Uhaba wa mafuta wazua balaa Zanzibar

Makamu wa pili wa rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiangalia kima cha mafuta katika baadhi ya vituo alivyovitembelea ghafla ambacho hakizidi lita 1000

CHANZO cha uhaba wa mafuta ya magari hapa Zanzibar kimeelezwa kinatokana na mfumo mbaya uliopo wa kuachiwa kampuni moja ya usambazaji wa mafuta nchini Tanzania. Meneja Mkuu wa Zanzibar Petroelum, Bw. Collin Chemngorem alimueleza Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi kwamba tatizo kubwa ni mfumo uliopo hivi sasa wa uagizaji na usambazaji wa mafuta nchini ambapo umepelekea huduma hiyo pungua hapa Zanzibar.

Balozi Seif Ali Iddi amefanya ziara ya ghafla katika baadhi ya Vituo vya Mafuta ya vyombo vya moto ndani ya mkoa wa Mjini Magharibi jana ili kusikiliza malalamiko mengi ya wananchi kutokana na uhaba mkubwa wa mafuta uliotokea kwa siku tatu sasa.

Bw. Collin alisema upungufu huo umekuja kutokana na mlolongo mkubwa wa upakizi wa mafuta kwenye meli katika kituo cha pamoja Mjini Dar es salaam hali iliyopelekea meli inayoleta mafuta Zanzibar kukaa kwa karibu mwezi mmoja kutokana na ufinyu wa kima cha mafuta yake ya lita milioni sita ambazo hutumika kwa mwezi.

Alisema mfumo huo wa sasa (Belco System) unatoa fursa zaidi kwa Meli zenye uwezo wa kupakia Mafuta kuanzia kima cha lita Milioni 30,000,000/-.

Meneja mkuu huyo wa Zanzibar Petroleum alimueleza Balozi Seif kwamba Kampuni zao kwa pamoja zimeshaandika Waraka na kuuwasilisha Serikalini ili mgao wa Zanzibar wa Mafuta wa lita milioni sita uingizwe katika utaratibu Maalum badala ya ule wa jumla.

Aliiomba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar izungumze na Serikali ya Muungano wa Tanazania kufikiria Tenda zinazotolewa pia zilenge na Zanzibar.

Naye Meneja Biashara wa Kampuni ya United Petroleum (UP) Bwana Altaf Jiwan alielezea usumbufu wanaopambana nao wa kutozwa kodi mara mbili wakati wa kusafirisha mafuta yao kutoka Tanzania Bara na Zanzibar.

Bw. Altaf ameipongeza Serikali kwa hatua inazochukuwa za kuzishirikisha Taasisi binafsi wakati wa kutunga Sera na Sheria zinazozihusu Taasisi hizo.

Akizungumza na wafanyabiashara hao katika ziara hiyo Balozi Seif alisisitiza ni vyema kwa wafanyabiashara wakaendelea kujenga urafiki na Wananchi wakati wanapotoa huduma hiyo.

Balozi Seif alisema Wananchi walio wengi wa Zanzibar bado wanategemea usafiri katika harakati zao za kimaisha.

“ Mwananchi anapokosa huduma ya usafiri kwa tataizo la mafuta wakati maisha yake hutegemea kilimo ni kumbebesha ukali wa maisha na kumuongezea umaskini ”. Alitahadharisha Balozi Seif.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alibahatika kuvitembelea vituo vya mafuta vya uwanja wa ndege, kiembe samaki, kijangwani na batini. Bado hakujawa na upungufu wa mafuta aina ya diesel.

Ziara hiyo imekuja kufuatia uhaba wa mafuta ya aina ya Petroli uliojitokeza kwa karibu mwezi mmoja sasa na kupelekea usumbufu kwa Wananchi walio wengi wanaotumia usafiri vya vyombo vya moto.

Balozi Seif alishuhudia msongamano mkubwa wa Magari katika Kituo cha Mafuta cha uwanja wa ndege ambapo wauzaji wa Vituo hivyo wamesema mgao wanaopata katika kipindi hichi hauzidi Lita 1,000 tu ambazo hazikidhi hata kidogo mahitaji ya wateja wao.

Wauzaji hao walimueleza Balozi Seif kwamba hakuna ujanja unaotumika wa ufichaji wa Bidhaa hiyo kwa kisingizio cha kutaka kupandisha bei. Balozi Seif alionya vikali tabia ya baadhi ya watu kuweka mafuta Majumbani na kwenye madumu kitendo ambacho ni hatari kwa maisha yao na Jamii inayowazunguuka.

“ Tumekuwa mashahidi wa matukio tofauti yanayojichomoza katika kipindi yanapoadimika mafuta ambayo mengi huleta athari ya vifo kutokana na uzembe wa uwekwaji wa mafuta ovyo katika makaazi ya Watu ”. Alionya Balozi seif.

Balozi Seif baadaye alivitembelea Vituo vya hifadhi ya mafuta vya Gapco, Zanzibar Petroleu, United Petroleu na BP Vilivyopo Mtoni nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.

