Mkutano wa elimu ya uraia juu ya katiba

Bi Maryam Aboud mkaazi wa Shangani Mjini Zanzibar akichangia katika mkutano wa elimu ya uraia juu ya katiba uliofanyika Lebanon Brothers hapo Shangani Mji Mkongwe

Bi Maryam Aboud akichangia katika mkutano wa elimu ya uraia kuhusu katiba katika mkutano ambao uliandaliwa na baraza la katiba la Zanzibar Bi Maryam alisema ni lazima kwanza watu wajipange vyema na nani na nani wajulikane kuwa watasimama kutuwakilisha wazanzibari lakini suala la elimu mjini mashamba Unguja na Pemba ni muhimu sana kwa kila raia wa nchi hii, lakini pia na alisema tuwe tayari wazanzibari maana nyinyi hampo tayari mnasema tu kwani tunapita humu mitaani na tukiwasikia wengine wakisema hayo ni ya watu fulani na sio yetu kwa hivyo kwanza tabia hiyo iondolewe ndipo tutakapofaulu.

Akichangia katika mkutano huo Khaleed Suleiman Said yeye alisema kwamba hakuna kisichowezekana na tukiamua wazanzibari tunaweza, tuanze kwanza na mkataba na sio katiba sasa kama hatuna mkataba tutakuwa vipi na katiba? tuwe na mamlaka kwanza ya zanzibar tuwe na jamhuri ya watu wa zanzibar kwanza, Khaleed anasema yeye hapingi mkataba lakini mkataba huo utasimama wapi bila ya nchi, pili vigezo vinavyohalalisha nchi kuwa nchi moja wapo ni serikali, lakini zanzibar licha ya kuwa serikali ipo lakini ukweli mamlaka yote yapo tanzania bara, jambo la msingi tunachotaka ni kuitishwa kura ya maoni tuulizwe tunataka muungano au hatuutaki, wenzetu wanaonesha dhahiri kuwa hawana nia njema na zanzibar, kwa hivyo sisi tuna haki kikatiba kutishiwa kura ya maoni kwa kuwa sheria zetu zinaturuhusu kuitisha kura ya maoni na mbona tuliweza wakati wa kutaka serikali ya umoja wa kitaifa vipi leo tushindwe katika hilo? Alihoji Khaleed

Aidha Khaleed alisema sisi ni washirika na bila ya zanzibar hakuna muungano lakini pia jambo jengine hapa hakuna muungano maana muungano ni ridhaa ya pande mbili lakini walikaa watu wawili tu Mwalimu Nyerere na Mzee Abeid Karume na sio sisi kwa hivyo tunahitaji sisi tuulizwe wazanzibari tunataka au hatutaki, mimi na nasema tunaweza kwa sababu kura ya maoni tuliulizwa kama tunataka serikali ya umoja wa kitaifa na tukasema tunataka japo kuwa wenzetu kule bara hawakuipenda lakini iliundwa na jee imeundwa au haikuundwa? alihoji tena kwa mara ya pili Khaleed

Kwa upande wake Salum (‎Sujae Sijauma Mkiji) yeye amesimama kuchangia akisema kwamba kwanza ije Jamhuri ya Watu wa Zanzibar yenye mamlaka ya ndani na nje ya nchi, akisema tena sisi kama wazanzibari kamwe hatuna haja ya kuwasemea wenzetu wa tanganyika bali watajisemea wenyewe hao.

Lakini Mkiji akaonesha wasiwasi wake katika suala la kuundwa kwa katiba mpya akitoa mfano wa nchini Kenya ambapo walipounda katiba mpya wakaja na jambo jimpya akisema kwamba katiba ya Mombasa imekufa kwa hivyo Mkiji wasiwasiwake ni kuwa isije katiba ya Zanzibar ikaambiwa imekufa. no hapatakalika kabisaaaa maana hilo ndilo tunaloliogopa.

