Wazanzibari toeni michango yenu

Uongozi wa zanzibaryetu kwa kushirikiana na uongozi wa mzalendo.net inawaomba wazanzibari wote ambao watakuwa tayari kutoa misaada yao ajili ya kutoa elimu ya uraia kuhusu mchakato wa katiba tunawakaribisha kutoa michango yao ili kuliwezesha baraza hilo kufikia wazanzibari wote, waliopo Unguja na Pemba, Mijini na Mashamba, michango hiyo ni kwa ajili ya kusaidia gharama mbali mbali za kuwafikia wananchi kama usafiri, vitabu vya elimu juu ya katiba, matangazo kwa vyombo vya habari. nk. Misaada hiyo kwa waliopo nje ya nchi wafikishe misaada yao kwa Jumuiya ya Wazanzibari inayoshughulikia Ustawi wa Jamii UK (ZAWA),  na waliopo ndani wafikishe misaada hiyo kwetu ofisi zetu zipo Kikwajuni Welesi.Wasiliana nasi kwa njia ya parua pepe au email yetu hii ni wahamaza@gmail.com na admin@mzalendo.net  na namba zetu za simu ni +255777477101 na +255777430022 na +447588550153 na kwa wale wanaotaka kutoa michango yao kwa paypal wanaweza kutumia paypal ya mzalendo tunatanguliza shukrani kwenu nyote. Ukitoa msaada wako ujue umewasaidia wazanzibari wenzako katika kuleta mabadiliko katika nchi yako. Tafadhali tutumie maoni na ushauri wako na kama hujafahamu unaweza kuuliza suali ukiwa unahitaji ufafanuzi tupo tayari kwa hilo na karibuni nyote tunawakaribisha.

Advertisements

11 responses to “Wazanzibari toeni michango yenu

 1. Maoni yangu ni kwamba wapeni wazanzibar katiba ya zamani kwa hawatokuwa na chakutolea maoni wakat icho cha kutolea maoni hawakijui.

 2. Assalaam aleykum.
  Mie niko tayari kusaidia malazi ya wajumbe watakao kwenda Mkoa wa Kaskazini Pemba. Ahadi hii nilitoa wakati wa elimu ya Kura ya Maoni. Inaendelea lakini ni muhimu kupanga pamoja wajumbe wanapotaka kwenda huko. Simu yangu ni 0777863310 na ya mshughulikiaji wa Hill View Inn hapo wete Bw. Msanif nambari 0776338366.
  Kila la kheri.
  Dr. Omar Juma Khatib.

 3. Asalamu Alaykum, nianze na Sheikh Omar Juma Khatib kwanza ahsante sana kwa msaada huo na nakumbuka sana kwamba ulitoa ahadi hiyo wakati ule tunashukuru sana kwa juhudi zako, msaada huo kwetu sisi utatusaidia kwani tunachokitaka ni kuwafikia wazanzibari wote na hivyo basi nitachukua nambazi za simu kwa ajili ya kuwasiliana inshallah, Sheikh Abousalah ahsante kwa pongezi lakini ndio wajibu wetu huo, Sheikh Ali Mbarouk wazanzibari unaowasema wewe kuwa hawajui ndio hao tunaotaka sisi kuwafikia ili tuwape hiyo elimu ya uraia juu yav masuala ya katiba na kwa ninavyofahamu ni kwamba mtu unapompa elimu akafahamu ataweza kupambanua kipi kizuri na kipi kibaya kwa kukaa na kulaumu tu au kubeza kazi inayofanywa hatuwezi kufika pahala ndugu yangu, kwani wazanzibari tumepoteza muda mwingi kwa kulaumiana na kuongea yasio na maana jambo ambalo hivi sasa tunataka kuachana na hayo na kwenda moja kwa moja katika masuala muhimu ya kurejesha hadhi ya nchi yetu kwa hivyo basi wapo wazanzibari ambao wana ufahamu mzuri juu ya masuala haya na tunaona tunapokwenda katika kutoa elimu jinsi wanavyouliza masuali unafahamu kabisa kwamba wapo wenye ujuzi mzuri lakini pia wapo ambao hawana elimu kabisa na ndio hao tunaotaka tuwafikie na tunahitaji misaada ili tuwafikie, na nimalize na Sheikh Said misaada tunatotaka sisi ni ya aina zote ukijitolea kuwalisha watu pia ni msaada kwa hivyo tunapokea misaada ya aina hiyo pia kwa wale ambao watakwenda nje ya mji au kufika huko Pemba. Nawashukuru sana kwa maoni na masuala yenu na inshallah kwa umoja wetu tutafika tutakapo. zanzibaryetu

 4. Assalaam Alaaykum, Waungwana

  UMOJA, UZALENDO, UHURU, UADILIFU

  Ni juhudi nzuri. Katika kulizingatia suala hili, nnaomba nifahamishwe haya:
  1. Kauli ya Mhishimiwa Pinda kuwa “Zanzibar si Nchi”,
  tunaitambuwa vipi?
  2. Vipi msimamo wa Katiba ya JMT juu ya Katiba ya Zanzibar?
  3. Tunayazingatia vipi maelezo ya Mhishimiwa Pinda kwenye Bunge la Tanzania wakati akieleza juu ya “marekebisho ya kumi ya Katiba ya Zanzibar ya 1984”?

  Naomba nifahamishwe haya machache.

  Wa Billahi Tawfiiq
  Farouk

  3.

 5. Asalaam alaykum! tumefurahi sana kwa juhudi zenu hizo inshaallah kwa sisi wengine wanyonge hatuna cha kuwasaidia isipokuwa duaa inshaallah kwa juhudi zenu hizo Allah atuwafikishe kufikia malengo yetu na iwe ndio moja kati ya sababu za nyinyi kuingia peponi inshaallaah Ameen.

 6. Assalam aleikum,

  Sheikh Farouk hapa pana mada moja tu nayo kunahitajika msaada na wewe umekuwa unakuja na mada isiyohusika kwa hiyo huko ndio kupotezeana wakati.

 7. Ewe mzanzibar elewa maadui wakubwa wa zanzibar ni watanganyika. WAZANZIBAR HATUTAKI MUUNGANO NA MAKAFIRI WA TANGANYIKA. zanzibar bila ya muungano na tanganyika inawezekana.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s