Tuiache Zanzibar iende kwa amani

Samia Suluhu Hassan ni Waziri anayeshughulikia masuala ya Muungano, Mohammed Aboud na Khalid Mohammed katika mkutano wakizungumzia suala la kero za Muungano ambapo kero 13 zilijadiliwa na tayari sita kati ya hizo zimepatiwa ufumbuzi lakini suala la mafuta bado linahitaji kupata uamuzi wa ngazi za juu, licha ya vikao na kamati kadhaa kuundwa kushughulikia suala hilo lakini bado wapo wanaopendekeza kuwa suluhisho ni kuvunjwa kwa Muungano wenyewe na nchi mbili hizo za Zanzibar na Tanganyika ikiwa zinataka kuungana waanze upya au kila nchi ibaki na mamlaka yake

Innocent Nganyagwa

NASHINDWA kuelewa ni kwa nini wahusika wamekuwa wakiilazimisha Zanzibar iendelee kubakia katika Muungano uliozaa Tanzania wakati wenyewe wameonyesha kuwa hawaridhiki na jinsi Muungano huo ulivyo.

Kwa wahusika hapa namaanisha Serikali ya Muungano pamoja na Chama Cha Mapinduzi (CCM). Kwa upande mmoja, serikali ya Muungano ndio mlezi mkuu wa Muungano huu na CCM ndicho chama pekee ambacho kimeonyesha kuutaka Muungano kwa sura yake ya sasa ya serikali mbili, ambayo nayo imekuwa ni chanzo cha malalamiko kutoka Zanzibar.

Zanzibar wanazo sababu nyingi tu za kuonyesha kutoridhishwa na Muungano jinsi ulivyo ambazo wao wanaamini kuwa ni za msingi. Wahusika wanaweza wasizione sababu hizo kuwa za msingi; lakini hilo nalo halizuii Zanzibar kujiondoa katika Muungano.

Kimsingi, Zanzibar ni mbia katika Muungano huo na kwa maana hiyo ina haki ya kuamua kuendelea kuwapo ndani ya Muungano au kujitoa.

Hata kama sababu za kutaka kujitoa hazitaonekana kuwa za msingi sana kwa upande wa pili, lakini hiyo haiondoi haki yao ya kutaka kujitoa kwenye Muungano pale wanapoamini kuwa Muungano huo hauwanufaishi tena.

Inashangaza kuwa kwa miaka sasa Zanzibar imekuwa ikipaza sauti kuwa hairidhiki na jinsi Muungano unavyoendeshwa. Lakini, wahusika walichokifanya, na ambacho wamekuwa wakiendelea kusisitiza kukifanya, ni kiini macho walichokipa jina la kutatua kero za Muungano.

Kinachowafanya waonekane kuwa ni majuha ni kuwa kwa miaka kadhaa sasa wamekuwa wakiendelea na kiini macho hicho cha kutatua kero za Muungano lakini badala ya kwisha, kero zimekuwa zikiongezeka.

Ajabu ni kuwa wanaonekana kuwa hawaoni kuwa kero zinaongezeka badala ya kupungua licha ya juhudi zao za kushughulikia kero za Muungano.

Kwangu mimi, ilichokifanya Zanzibar mpaka hivi sasa ni njia za kuonyesha kistaarabu kuwa hairidhishwi na Muungano kwa sababu Wazanzibari wanaamini kuwa hauzingatii masilahi ya Zanzibar. Na walichokifanya wahusika ni kutumia nguvu kuwanyima Wazanzibari haki yao ya kujiamulia mambo yao.

Walianza kudai kwa maneno tu, wakaonekana hawana hoja, wakakataliwa. Kwa kuwa walidhamiria kuendelea kudai kile wanachoamini kuwa ni haki yao, wakaanza kufanya baadhi ya vitu kwa vitendo.

Wakabadilisha sheria kadhaa ambazo kimsingi zinakiuka kabisa makubaliano ya Muungano kama ilivyopo sasa. Walipoona upande wa pili haujashtuka, wakaamua kubadili na Katiba kabisa. Lakini, inaonekana bado wahusika hawaelewi hawa jamaa wanataka nini.

Kitakachotokea sasa, sidhani kama ni kosa la Wazanzibari kwa sababu kama ni onyo walishalitoa na wakadharauliwa.

Upo msemo kuwa paka akibanwa kwenye kona, anaweza kugeuka kuwa chui. Hilo ndilo litakalotokea kwa Zanzibar. Kwa sababu imebanwa sana katika azma yake ya kutaka Muungano ambao una masilahi kwake, sasa itageuka kuwa mbogo kweli kweli. Na dalalili zimeanza kuonekana.

Zipo chockochoko za chini kwa chini ambazo zinawahusisha watu wa kawaida tu hivi sasa. Wapo watu wenye asili ya Tanzania Bara huko Zanzibar ambao wameanza kunyanyaswa na watu wa kawaida tu wa Zanzibar.

Kwa maelezo yanayotolewa, inaonyesha kuwa hilo ni suala la uhalifu wa kawaida tu ambao hata Tanzania Bara upo, ingawa haulekezwi kwa Wazanzibari.