Juma Kombo, alisema ikiwa tutaamua kujitoa katika muungano basi tujitoe mimi nipo katika kujitolea muhanga kwa ajili ya kuikomboa zanzibar, sisi ni vijana tumo katika harakati hizi na tunaendelea kujitolea na tayari tumeshawaambia wawakilishi wetu kwamba tunataka kuitoa zanzibar katika makunya ya watanganyika, na kama tunataka kujitoa basi ni kujitoa kwanza kwa hawa watanganyika, ikiwa tunakubali kudanganywa hatutapata fursa hii tena …tupiganie haki zetu twendeni tunakuombeni barza la katiba mtukutanishe na wawakilishi na wabunge wote ili tuwape msimamo wetu sisi tuna haki zote katika nchi hii na viongozi wametuuza na wao ndio watakaotutoa kwa hivyo na wakenda kinyume basi tutawaondoe wote jambo ambalo lilionekana kuwafurahisha watu wengi.

Wakati akijibu maswali na hoja mbali mbali zilizochangiwa katika mkutano huo muwezeshaji Ally Saleh alisema suala la kuondoshwa wawakilishi hilo haliwezekani kwa kuwa katiba haisemi hivyo ila kumuondosha rais ni jambo linalowezekana lakini sio muwakilishi au mmbunge, na akasisitiza haja ya watu kwenda kutoa maoni kwa kutumia busara bila ya kuonesha jazba kwani kuonesha jazba kunaweza kuhatarisha mchakato mzima wa utoaji wa maoni kuhusu katiba huku suala la sheria likiwa litazingatiwa kwani iwapo mtu atakwenda kwa jabza au kuwashawishi watu wengine waondoke au wasitoe maoni huenda akachukuliwa kama anakwenda kinyume na sheria na adhabu yake itakuwa ni kufungwa miaka saba na kutoa kulipa fidia.

Naye Professa Abdul Shareef alisema aliwasisitiza wanazanzibari kutotimia jazba katika suala katiba kwani jabza haziwezi kusaidia bali huharibu zaidi alisema wakati wa kurekebishwa katiba kwa mara ya kwanza watu walitoka na serikali ikawaunga mkono kwa jazba lakini kilichotendeka ni kuwa Mwalimu Nyerere alipoona kuwa watu wametoka na jazba na kutaka kupigana basi alitumia mamlaka yake na akalizima suala hilo.

Alisema “Mjue tunawakaribisha kutufunga midomo, lakini jambo la msingi ni kuwa na umoja wa kweli tukishajenga umoja wetu ndio tutafanikiwa lakini tujenge umoja mpaka tuwe angalau asilimia 80 na tusirihike na umoja huu tulionao bado tuongeze nguvu katika umoja wetu zaidi” alisema Professa Abdul Shareef.

Aidha Professa Shareef alisema umoja unapaswa kuungwa mkono kwa nguvu ili wazanzibari wakishakuwa kitu kimoja basi hata hao wawakilishi na wabunge wataona aibu kwenda kinyume matakwa ya wananchi walio wengi sambamba na hilo Professa alisisitiza kutokuwepo jembo lolote la tuwatenganisha wazanzibari kwa hivi sasa tofauti za kivyama na kiitikadi ziwekwe kwando ili umoja huu uliopo uzidi kuimarishwa zaidi.

Msitoe nafasi hata kidogo kwa jambo lolote ambalo litatutenganisha tujitahidi sana kufanya mambo yetu kwa umoja na kwa kujua kwamba sisi ni wamoja tusiridhike tu kwa umoja huu tulionao lakini tuimairshe zaidi ili tujue kwamba hakuna kitu ambacho kitatutengenisha na kuturejesha nyuma katika hili” alisisitiza Professa Shareef.

 Naye akichangia mada Ibrahim Said alisema kwamba kwa mujibu wa maelezo yanayotolewa kwamba machakato wa kuchangia au kutoa maoni juu ya katiba utakuwa huru lakini wapo baadhi ya wananchi wana khofu juu ya uhuru huo unaoelezwa kwa kuwa kawaida imekuwa hakuna kutoa maoni huru wakati kumeenza kuwekwa vikwazo na sheria mbali mbali za kudhibiti utoaji wa maoni hayo.

