Ziara ya Maalim Seif ,Wizara ya Habari

Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad akisalimiana na Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji Zanzibar (ZBC) Hassan Mitawi katikati ni Abdallah Mohammed Mhariri Mkuu wa Gazeti la Zanzibar Leo, Maalim Seif alifanya ziara katika vyombo vya habari leo

Makamu wa Kwanza wa Rais Maalim Seif Sharif Hamad amesema changamoto zinazotokea katika utendaji kazi katika Taasisi mbali mbali ni chachu katika kuleta maendeleo na kujikwamua pale tulipofika. Amesema bila ya kuwa na changamoto maendeleo yataendelea kusuasua kwani kutakuwa hakuna hatua itakayopigwa mbele katika kuleta mafanikio.

Maalim Seif aliyaeleza hayo leo wakati akizungumza na uongozi wa Vyombo vya Habari vya Serikali ikiwemo Idara ya Habari Maelezo,Shirika la Utangazaji Zanzibar ZBC na Gazeti la Zanzibar ikiwa ni mfululizo wa kutembelea Idara za Wizara ya Habari Utamaduni Utalii na Michezo.

Amesema vyombo vya habari ndio kiungo kikubwa kati ya wananchi na Serikali hivyo ni vyema kufanya kazi kwa uadilifu na kuweza kukabiliana na vikwazo ambavyo vinaweza kurudisha nyuma juhudi mbali mbali zinazochukuliwa na wananchi na hata Serikali.

Akizungumzia juu ya mafunzo kwa wanahabari, Maalim Seif alizitaka taasisi hizo kuwa na mpango mzuri wa kuwapeleka waandishi wa habari masomoni na katika mafunzo mengine ili waweze kukabiliana na kasi ya maendeleo ya teknolojia ambayo kwa sasa inakwenda kwa kasi kubwa.

Amesema masomo humjengea uwezo mwana habari wa kuweza kutumia kifaa chochote na kuweza kuibua mambo kadha ikiwemo uwezo wa kumkabili mtu yeyote bila ya woga au wasi wasi.

Amewataka waandishi wa habari katika Idara hiyo kuendelea kuwa wabunifu katika uandishi na kuandika habari zilizofanyiwa utafiti wa kina bila ya woga wowote

Maalim Seif alisisitiza haja ya kuwa na vifaa vya kisasa vinavyokwenda na wakati ili kuweza kufanya kazi kwa ufanisi , haraka na kwa wepesi zaidi.

Mapema Makamu wa Kwanza wa Rais aliipongeza Idara ya Habari kwa utendaji wake hasa kwa vile inatoa huduma ndani na nje ya nchi na kuishauri kuanza kupeleka taarifa zake katika vituo vyengine vya kigeni kama BBC,AFP CNN na REUTERS ili kuweza kutumia taarifa hizo na kuitangaza Zanzibar.

Akizungumzia suala la mishahara alisema kuwa viwango vya mshahara kwa wafanyakazi wa Vyombo vya habari ni vidogo kulingana na hali halisi na kupendekeza viwango hivyo kubadilishwa kulingana na wakati uliopo.

“Binadamu ni binadamu anaangalia maslahi yake tukisema uzalendo tu wengi watashindwa”alisema Maalim Seif

Katika Ziara hiyo Maalim Seif alitembelea Idara ya Habari Maelezo,Shirika la Magazeti ya Serikali,Shirika la Utangazaji la Zanzibar ZBC pamoja na maeneo ya Mitambo ya kurushia matangazo ya Shirika hilo.

Imetolewa na Maelezo Zanzibar

Advertisements

One response to “Ziara ya Maalim Seif ,Wizara ya Habari

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s