Tatizo la uhaba wa mafuta hivi sasa limekuwa likijirudia mara kwa mara ambapo uchunguzi unaonesha hufichwa kwa makusudi ili wafanyabiashara wauze bei ya juu.

Kufuatia tatizo hilo wajanja wamepata mwanya wa kununua mafuta hayo na kuyaweka katika mageloni na baadae kuuza kwa bei ya juu ambapo yanaponunuliwa katika mageloni na kuyauza vipembeni kwa bei ya juu sana. 


Advertisements

13 responses to “Uhaba wa mafuta wazua balaa Zanzibar

 1. “”Hata hivyo Waziri wa Miundo Mbinu na Mawasiliano, Hamad Masoud Hamad, alisema Mamlaka ya Usafirishaji Baharini Zanzibar (ZMA) imelazimika kupiga marufuku uingizaji mafuta kwa kutumia huduma ya meli kwa meli kutokana na biashara ya magendo ya mafuta.

  Hamad alisema serikali imezuia kwa muda utaratibu huo wakati ukiandaliwa utaratibu mzuri ambao utasaidia kuthibiti biashara ya magendo kwenye nishati ya mafuta ambayo imekuwa ikisababisha Serikali ya Mapinduzi ya Zanziba kupata Hasara ya Sh.milioni 300 kwa mwezi.””

  Hayo ni maneno ya Mh Waziri mwenye Dhamana kama nilivyo yanukuu katk gazeti la Nipashe. Hapa mojakwamoja tunaona uzaifu wa kitendaji wa viongozi wetu. Iweje Mh Waziri anatoa kauli kama hii bila ya kuangalia kwa kina ni jinsi gani wananchi wanaumia na hali gumu ya maisha? Na iwe kweli kuawa mafuta yakichakachuliwa kimagend na serikali inakosa mapato je Mh Wazir kabla ya kutoa maamuzi mlifikiria athari gani inaweza kupatikana? Na kwanini msiweke mkakati wakukabiliana nathari itayotokea baada ya hayo maamuzi.
  Mimi kwa hili sotowacha kumkumbuka Dk Salmin Amour, Katika awamu yake ya uwongozi Zanziba ilikua na mbavu ijapo kidogo katika mabo ya ke ya ndani Kulikuwa na sera na mipango maalum ya uagizwaji na usambazaji wa mafuta. Nawa haikutokea kupanda bei kiholela seuze kuwa haba kabisa nishati hii. Si mafuta pekeyake bali bidhaa nyingi zikipatika nan Zanziba tena kwa urahis kabisa.

  Kauli ya Mh Masoud (wazir) inaonesha wazi kua baadhi ya viongodhi wetu hawajabobea kiutendaji Namuomba Rais wetu mpenzi afikirie vizuri anapoteua na anaouwapa dhamana. Isiwe tu eti kuridhisha upande fulani.
  suaala hili la uhaba wa mafuta ni changamoto kubwa katika maisha ya wanzanzibar wanaoumia naukali na ugumu wa maisha sika bada yasiku.
  MUNGU IBARIKI ZANZIBAR NA WATU WAKE. heko GNU

  • Hongera kwa kueleza ukweli zanzibar hakuna serekali bali kuna wezi wamejikusanya wengine wanauza bahari ya zanzibar wengine wanaiba mafuta, wengine wanaleta mchele wa mapembe hizo ndizo kazi za za viongozi wa smz. HAKIKA ALIYEIUA TVZ, NA ALIYEUZA 200KM ZA BAHARI YA ZNZ NDIYE WAZIRI ANAEHUSIKA NA MAFUTA ZANZIBAR.

 2. Hata bado shida nyengine zaja. Wamiliki wa mafuta na mchele wa mapembe ni viongozi wa smz na wameshawakera wabara kwa kukataa kuuza 200km za bahari na zanzibar imeshafukarishwa na wabara kupitia TRA pesa zote za znz hupelekwa bara. Wabara hawatoi pesa za kununulia mafuta znz mpaka wauziwe 200km za bahari ya zanzibar. ZANZIBAR BILA YA MUUNGANO NA MAKAFIRI WA BARA INAWEZEKANA.

 3. HATIMAE BAADA YA U.S KUTOA MSAADA WA VYANDARUA ZANZIBAR MASHE HA WA SHEHIA ZANZIBAR WABAGUA BAADHI YA NYUMBA ZA CUF KUWAPATIA MSAADA WA VYANDARUA ZANZIBAR. Ikiwa kama vyandarua hivi vinatolewa kisiasa MALARIA hayatokwisha milele zanzibar. Nina ushahidi wa kushuhudia kwa macho yangu sheha akiichupa / kutokuandikisha kupewa chandarua katika nyumba za CUF zanzibar.

 4. HATIMAE BAADA YA U.S KUTOA MSAADA WA VYANDARUA ZANZIBAR MASHE HA WA SHEHIA ZANZIBAR WABAGUA BAADHI YA NYUMBA ZA CUF KUWAPATIA MSAADA WA VYANDARUA ZANZIBAR. Ikiwa kama vyandarua hivi vinatolewa kisiasa MALARIA hayatokwisha milele zanzibar. Nina ushahidi wa kushuhudia kwa macho yangu sheha akiichupa / kutokuandikisha kuwapa chandarua katika nyumba za CUF zanzibar.

