Utafiti: Nusu ya wanaume nchini wagumba

Wanaume wengi wanaamini tatizo la kukosa watoto ni la wanawake pekee lakini kwa utafiti huu utasaidia wengi kufahamu suala hilo

Florence Majani

UTAFITI mpya umebaini kuwa nusu ya wanaume nchini ni wagumba ukipingana madai ya wengi kuwa tatizo hilo linawaathiri zaidi wanawake.Kwa mujibu wa utafiti huo, uliofanywa na Chuo Kikuu cha Tiba Muhimbili kati ya mwaka 2009 na Septemba 2010 unaonyesha, asilimia 47.05 ya wanaume wanaokwenda kupima afya zao za uzazi, hawana uwezo wa kutungisha mimba.Malengo ya utafiti huo uliosimamiwa na Dk Henry Mwakyoma, yalikuwa ni kubaini ni kwa kiasi gani wanaume huweza kuathiriwa katika via vyao vya uzazi na hatimaye kushindwa kutungisha mimba.

Utafiti huo  ulionyesha kati ya wanaume 221 waliopimwa, asilimia 30.03 walikuwa na mbegu dhaifu na asilimia 17.02 walikuwa hawana kabisa mbegu zenye uwezo wa kutungisha mimba, zaidi ya maji tu.Akizungumza katika mahojiano maalumu na Mwananchi, Dk Mwakyoma alisema, ugumba kwa wanaume limekuwa tatizo sugu katika miaka ya hivi karibuni.

“Nasisitiza kuwa, pengine mwanaume aliwahi kupata watoto hapo awali, lakini sasa hivi hapati, bado atakuwa mgumba,” alisema Dk Mwakyoma.Alisema hapo awali ilikuwa vigumu kupata idadi kamili ya wanaume wenye ugumba kwa sababu walikuwa hawajitokezi kupima.“Angalau sasa hivi wanakuja  na tunawapima, ingawa ni kazi ngumu kuwapa majibu yao,” alisema Mwakyoma.

Sababu za ugumba Mwakyoma alitaja sababu za ugumba kwa wanaume kuwa ni uambukizo katika tezi inayozalisha manii.Alitaja sababu nyingine kuwa ni kemikali zinazoingia katika mili yetu, mionzi na wakati mwingine ajali inapoathiri tezi hiyo

Dk Mwakyoma aliongeza kuwa, wanaoathirika zaidi ni wanaofanya kazi migodini, jeshini au wanaozungukwa na kemikali kwa muda mrefu.“Sababu nyingine ni joto kuzidi katika sehemu za siri za mwanaume, kubeba laptop, unene kupita kiasi na mazingira,” alisema.

Dk Mwakyoma akifafanua  jinsi kitengo chake kinavyopima manii  ili kujua kama zina matatizo au zipo salama, alisema, ” rangi ya mbegu pamoja na umbile huangaliwa ili kutambua ubora wake. Hata kwa kuziangalia tu, mbegu zenye rangi aidha kijivu au nyeupe si salama.”

Kwa upande wake, Dk Innocent Mosha, ambaye ni daktari wa uchunguzi wa magonjwa katika Hospitali ya Muhimbili alisema, wamefanikiwa kupata takwimu hizo kutokana na wanandoa wengi kufika hospitalini hapo kwa ajili ya kujua sababu ya kutokuwa na watoto katika ndoa yao.”Mara nyingi matokeo huonyesha tatizo liko kwa mwanaume. Lakini kuna tabu ya kuwaeleza ukweli, wengi hawataki kukubali,” alisema Dk Mosha.

Aliongeza, “Kesi kama hizo huleta migogoro ya kifamilia, kwani huenda mwanamke huyo amekwishamzalia mumewe watoto ambao kimantiki si wa kwake,” alisema Dk Mosha.

Dk Mosha alisema, kuna ugumba wa aina mbili; wa kuzawa nao na ugumba unaopatikana ukubwani.
“Wapo wanaozaliwa na ugumba, yaani mbegu  zao aidha ni dhaifu au hawana kabisa mbegu tangu kuzaliwa kwao,” alisema Dk Mosha

Shirika la Afya duniani (WHO) linathibitisha kuwa, ujazo wa manii anaopaswa kuwa nao mwanaume ili aweze kutungisha mimba ni  milligram moja na nusu hadi nne na nusu na kuongeza, “Ujazo wa manii  ukipungua au ukizidi  basi mbegu hizo zina matatizo” alisema Dk Mwakyoma.

Naye Dk Joshua Noreh wa kituo cha upandikizaji cha jijini Nairobi (IVF centre) alisema, tatizo la ugumba alianza kuliona tangu mwaka 2006 baada ya kupokea wanandoa wengi kutoka Afrika Mashariki ikiwemo Tanzania waliofika kutafuta huduma ya upandikizaji wa mbegu ili kupata watoto

Utafiti uliofanywa na WHO mwaka 2009 duniani, ulibainisha kuwa, mwanaume mmoja kati ya saba wanaofika kupima afya ya uzazi hugundulika na matatizo ya ugumba.

Chanzo: MWANANCHI

Advertisements

4 responses to “Utafiti: Nusu ya wanaume nchini wagumba

  1. JUU YA YOTE HAYA SPAMATOZOIDI KWA MWANAMME HUFANYIKA KILA BAADA YA MIEZI MITATU KWA HIYOO SIO TATIZO SANA KWA MWANAMME KWA HIYO NI MATATIZO MARA NYINGI HUWA NA DAWA

  2. Mimi kwa mtazamo wangu sikubaliani na maelezo ya Shamhuna kua SMZ ilikua haijui suala hili. Shamhuna anajaribu kuficha ukweli. SMZ inajua A to Z juu ya suala zima hili na ndo maana mpaka leo iko kimya juu ya suala la kumuwajibisha Shamhuna. Vipi waziri mmoja tu ajifungie ofisini na ajiamulie suala zito kama hili peke yake halafu Serikali iliyomteua ikae kimya tu. Haiwezekani ispokua lazima iko namna. Serikali inajua the whole plan na ilishiriki kikamilifu vyenginevyo ingemchukulia hatua kikamilifu Shamhuna na pia ingekua imeshapeleka malalamiko rasmi UN kupinga hili. Ukimya wa Serikali unaonyesha kukubaliana na yote aliyoyafanya Shamhuna.
    Kama hivyo ndivyo, nadhani sasa Waheshimiwa Wawakilishi wetu ambao kwa sasa ndio tegemeo pekee lililobakia kwa Wazanzibari, wakati umefika, kama mlivyoondoa tofauti za kiitikadi katika hili, muendeleze mapambano dhidi ya wale wote wanaoihujumu na wasioitakia mema Zanzibar na watu wake kwa kukitumia kifungu cha 37 na 41 kwani inaonekana wazi kua Shamhuna anapata support kubwa sana katika hili kutoka juu.

    SHARIFF, ISS-HAQ

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s