Lakini kwa wanaotaka kukiita kitu kwa jina lake halisi wanaelewa fika kuwa chokochoko hizi zina uhusiano ya kutoridhishwa kwa Zanzibari katika masuala ya Muungano. Wahusika hawataki kulikubali hilo lakini hiyo haibadilishi ukweli wa suala hilo.

Kwa kuwa tumeamua kuficha maradhi, tusubiri kifo kituumbue. Naamini kuwa Zanzibar haitachoka wala kuacha kudai haki zake ndani ya Muungano. Na kwa jinsi mambo yalivyo, wahusika wataendelea kukataa kutekeleza matakwa hayo.

Kwa kuwa suala hili limeshafika kwenye ngazi ya wananchi, ambao wameamka baada ya kuona kuna viongozi wao wengi tu ambao wana mawazo kama yao, tusitarajie kuwa litakwisha hivi hivi.

Nadhani wahusika wana hofu ya kuvunjika kwa Muungano. Lakini wafahamu kuwa kuvunjika huko kwa Muungano kunaweza kuwa ndio suluhisho la kujenga Muungano mwingine utakaokuwa imara kwa sababu utajengwa chini ya Maridhiano ya pande mbili zikikubaliana kuungana.

Lakini, kuna uwezekano mwingine kuwa ni kweli Zanzibar inabanwa sana kiuchumi ndani ya Muungano na hivyo kuvunjika kwa Muungano kunaweza kuisaidia ikajitanua. Itaisaidia pia Tanganyika iwapo itakuwa na jirani tajiri.

Kuendelea kulazimisha Muungano huu kutatuletea maafa hapo baadaye. Imeshajidhihirisha kuwa Wazanzibari hawataacha kudai haki zao mpaka wazipate.

Na itafika wakati Watanganyika nao watakapochoka na chokochoko hizo na wao kuamua kuanza kudai haki zao kwa hila na kwa nguvu. Sijui kama wahusika watakuwa na nguvu za kutosha kukabiliana na Watanganyika na Wazanzibari watakapoamua kudai haki zao kila mmoja kivyake.

Kuna nafasi adhimu ambayo viongozi wetu wanataka kutukosesha bila sababu za msingi. Kwa mtu anayepima upepo, atagundua kuwa watu wengi hawaridhishwi na aina ya Muungano uliopo. Na kwa hakika kabisa, miongoni mwa watu hao ni viongozi wetu wengi tu.

Tatizo ni kuwa waliopo madarakani hawataki kuingia kwenye vitabu vya historia kuwa ndio walioshiriki kuua Muungano. Wana hofu kuwa Zanzibar ikiruhusiwa kutoka basi Muungano utakuwa umekufa. Ile fursa kuwa kuondoka kwa Zanzibar ni mwanzo mzuri wa kuunda Muungano imara wala hawajaiona.

Wamejawa hofu ya kihistoria iliyopatia upofu wa masuala dhahiri kuwa kwa kulazimisha Muungano, eti tu kwa sababu ulianzishwa na waasisi wa taifa, watakuwa wanadumisha utaifa. Lakini kama wakiamua kufungua macho, watabaini kuwa wanachokifanya kinaua utaifa.

Kama nilivyoeleza awali, Zanzibar haiwezi kuendelea kuvumilia kulazimishwa kuwepo ndani ya Muungano. Itafika mahali itageuka mbogo na kulazimisha kile inachokitaka. Itakuwa vigumu sana kuzuia na kudhibiti hali ya mambo wakati huo.

Kama tunataka salama, ni heri tukaiacha Zanzibar iondoke kwenye Muungano sasa hivi kwa amani na utulivu, nasi tutabaki salama huku tukiwa na uwezekano wa kuunda Muungano mwingine wenye nguvu zaidi.

Lakini iwapo tutasubiri mpaka Zanzibar, au hata Tanganyika, ikaamua kujiondoa kwa nguvu, hatutabaki salama na wala hakutakuwa na uaminifu uliobakia wa kuwa msingi wa kuunda Muungano mwingine wenye nguvu.

CHANZO: TANZANIA DAIMA

Advertisements

16 responses to “Tuiache Zanzibar iende kwa amani

 1. Mm nahisi hili suala si lakudharau kwa hakuna marefu yasio ncha kwa wasikubaliane wakachukua maamuzi kuliku kuwaachia wananchi wakatoa maamuzi ambayo yataleta athari kubwa tena mbaya kwa nchi yetu lakini kila wakitufanyia ugumu sisi tunajipanga mifano inaonekana, ukiona mwenzako ananyolewa na wewe tia maji.

 2. Naamini ipo cku ya boko kharamu yatahamia tanzania alafu tutakuja kutaftana tukumbuke burundi rwanda congo naigeria hakukuanza vile ilikuwa km maskhara lakini mwisho wake ukawa m baya zaidi ya vile mtu alivyotarajia nafahamu tanganyika haitoiachia zanzibar mpaka itimize malengo yake lakini nawambia watanganyika wasioipenda zanzibar binadamu c ngombe iko cku atageuka na kujiuliza hv kwa nn mimi nafanyiwa hv?napelekwa wapi?…remember… I have a dream…iko cku itakuwa kweli.

