Chama kipya chaundwa Tanzania

Aliyekuwa Meneja Kampeni wa Mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Professa Ibrahim Lipumba kwa tiketi ya Chama Cha Wananchi (CUF), Said Miraji amejitoa katika hicho na kuunda chama chake kipya kiitwachoAlliance for Democratic change (ADC)

Nchini Tanzania kumeundwa chama kipya cha kisiasa kwa jina la Alliance for Democratic change ADC. Kuundwa kwa chama hicho kunafuatia tangazo la kujitoa kwa wahusika kutoka chama cha upinzani CUF. ADC Inaongozwa na Said Miraji aliyewahi kushika nyadhifa mbali mbali katika CUF ikiwa ni pamoja na kuwa Katibu wa Katibu mkuu ,Mkurugenzi wa Vijana wa taifa na pia Mkurugenzi wa kamati ya Ulinzi ya taifa ya chama hicho. Mohammed Abdulrahman amezungumza na Bw.Said Miraji akiwa Dar es salaam na kwanza alielezea madhumuni ya kuunda ADC. Kwa kupata maelezo zaidi Mwandishi wa DW, Mohammed Abdurahman alizungumza na Muanzilishi wa chama hicho kipya, Said Miraji. Bonyeza hapa. 

 

 

Advertisements

5 responses to “Chama kipya chaundwa Tanzania

  1. KILA LA HERI SAID MIRAJI NA TUNASUBIRI KWA HAMU TUONE MWISHO WA SIASA ZAKO ZA UBABAISHAJI CC TUNAKUJUA WEWE NI KIBARAKA UNAETUMIWA NA HAMAD RASHID NA HAO WALIOKUHADAENI KWAMBA WAMERUDISHA KADI ZA CUF NDIO WA MWANZO WATAKAOKUKATAENI SIKU MKITAFUTAS USAJILI WA KUDUMU

  2. Nnachoshuri kwa waheshimiwa wa chama kipya wajue wazi kua chama sio lelemama. Tunawasubiri tuone nguvu za soda zitaishia wapi. Mh Hamad Rashid nna imani atapeperusha bendera ya chama chake kipya katika jimbo la Wawi 2015.

  3. ADC DIRA YA MABADILIKO sisi tuko tayari kwa lolote kwani CUF ni CCM B hiyo inafahamika si mulimsikia Seif Sharif aliposema hawezi kuilaumu serekali kwani yeye ni sehemu ya serekali,pia akasema iwapo atapewa uenyekiti wa CCM yupo tayari kuenda huko hii inamaanisha yeye ni mlafi wa madaraka

  4. Poleni sana siasa si lelemama wala utapeli, siasa anahitajika mtu akubalike mbele ya jamii. na kinachomfanya mtu akubalike ni ukweli wake
    Nyinyi waasisi wa chama kipya tunawajuwa utandu na ukoko, nendeni mkatapeli mrima , labda huko munaweza mukakubalika, kwani si ajabu huko alikubalika Babu wa Loliondo,
    Lakini Zanzibar mutaula na chuwa

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s