Siasa sio mradi wa biashara- Maalim Seif

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akikata utepe kuashiria uzinduzi wa mradi wa (MKUAJI) katika shehia ya Mtoni Kidatu, Wilaya ya Magharibi Unguja. Kushoto kwake ni Mwakilishi wa Jimbo hilo Nassor Ahmed Mazrui

MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad amesema siasa sio uwanja wa biashara bali ni fursa ya kuwatumikia wananchi, hasa katika majimbo ya uchaguzi. Alisema kwa kuzingatia kuwa kuingia katika siasa ni fursa ya kuwatumikia wananchi, viongozi wa kuchaguliwa lazima wajenge utaratibu wa kushikikiana kwa karibu katika kufanyakazi za kuwakomboa wananchi kutoka katika umasikini.

Maalim Seif alikuwa anazungumza katika sherehe za uzinduzi wa Mradi wa Kuendeleza Ujasiriamali na Ajira (MKUAJI) unaodhaminiwa na Mwakilishi wa Jimbo la Mtoni, Nassor Ahmed Mazrui nje kidogo kutoka mjini hapa jana.

Alisema Madiwani, Wawakilishi na Wabunge wakiendelea kufanyakazi kwa mtindo wa “kila mtu na wake” na kugeuza siasa kuwa mradi wa biashara wa kuwaneemesha, juhudi ya kuwaletea maendeleo wananchi itakwama. “Wanasiasa wote, Zanzibar tumeomba kazi kuwatumikia watu, sio matumbo yetu,” alisisitiza Maalim Seif.

Maalim Seif alisisitiza kuwa anasikitika sana anapoona Mwakilishi au Mbunge visiwani Zanzibar na Tanzania bara kwa jumla anatumia muda mwingi kwa shughuli za biashara zake na kuwasahau watu.

Alisema Madiwani, Wawakilishi na Wabunge wote wameomba fursa hiyo kwa ahadi nyingi, lakini baadhi yao wakishaingia ndani ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar na Bunge wanawatelekeza watu katika majimbo yao.

Alimpongeza Mwakilishi Mazrui kwautekelezaji wa ahadi kwa kuchimba visima 11 chini ya mpango aliojiwekea wa kuwaondolea wakazi wa Jimbno la Mtoni tatizo la ukosefu wa huduma ya maji.

Pamoja na kupunguza tatizo la huduma hiyo, Kwa kushirikiana na Kituo cha Mafunzo ya Ujasiriamali Tanzania, kanda ya Zanzibar Mwakilishi huyo pia amejenga kituo cha biashara chini ya MKUAJI na kuwahamasisha wananchi kuunda vikundi 36 vya ujasiriamali huko Mtoni.

Kituo hicho ambacho bado kinaendelea kujengwa, tayari ujenzi umegharimu shilingi milioni 32, na kwa mujibu Mazrui pamoja na mambo mengine kituo hicho kitatoa mafunzo juu ya uendeshaji miradi ya maendeleo, hasa inayolenga kuondoa tatizo la ajira kwa vijana.

 

Advertisements

3 responses to “Siasa sio mradi wa biashara- Maalim Seif

  1. Tunataka uongozi wa namna kama hii,kwa kutumia utaratibu kama huu tunaweza kupunguza dhiki ya maisha.
    Wanao’omba uongozi lazima waangaliwe uwezo wao,tabia na kiwango cha Elimu.Tusiwe tunachaguwa watu kwa jazba za kichama pekee.
    Huika UHuru wetu,huika dola ya Zanzibar.

  2. Umuhimu wa kuwachagua maraisi wabunge. Wakili, nikutatua matatizo yt sisi wananchi sio kufanya vile wanavyo taka wao wananchi sasaivi wanalalamika kilakitu kinapanda bei tunateseka sana wananch tuangalieni tutakufa kama sisimizi walio mwagiwa sumu

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s