Alisema Muungano umewaumiza sana wazanzibari na unaendelea kuwaumiza zaidi ambapo alisema kuna watu wanakwenda kinyume na katiba mfano suala la ongezeko la bahari kama watu wanajulikana waliofanya suala hilo na kujiamuliwa lakini jambo la kushangaza ni kuona kuwa hawachukuliwi hatua yeyote.

Ibrahim alisema “sisi hatukubali tena Muungano, maana tunaumia, sisi ni waislamu na tunajua kuwa baba anapokufa mtoto ndio hurithi sasa kwa nini tunaambiwa tusitokea katika muungano huu wakati sisi tumerithi kwa baba yetu na yeye ndio aliyeingia katika mkataba wa kuungana?” alihoji Ibrahim.

Akitoa mfano wa Sudan ya Kusini alisema na wao waliadhibiwa katika muungano wao lakini hatimae wakaondokana na dhiki walizokuwa nazo na kuhoji iweje Zanzibar ishindwe kuondokana na dhiki ya muungano wakati wamechoshwa na muungano wao na tanganyika hauna faida nao?

Haroub Mohammed amesema mimi ni miongoni mwa watu wasioutaka huko muungano na wala siogopi kama nyumba zitataifishwa potelea mbali, kama viongozi wetu hawataki basi tuwaachie kina Dk Shein, Balozi Seif  Idd na Maalim Seif Shariff lakini sisi wananchi hatutaki maana tumedhulumiwa muda mrefu wanataka kutumaliza sasa lakini tunasema hatutaki tena muungano hatuutaki sote potelea mbali uvunjike …watu wengine wanasema ni kweli uvunjike potelea mbali.

Awali akitoa mada katika mkutano huo Ally Saleh alisema masuala ya muungano yanapaswa kushughulikiwa hivi sasa na wazanzibari wote kwani kuna mengi ambao yanahitaji kufuatiliwa ambapo alisema suala la kwenda kutoa elimu yav uraia ni muhimu katika kipindi hiki ikiwemo Unguja na Pemba mashamba na mijini kwani ndio lengo lakini katika ngazi ya wilaya lakini hatuna uwezo kwa sababu uwezo wa kwenda kila pahala hatuna lakini tutakwenda lakini muhimu twende lakini na nyie mjitahidi kukubali kutuita,

Ally alisema anafahamu kwamba kuna watu wana jazba lakini wakumbuke kwamba hakuna kitu kisichowezekana hivyo aliwataka wananchi kutokuwa na jazba sana kwani tume iliyopewa jukumu la kukusanya maoni ya katiba imepewa mamlaka ya kumfunga mtu miaka saba na faini juu kwa hivyo aliwataka watu wanapokwenda katika tume wajitahidi kudhiiti jazba zao.

Alisema iwapo kuna watu wanataka kufanya maandamano wapo huru hatuwazuwia lakini pia kama watu wanataka kutoa maoni hatukatai, tunataka tutoe elimu ya uraia sisi kama baraza la katiba jukumu letu ni kutoa elimu hii lakini hatuwezi kusema watu waingie mababarani lakini mkisema nyie ni sawa hamkatazwi lakini hatuwezi kusema sisi maana sisi tukisema ndio tutawapa fursa wale wanaotufuatilia watunyime hata hii fursa ya kutoa elimu ya uraia na sio kama tunaogopa lakini tunafanya hivyo kwa sababu tukisema hivyo tutakuja kufungiwa hata hiyo elimu ya uraia tutaikosa” alisema Ally Saleh.

aliongeza kwamba jambo la muhimu ni kuhakikisha sauti ya watu zinasikika kwanza ikijitokeza watu wengi hawataki muungano basi hili linaweza kukubaliwa na lazima tupitie mchakato wa katiba kwanza mimi naamini hili litawezekana lakini bila ya hivyo kuna ugumu wake ingawa hayo mengine yote tayawezekana ikiwa wazanzibari wataungana na kusema hatutaki” alisema Ally Saleh.

