Jengo la ZSSF laungua moto

Makamo wa Pili wa Rais Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi (hayupo pichani)alitembelea eneo la Mfuko wa Hifadhi wa Jamii Zanzibar (ZSSF) huko Kilimani Mjini Unguja ambapo chumba kimoja cha jengo hilo kiliungua moto lakini moto huo uliweza kudhibitiwa na gazri la zima moto leo asubuhi

Kikosi cha zima moto na uokozi kimefanikiwa kuuzima moto uliotokea katika jengo la Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF) ililiopo Kilimani Mjini Zanzibar. Chanzo cha Moto huo kimesababishwa na khitilafu za umeme uliotokea majira ya saa nne na nusu za asubuhi na kuweza kudhibitiwa majira ya saa tano.

Mmoja wa wafanyakazi wa usafishaji wa Jengo hilo, Vuai Haji aliwaeleza waandishi wa habari kwamba hitilafu hiyo imetokea katika Chumba cha iliyokuwa afisi ya bodi ya mapato Zanzibar (ZRB) cha mtandao wa kompyuta.

Usafishaji huo umekuja kufutia watendaji wa bodi hiyo kuhama na kujitayarisha kukabidhi ofisi hiyo kwa uongozi wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii hapo kesho.

Msaidizi Kamishna wa Kikosi cha zima moto na uokozi Kamanda Simai Ame Simai amesema watedaji wake wamelazimika kuvunja vioo vya dirisha la Ofisi hiyo kwa lengo la kuzima moto ili kunusuru kuzagaa kwa maafa zaidi.

Kamanda Simai ametoa wito kwa jamii kutoa Taarifa za haraka pale yanapotokezea matukio kama hayo ili waweze kupata huduma za haraka na uhakika.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alifika katika eneo hilo kujionea hali halisi ya tukio hilo.
Akizungumza na Uongozi wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar Balozi Seif ameagiza kutolewa kwa Elimu ya Huduma za mwanzo ya kukabiliana na maafa kwa wafanyakazi wa Ofisi na Taasisi za Umma. Balozi Seif alisisitiza pia kufuata utaratibu wa kuzimwa kwa mashine zote za umeme wakati wanapomaliza shughuli zao za kikazi. Hadi sasa bado haijajuilikana hasara iliyopatikana kutokana na moto huo.

Advertisements

3 responses to “Jengo la ZSSF laungua moto

  1. Hii ya Kuungua jengo hili inashtusha sana. isiwe kuna watu wesha pora pesa za walala hoi na sasa wanataka wapoteze ushahidi. Kwanza ofisi hii imegubikwa na usiri mkubwa. Sisi wenye pesa zetu hatujuwi hali zake.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s