  • Muongo, tena muongo. Bado unakasumba za kugombanisha watu kwa fitina zisio na ukweli.
   Tafadhali toa takwimu . Acha uchochezi usio na tija

   • Ewe kijana mpaka usiku huu kuna nyumba za CUF 4 Katika jimbo la JANG’OMBE hawajaandikishwa katika ugawaji wa vyandarua vya msaada wa U.S ukizingatia majirani wao ambao ni CCM wote wamekwisha andikishwa kupatiwa vyandarua. Jee unahitaji namba za nyumba hizo? Hivi wewe yaelekea humjui sheha wa JANG’OMBE?

 5. Bi Salma Said, ahsante kwa kukutaarifu hili ila mimi natatizika hapa!, kwanini Zanzibar mafuta yetu yasije moja kwa moja?

 6. Hatutaweza kufika Iwapo waliopewa dhamna ya kututumikia hawajaonyesha zamira ya kweli. Wao nadhani wapo kisiasa zaid. Ni hali yakusikitisha kuzorota kwa huduma za kijamii hususan wakati huu Wanzibari kwa uwezo wa Mungu tumeungana na tunaongozwa na GNU. Binafsi nilifajika sana kuona tumeingia katika zama mpya za maridhiano, kuvumiliana na tumekua huuru kutoka kifungo cha historia za kisiasa.

  Kuna baadhi ya weheshimiwa wamekaririwa katika vyombo vya habari wakituvunja moyo kwa makusudi katika kupigania haki yetu na kulinda umoja wetu.
  nimewahi kumnukuu Mh Waziri mmoja tena muandamizi, akisema wazanzibari hawana sifa za kidiplomasia au kuwa mabalozi. Waziri huyohuyo tukiwa katika janga la kitaifa (msiba wa MV Spice ) amekaririwa akisema serikali bado haijamjua mmiliki wa boti hiyo wala kampuni.Kama hiyo Haitoshi Pia meshawahi kunukuliwa akijibu hoja kifumbo kuhusu kupokezana urais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, alisema si utaratibu mzuri na unaweza ukaleta Rais asie na Sifa

  aleo hii tumeskika waziri mwengine anaesema kimakusudi kua wamechukua uamuzi na utaratibu utafuata baadae kuhusu suala lamafuta (reajea kusoma comment yangu hapo juu). Haya na mengine mengi yatawezaje kutufikisha tulipo tumainia baada ya kuundwa GNU?

  KATU HATUWEZI KUFIKA. Ukubwa wa kichwa siwingi wa akili. niheri tungekuwa na team ndogo ambayo ingeteuliwa kupitia Experience yamtu na uwajibikaje wake kuliko kua nagroup kubwa inooenkana wazi utendaji wake (upo kisiasa na kirafi).

  Kila Dhama na wamu ina mabaya na mazuri yake. Mimi bado sitowacha kuyakumbuka mazuri ya japo madogo ya awamu ya tano chini ya Dk. Salimini. Hatukufika hapa tulipo kiuchumi.Siataki Kuyaelezea ila kifupi mzunguko wa kibiashara ulikua ukionekana . Vyakula vinoagiza kutoka nje vilikua rahis na vilikua standa (sio mchele wa mapembe) Petroli haikuadimika wala kupanda bei kiholelela. kulikua kuna compani ya uhakika iliopewa dhamana ya kuhakikisha mafuta yapo muda wote naudhibiti wabei yake. Kampuni hii imekuja fisidiwa mwanzoni tu wa awamu ya sita na madhara yake tunayaona hivi sasa. Mwenye macho hafundishwi cha kuona.

  Yaleti awamu ya sita ingeliyaendeleza hayo machache ya awamu yatano tungefika wapi?

  • HIVI NI NANI ASIYEJUA ZANZIBAR KUWA MOH’D ABOUD ANATUMIWA NA TANGANYIKA KUIUA ZANZIBAR. Jambo hili ndilo lililomkasirisha SHAMHUNA mpaka akachukua uamuzi wa Kuuza 200km za bahari ya zanzibar kwa watanganyika ili apate pesa kama MOH’D ABOUD. WAZANZIBAR HATUTAKI MUUNGANO NA MAKAFIRI WA TANGANYIKA.

 7. Zanzibar bila ya muungano na WASHENZI WA BARA inawezekana. HIVI NI NANI ASIYEJUA ZANZIBAR KUWA MOH’D ABOUD ANATUMIWA NA TANGANYIKA KUIUA ZANZIBAR. Jambo hili ndilo lililomkasirisha SHAMHUNA mpaka akachukua uamuzi wa Kuuza 200km za bahari ya zanzibar kwa watanganyika ili apate pesa kama MOH’D ABOUD. WAZANZIBAR HATUTAKI MUUNGANO NA MAKAFIRI WA TANGANYIKA.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s