la utafiti mwingine.

Utafiti ulipofanya Septembe 2011, ZBC ilikuwa bado haijaanzishwa rasmi kwa sheria iliyopitishwa na Baraza la Wawakilishi ili kubaini karma ile dhamira ya kuanzisha uangazaji wa umma iliyomo kwenye Sera ya Utangazaji imezingatiwa na ZBC inajiendesha karma shirika la utangazaji wa umma. Hivyo, kuna haja kufanyika utafiti mwingine miaka mitatu baadae kubaini kama ZBC ni shirika la utangazaji wa umma au utangazji wa dola uliovikwa sare ya utangazaji wa umma.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s