Advertisements

7 responses to “Mkutano wa elimu ya uraia juu ya katiba

 1. Mkataba wowowte ule ni lazima uwe na muda wa kuisha (UKOMO) kwa kimomo(LIMITATION) hata kama ni wa kutumia maguvu.. Mfano ni Mkataba kati ya China na UK juu ya Hongkong ambapo ulikua ni wa China kulazimishwa baada ya Vita maarufu vya Bangi (OPIUM WAR) ambapo China ilipigwa vibaya na UK na kuzaa mkataba huo ambao pamoja na hayo ulikua na muda maalumu na ulipoisha Hongkong ikarudi China.
  Pia hua na njia za kistaraarabu iwapo upande mmoja umechoka na mkataba na unataka kujitoa, unaweza kufanya hivyo kwa ridhaa yake/ya Wananchi wake.Mkataba wetu wa Muungano haijulikani hata umefungwa chini ya sheria ipi. Ya Kiislamu, Kimila au Kiingereza? kwani vitu vyote hivyo ambavyo kwenye sheria zote hizo nilozitaja hapo juu ni lazima viwepo lakini hapa vinakosekana. Picha inayojitikeza kwa mtu wa kawaida ni kama vile kuna upande mmoja unalazimishwa jambo ambalo katika sheria za mikataba halikubaliki kwani mkataba wowowte ule wa kulazimishana ni batili.
  Kupata uhalali wa mkataba huu ni lazima Wananchi waulizwe tu Wanautaka au Hawautaki full stop.Baada ya kupata jibu la masuali hayo mawili, hapo tena mambo mengine yote yatafuatia kulingana na jibu la Wananchi.

  • hili swala si la wananchi tena wanajulikana wananchi wanataka nini. Kwa njia tofauti wananchi washajieleza lakini kuna kitu kama kwamba interest za watu fulani zitapotea tena wakubwa wenye uwezo wa kulichelewesha jambo tena la kitaifa

 2. mwadishi waambie wende donge na makuduchi ili tusikie na wao wana maoni gani ikiwa watakuwa na maoni kama haya basi tumetowa juu kwa juuuu na chaani pia

 3. Kwa niaba ya zanzibaryetu nasema bila ya shaka Sheikh Abdulmajid na wachangiaji maoni katika mtandao huu kwa kweli lengo letu ni kuwafikia wananchi wote sio Donge na Makunduchi tu tumesema tutawafikia watu kila pembe kama ilivyofanyika kura ya maoni ya kutaka serikali ya umoja wa kitaifa na hili tumesema inshallah Mwwenyeenzi Mungu atatufikisha tufike Unguja Pemba, Mijini na Mashamba lakini jambo muhimu tunahitaji kuungwa mkono kwa hali na mali ili baraza la katiba liweze kuwafikia watu wengi katika maeneo mbali mbali ya Zanzibar.

 4. JINA JIPYA LA WATANGANYIKA NI “WAISRAEL” ni lazima kwa kila mzanzibar kuhubiri chuki dhidi ya WATANGANYIKA walioikalia nchi yetu kimabavu. Ewe mzanzibar elewa WATANGANYIKA hawa walileta JWTZ wenye UKIMWI katika kisiwa cha PEMBA vitendo walivyo kuwa wakivifanya ni KUWAFIRA WAPEMBA KWA NGUVU KWA KUWAEKEA MTUTU WA BUNDUKI BAADA KIPINDI CHA UCHAGUZI WA MWAKA 2000. Anafirwa mama, baba, jirani na watoto pia wakiwa wote wanashudia, wengine waliuliwa. baya zaidi ni kuwa hawa wote waliofirwa wamegundulika wana UKIMWI. Jee watanganyika wanaimani na wazanzibar kweli?

 5. Ahsante da salma, ili kupata uhuru wa znz ni lazima sisi wasomi tunaojali maslahi ya znz kuwahamasisha kupitia mitandao wazanzibar wote waelewe kuwa WATANGANYIKA (waisrael) ni maadui wakubwa wa wazanzibari.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s