CCM waanza kupanga safu za uongozi

Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM Balozi Seif Ali Iddi akiufungua Mkutano Mkuu wa Umoja wa Wapanda Mapiki Piki wa CCM hapo ukumbi wa Mikutano wa CCM Mkoa uliopo Amani Mjini Zanzibar. Kulia ya Balozi ni Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa Mjini ambae pia ni Mbunge Viti Maalum Mh. Tauhida Gallos Nyimbo na Kulia ya Balozi ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa Mjini Magharibi Nd. Yussuf Mohammed Yussuf.

Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM Balozi Seif Ali Iddi akiufungua Mkutano Mkuu wa Umoja wa Wapanda Mapikipiki wa CCM hapo ukumbi wa Mikutano wa CCM Mkoa Amani Mjini Zanzibar. Kushoto ni Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa Mjini ambae pia ni Mbunge Viti Maalum, Tauhida Gallos Nyimbo na kulia ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa Mjini Magharibi, Yussuf Mohammed Yussuf.

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar kimekiri kupata uvamizi katika jumuiya zake na kuahidi kitendo hicho kutorejewa tena ili kupanga safu nzuri za uongozi bora wa chama hicho. Hayo yameelezwa na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Balozi Seif Ali Iddi jana wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Umoja Wapanda Mapikipiki wa CCM katika Ukumbi wa Chama hicho Mkoa Amani Mjini Zanzibar ambapo alisema kusit9olewe mwanya wa watu wenye lengo la kuharibu.

“ CCM haioni shida kupoteza wanachama watatu, watano au zaidi ambao wana tabia na njama za  kukidhoofisha chama kwa maslahi yao binafsi”. Alisema Balozi Seif katika mkutano huo ambao wa kuchagua viongozi  watakaoongoza Umoja huo katika kipindi cha miaka mitano ijayo.

Balozi Seif ambae pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alisema kuna kipindi CCM iliwahi kupata watu waliojipandikiza na kujiingiza ndani ya Jumuiya na baadhi ya taasisi zake na hatimaye kupelekea matatizo hasa  katika chaguzi zilizopita.

Aidha alitahadharisha kwamba wakati umefika kwa Wanachama wa Chama hicho kuwa makini na watu kama hao hasa katika kipindi hichi kinachoingia cha chaguzi mbali mbali za viongozi wa chama hicho cha CCM.

Hata hivyo Balozi Seif amewaomba Vijana hao kujisaidia katika kuachana na mifarakano kwa lengo la kutengeneza safu nzuri ya muelekeo bora wa uongozi makini.

Balozi Seif amewataka wanachama wa umoja wa wapanda mapikipiki wa CCM kufanya maamuzi magumu na kusisitiza kutumika busara katika kuhakikisha wanachagua viongozi bora kwa ajili ya kujenga safu ya ushindi wa chama hicho kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.

Akiwapongeza vijana hao Balozi Seif aliwaomba kuendelea kukiimarisha Chama chao kwani wao ndio nguvu ya Chama wakati wote.

Balozi Seif ameahidi kwamba kwa kushirikiana na mlezi wa Umoja huo ataangalia hatua za namna ya kuisaidia Taasisi hiyo muhimu kwa CCM katika masuala ya  uhamasishaji Wanachama.

Katika Taarifa yao iliyosomwa na Katibu wa umoja huo wa wapanda Mapiki Piki Mkoa Mjini Magharib, Amour Ali Mwinyi amesema umoja huo umepata mafanikio makubwa tokea kuanzishwa kwake.

Amour alisema Taasisi yao bado inakabiliwa na baadhi ya changamoto zinazokwaza utendaji wao ikiwa ni pamoja na msingi wa kianzio cha kuelekea katika uzalishaji mali.

Mapema Mlezi wa Umoja wa Wapanda Mapikipiki Mama Asha Suleiman Iddi amempongeza Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein kwa jitihada zake za kuunga mkono umoja huo.

Mama Asha ameziasa Taasisi za CCM zinazoingia kwenye uchaguzi kuwachagua Viongozi wao kwa kigezo cha uwezo na kuachana na tabia ya kuangalia udugu au rafiki.

Alisema tabia hiyo ya kuchaguana kwa udugu na urafiki ikiendekezwa inaweza kukijengea mazingira mabovu Chama katika utekelezaji wa Sera na Majukumu iliyojipangia ndani ya ilani yake.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s