Soma gazeti la Annuur kila Ijumaa

ANNUUR1002

Tangazo la wanaotaka kupendekeza majina kwa ajili ya mchakato wa katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wampelekee Rais Kikwete

HIVYO BASI, MIMI, JAKAYA MRISHO KIKWETE, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa masharti ya kifungu cha 6(6) cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, 2011, NATOA tangazo lifuatalo: Jina 1. Tangazo hili litaitwa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba (Mwaliko wa Orodha ya Majina)(Wajumbe wa Tume) la mwaka, 2012. Mwaliko wa orodha ya majina

 

TANGAZO LA SERIKALI NA. 66 la tarehe 24/02/2012

SHERIA YA MABADILIKO YA KATIBA YA MWAKA

(NA. 8 YA MWAKA 2011)

TANGAZO

(Limetolewa chini ya kifungu cha 6)

KWA KUWA, kifungu kidogo cha (1) na (2) cha kifungu cha 6 cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya mwaka,

2011 kinampatia mamlaka Rais, baada ya kushauriana na kukubaliana na Rais wa Zanzibar na kwa kuzingatia

msingi wa usawa wa wajumbe kutoka kila upande wa Jamhuri ya Muungano kuteua Mwenyekiti, Makamu

Mwenyekiti, na wajumbe wengine wa Tume wasiopungua ishirini na wasiozidi thelathini kama inavyoelekezwa

na kifungu cha 7(1);

NA KWA KUWA, katika kufanya uteuzi wa wajumbe wa Tume atalazimika kutilia maanani:

(a) uzoefu katika kufanya mapitio ya katiba na sifa za kitaaluma za wajumbe kwenye mambo ya katiba, sheria, utawala, uchumi, fedha na sayansi ya jamii;

(b) jiografia na mtawanyiko wa watu katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; na

(c) umri, jinsia na uwakilishi wa makundi mbalimbali ya kijamii;

NA KWA KUWA, vifungu vidogo vya (4) na (5) vya kifungu cha 6 vinaeleza kwamba mtu hatakuwa na sifa ya kuteuliwa

kuwa mjumbe wa Tume isipokuwa kama ni mwaminifu wa hali ya juu na ana tabia isiyotiliwa mashaka na jamii na mtu

huyo si mtumishi katika vyombo vya usalama au si raia wa Tanzania;

NA KWA KUWA, kifungu kidogo cha (6) cha kifungu cha 6 kinamtaka Rais kualika vyama vya siasa vyenye usajili wa

kudumu, jumuiya za dini, asasi za kiraia, jumuiya, taasisi na makundi mengine ya watu yenye malengo yanayofanana

kuwasilisha kwa Rais orodha ya majina ya watu kwa ajili ya kuteuliwa kuwa wajumbe na ambayo itaonyesha umri, jinsia,

uzoefu, sifa na mahali mtu huyo anapoishi;

NA KWA KUWA, Rais ana nia ya kuwateua wajumbe wa Tume kwa kuzingatia masharti ya sheria;

HIVYO BASI, MIMI, JAKAYA MRISHO KIKWETE, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa masharti ya kifungu cha 6(6) cha Sheria ya

Mabadiliko ya Katiba, 2011, NATOA tangazo lifuatalo:

Jina 1. Tangazo hili litaitwa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba (Mwaliko wa Orodha ya Majina)(Wajumbe wa Tume) la mwaka,

2012.

Mwaliko wa

orodha ya

majina

2.-(1) Tangazo la Mwaliko unatolewa kwa vyama vya siasa vyenye usajili wa kudumu, jumuiya za dini, asasi za kiraia,

jumuiya, taasisi na makundi mengine ya watu yenye malengo yanayofanana kuwasilisha kwa Rais orodha ya majina ya watu

watakaoteuliwa kuwa wajumbe wa Tume.

(2) Orodha ya majina itakayowasilishwa kwa mujibu wa kifungu kidogo cha (1), itapaswa kuwa na majina yasiyozidi matatu

na itaonyesha umri, jinsia, uzoefu, sifa na mahali anapoishi kila mtu aliyemo katika orodha.

Muda wa

kuwasilisha

orodha

3. Kipindi ambacho orodha ya majina itawasilishwa kwa Rais kwa mujibu wa aya ya 2, kitakuwa ni siku ishirini na moja

zitakazohesabika kuanzia tarehe 25 Februari, 2012 na kitakoma tarehe 16 Machi, 2012.

Kuwasilisha

orodha

4.-(1) Orodha ya majina itawasilishwa kwa Rais kwa maandishi ama moja kwa moja kwa mkono au kwa rejista ya posta

kupitia anuani kama ifuatavyo:

Ama: Katibu Mkuu Kiongozi,

Ikulu,

S.L.P. 9120,

DAR ES SALAAM.

Au: Katibu wa Baraza la Mapinduzi na

Katibu Mkuu Kiongozi;

Ofisi ya Rais,

S.L.P. 4224,

ZANZIBAR.

(2) Tangazo hili litakoma tarehe 16 Machi, 2012.

KWA AMRI YA RAIS

Dar es Salaam, PENIEL M. LYIMO,

24 Februari, 2012 Kaimu Katibu Mkuu Kiongozi

 

Advertisements

2 responses to “Soma gazeti la Annuur kila Ijumaa

  1. Shime wazanzibari wenye uwezo, sifa na mtizamo wa maslahi kwa nchi ya Zanzibar wajitokeze. Tupeleke ‘vichwa’ madhubuti ili tukaitetee nchi yetu na hatimae kuzaa katiba mpya kulingana na matakwa ya wananchi wa Zanzibar na Tanganyika.

  2. Nimefarijika kusoma habari hizi ambozo ni muhimu sana kwetu sisi wazanzibari. Napenda kutoa pendekezo langu kwa wahusika wakuu wa kusimamia suala hili la mchakato wa madiliko ya katiba. Ninawataka kuanda mpango madhubuti wa kuwahamasisha vijana kushiriki ktk kutoa mapendekezo yao kwani wingi wetu tunaona haya mambo ya siasa kama hayana umuhimu kwetu, wengi tunapoteza muda mwingi kwenye facebook pamoja na kusikiliza musiki.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s