 3. wanaotaka muungano tofauti na huu wa sasa ni wanasiasa,kwa sababu ulafi wa madaraka.mimi kama raia wa kawaida ningependa tuendelee na huu muungano au twende kwenye muungano wa serikali moja

 4. Kimsingi muandishi huyu anastahili sifa maana ameweza kupata nguvu ya kuzungumza hoja ya msingi ambayo mimi sijawahi kupata kusikia hata siku moja waandishi wengi kuthubutu kuiongelea kwani hua wanapata kigugumizi kuweza kuitamka.Aliyoyaeleza yote ni ukweli mtupu 100%.
  Hakuna ubaya wowote ule iwapo muungano kweli unatokana na ridhaa ya wananchi kuwauliza kila baada ya kipindi kama wanautaka uendelee au la kwani hii ndo itaonyesha kwamba kweli muungano huu ni MALI YA WANANCHI na sio kama picha inayojitokeza sasa kua ni wa SMT na viongozi peke yao.Hata viongozi kila baada ya miaka mitano hurudi kwa wananchi kutafuta ridhaa nyengine hivyo pia si vibaya ikiwa kila baada ya miaka 5 wananchi pia wakaulizwa masuala hayo kuhusu muungano. Njia rahisi ipo KURA YA MAONI ambayo katiba ya Zanzibar inaruhusu na kama wakisema wanautaka hapo tena ndo waulizwe WA NAMNA GANI.Serikali 1,2,3,4 au hata 5. Baada ya hapo ndo tuje kupanga Katiba ya huo Muungano ambao utakubaliwa na wananchi wenyewe.
  Hii ndo njia pekee ambayo itaondosha haya manung’uniko ya Upande wa Zanzibar.

 5. Awali kabisa namshukuru mwandishi kwa kuwa ameeleza ukweli mtupu. Mimi naungana nae, na kweli vijana wa Kizanzibari kama mimi, hatuutaki Muungano huu. Kiukweli, hata baadhi ya vingozi nao hawautaki lakini hawawezi kusema moja kwa moja kuwa hawautaki… Nnachoamini mimi, ni kama alivyoeleza mwandishi wa makala hapo juu..Muungano upo katika hatuwa za mwisho kumalizika, na inshaalah utamalizika kwa salama, ili kila upande ufanye mambo yake kama unavyotaka wenyewe..

  MUNGU IBARIKI ZANZIBAR…

  • Palipo na wanafiki mungu haleti baraka. Viongozi wa znz ni wanafiki ZANZIBAR INAULIWA NA MAFISADI WACHACHE TU AMBAO NI MOH’D ABOUD NA A.J.SHAMHUNA.

 6. TANGAZO: mtu yoyote atakaye niletea kichwa cha MOH’D ABOUD nitamzawadia Tsh 50000000/- hapo hapo. Pia, mtu yoyote atakayesababisha kifo cha mfanyakazi wa TRA zanzibar nitamzawadia Tsh20000000/- hapo hapo.

 7. HAKIKA BILA YA KUMWAGA DAMU ZA WABONGO NA WANAOUNGA MKONO ZANZIBAR KUWA WIZARA YA TANZANIA UHURU WA ZNZ UTACHELEWA KUPATIKANA. Enyi wazanzibar wenzangu ni lazima kujua kuwa hivi VITAMBULISHO VYA MTANZANIA vimeanzishwa kwa ajili ya kuimaliza zanzibar.

 8. HUO MWANDISHI MWENYEWE anaonyesha wazi ni msanii,kwano izo kero ameziona za wazanzibar wanawafanyia watanganyika kuwa ni kero kuliko hayo wanayotufanyia?karibuni tu nimesikia kutoka zenj fm,”malaya kutoka bongo walalamikia simba na yanga kutolewa kwenye kombe la muungano wakisema kumewasababishia biashara yao kuzorota”haya wanayotufanyia kutuenezea maradhi ktk jamii yetu ni madogo,tazama matokeo ya mitihani kidato cha 4,6,wazanzibar wanavyobanwa!ati lumumba nzima d1,ipo 1,b/mbela 1,hmmn 1,lakini watizame maskuli yao,hayo madogo,nenda kwenye mikopo watoto elf1,kutoka znz hawajapata mmikopo,=yote hayo huyo muandishi hajayaona,kayaona ya wazanzibar kuwaudhi watanganyika,tizama ramadhani wanavyojazana kuja kutuharibia mila,silka na tamaduni za dini yetu na taifa letu,hajayaona haya?HATUUUTAKI.

 9. Wazanzibari hivi sasa lakufanya nikuhakikisha kuwa tunazidisha UADUI na watu wa bara hata kama ikifikia kumwagadam za wabongo tuwe tayari lakini tuhakikishe kuwa tunapata UHURU WA ZANZIBAR.

 10. hili kwa sasa halitaki vikao wala semina ni kuturejeshea wenyewe wananchi tuamue tunataka au hatutaki kwa upande wetu wazanzibar .halafu mutizame matokeo vipi.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s