Vyombo vya habari vifuate maadili-Dk Shein

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein,akizungumza na Uongozi wa Baraza la Habari Tanzania,ulipofika Ikulu Mjini Zanzibar kwa mazungumzo,chini Makamo Mwenyekiti wa baraza hilo,Chande Omar,(wa pili kulia) pia Katibu Mtendaji wa Tume ya Utangazji ya Zanzibar.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, amekutana na uongozi wa Baraza la Habari Tanzania (MCT) na kueleza haja kwa vyombo vya habari na watendaji wake nchini kufuata maadili ya fani hiyo kwani maadili ndio yanayoongoza fani zote. Dk. Shein aliyasema hayo wakati alipokuwa na mazungumzo na uongozi wa Baraza la Habari Tanzania, ulioongozwa na Makamu Mwenyekiti wake Chande Omar,ambaye pia ni Katibu Mtendaji wa Tume ya Utangazaji Zanzibar, uliofika Ikulu mjini Zanzibar.

Katika mazungumzo hayo, Dk. Shein aliueleza uongozi huo kuwa migogoro mingi inayotokea katika vyombo vya habari inatokana na kutofuatwa maadili ya sekta hiyo, hivyo kuueleza uongozi huo haja ya kulisimamia kwa nguvu zake zote jambo hilo kwani litaijengea heshima Baraza hilo, Bodi pamoja na viongozi wake.

Alisema kuwa yeye mwenyewe binafsi amevutiwa na malengo na mikakati ya Baraza hilo tokea kuanza kazi zake hatua ambayo imepelekea kupatikana mafanikio makubwa katika sekta ya habari hapa nchini.

Dk. Shein alisema kuwa licha ya kuwa Baraza hilo lina kazi nyingi na ngumu lakini ipo haja ya kulisiamamia suala la maadili ili liweze kuiweka sekta ya habari pazuri hapa nchini sanjari na kuwa wawazi.

Aliueleza uongozi huo kuwa kwa kawaida jamii inatakiwa kupata habari zilizo sahihi ili kuondosha migogoro katika jamii, hivyo Baraza lina kazi ngumu ya kuhakikisha jamii inapata habari sahihi na vyombo vya habari pamoja na taasisi za habari zinafuata maadili.

Dk. Shein alisema kuwa jambo la kuzuia migogoro isitokee juu ya vyombo vya habari ni kusisitiza kufuatwa kwa maadili na kulitaka Baraza kupanga taratibu zake vizuri katika kuhakikisha kila baada ya muda linavikumbusha vyombo vya habari maadili ya fani hiyo.

Alieleza kuwa wananachi wana uhuru wa kupata habari, kusema na kutoa maoni yao kwa mujibu wa Katiba zote mbili za Tanzania, hivyo itakuwa ni jambo la busara iwapo watapata habari zenye uhakika na usahihi zaidi.

Dk. Shein alisema kuwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar chini ya uongozi wake itaendelea kuhakikisha wananchi wanapata haki yao hiyo ya msingi huku akieleza juu ya taratibu zilizowekwa na Serikali kwa viongozi kutoa habari kwa wananchi ambapo hata yeye mwenyewe ameshaanza utaratibu huo.

‘Mimi nimekuja na mfumo wa kutoa habari kwani wananchi wanahitaji kupata habari juu ya nchi yao na maendeleo yao…. hakuna haja ya kuficha habari”,alisisitiza Dk. Shein.

Aidha, Dk. Shein alisisitiza juu ya suala zima la kuwepo kwa kumbukumbu na historia katika vyombo vya habari vya hapa Zanzibar kwani Zanzibar ina historia kubwa katika sekta hiyo kwa Afrika Mashariki na Afrika nzima kwa jumla.

Dk. Shein alitoa pongezi kwa Baraza hilo kwa namna inavyotoa mafunzo yake kwa vyombo vya habari pamoja na namna linavyosimamia suala zima la upanishi.

Nae Katibu Mtendaji wa Baraza hilo Bwana Kajubi Mukajanga alieleza kuwa Baraza hilo lililoanzishwa mwaka 1995 liliundwa kutokana na haja ya kuwepo kwa usimamizi wa vyombo vya habari nchini Tanzania, baada ya kufunguliwa milango kwa vyombo vya habari binafsi nchini.

Mukajanga alieleza kuwa kutokana na hali hiyo ndipo mnamo mwaka 1997 kazi rasmi ilianza na mwaka 2003 likafungua afisi zake hapa Zanzibar ambapo kwa sasa Baraza hilo lina wanachama 15 ha Zanzibar zikiwemo Klabu za waandishi wa habari, taasisi za vyombo vya habari vikiwemo vya Serikali na vyenginevyo.

Kwa upande wa Baraza hilo Katibu huyo alieleza kuwa limekuwa likitoa mafunzo kwa vyombo vya habari na watendaji wake Unguja na Pemba, kufanya upatanishi na kusimamia demokrasia, kuiendeleza siku ya vyombo vya habari duniani tarehe 3 Mei kila mwaka, kutoa machapisho sanjari na kufanya utafiti.

Aidha, Katibu huyo alileza kuwa Baraza hilo limekuwa likitoa mafunzo kwa vijana wanaotoka vyuoni na wanaoendelea katika fani hiyo ya habari, kufanya mafunzo ya ndani kwa wanahabari kwa kupeleka wataalamu katika taasisi zao ili wakatoe elimu.

Nae Makamu Mwenyekiti alieleza mafanikio ya Baraza hilo ambalo limekuwa ni kigezo kikubwa kwa nchi za Afrika Mashariki na kuahidi kulisimaia suala zima la historian a kumbukumbu kwa vyombo vya habari nchini.

Nae Meneja wa Udhibiti wa Viwango wa Baraza hilo Bi Pili Mtambalike, akieleza jinsi uongozi huo unavyolifanyia kazi suala zima la maadili kwa vyombo vya habari huku ukieleza matumaini yao makubwa juu ya Mabadiliko ya Sheria. Uongozi huo pia, ulimkabidhi Rais machapisho kadhaa ikiwemo Katiba ya Baraza hilo.

Advertisements

One response to “Vyombo vya habari vifuate maadili-Dk Shein

  1. VYOMBO VYA HABARI VITUMIKE KUHAMASISHA WANANCHI WA ZANZIBAR WOTE KUSHIRIKI KATIKA HARAKATI ZA KUDAI UHURU WA ZANZIBAR 2012 KUTOKA MIKONONI MWA MAKAFIRI WA TANGANYIKA. Mvunja nchi ni mwananchi ni ukweli usiofichika kuwa viongozi wa smz ndio walioifanya zanzibar kuwa koloni la NGURUWE WEUSI WA TANGANYIKA. TRA wanakusanya mapato kutoka katika MISHAHARA YA WAFANYAKAZI WA ZANZIBAR.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s