Misumari ya mwisho katika jeneza la Zanzibar

Na pale Zanzibar ilipojiunga na Jumuiya ya Nchi za Kiislamu (OIC) ili inufaike kiuchumi,mshirika wetu wa muungano alitutia munda na kuupiga msumari mwengine katika JENEZA la kuizika Zanzibar katika Jukwaa la Kimataifa. Marais Mwinyi na Salim,in wakavuliwa nguo hadharani na wakakemwe na Mwalimu Nyerere watoke kwa mlango wa nyuma kama walivyoingilia. Kwani, zanzibar haitakiwi kuwa na sauti katika jukwaa lolote la kimataifa na hata kucheza dimba katika FIFA-Shiriklisho la kabumbu Ulimwenguni.

MISUMARI YA MWISHO INAPIGWA SASA  NA TANZANIA-BARA KATIKA JENEZA LA ZANZIBAR. JE.WAZANZIBAR MPO ?

Na Laila Abdallah.

Ombi la Januari 18,2012 la Tanzania-bara (Tanganyika ) huko Umoja wa Mataifa,New York,  kutanuliwa  mipaka yake ya baharini  ni misumari ya mwisho inayopigwa  kufuatia ule wa  kwanza  katika JENEZA la Zanzibar  hapo April 26,1964. Mara tu baada ya  kuapishwa rasmi Mwalimu Nyerere  kuwa rais wa Jamhuri  ya Muungano ya Watu wa Tanganyika na Zanzibar,kanuni yake ya kwanza aliotunga (decree), ilikua kuifuta Tanganyika  kwa njia za  kiinimacho  na kuibua Tanzania ambayo ni ile ile Tanganyika  aliyoifuta lakini imeibuka na mipaka mipya ya aridhni.Ilijumuisha   visiwa vya Zanzibar na Pemba. Sasa inajiandaa kupiga misumari ya mwisho kwa kutanua zaidi mipaka yake ya baharini na kiliomo ndani yake tangu dagaa hadi papa.

Tangu 1964, misumari mingi imekuwa ikigongomelewa jeneza letu  tena hatua kwa hatua; na sisi wazanzibari  twatazama macho tu.
Kufuatia Muungano uliofanyika bila umma kuulizwa ndewe wala sikio, akiba kubwa ya fedha za Zanzibar katika Bodi ya ile iliokua Jumuiya ya AFRIKA MASHARIKI  ziliporwa na Mshirika wetu wa Muungano na kuzitia  kibindoni katika Bank yake (BOT) bila ya ridhaa  ama  ya Mzee Karume  au ya serikali yake. Shabaha ilikua  ni kuiua Zanzibar  kiuchumi ili kuidhibiti. Sehemu ya Zanzibar katika  “Currency Board ” ya Jumuiya ile  ilikua 11.2%. Huo ukawa msumari mwengine kati ya mingi katika jeneza letu. Licha ya juhudi nyingi za Viongozi wetu , walishindwa kuzuwia hilo. Kwani wenzetu hizo wanazoziita “KERO” ndio “MISUMARI” wanayoigongomelea JENEZA LETU hadi watapotuzika kabisa.

Msumari mwengine mjarabu kabisa ni kule  kuunganishwa kwa Afro-shirazi party (ASP) na TANU, 1977 kinyume na  Marehemu mzee Karume alivyowausia   wandani wake wasifanye,kwani yeye binafsi hakuridhia hilo katika utawala wake mzima wa miaka 8 .Kwa msumari huo,hatima ya kisiasa ya Zanzibar ilianza kuamliwa  Dodoma badala ya kisiwandui. Rais wetu Aboud Jumbe alipofanya nyoko huko Dodoma, 1984 , alikiona kilichomtoa kanga manyoya. Kuanzia hapo hata viongozi wetu wa Zanzibar bila ya ridhaa ya Dodoma,ni mwiko  kukalia kiti cha Urais. Wenzetu wanatuchagulia hata   marais wetu-aibu gani hii ?

Msumari mwengine katika jenzea la Zanzibar ni kuondolewa kwa wadifa wa ” Makamo-rais ” na kumfanya Rais wetu kana kwamba ni   rais wa kilabu cha mpira cha ” MIEMBENI SPORTS CLUB”. Hana nchi hata akiwsa na bendera..

Na pale Zanzibar ilipojiunga na Jumuiya ya Nchi za Kiislamu (OIC) ili inufaike kiuchumi,mshirika wetu wa muungano alitutia munda na kuupiga msumari mwengine katika JENEZA la kuizika Zanzibar katika Jukwaa la Kimataifa. Marais Mwinyi na Salim in wakavuliwa nguo hadharani na wakakemwe na Mwalimu Nyerere watoke kwa mlango wa nyuma kama walivyoingia. Kwani,  Zanzibar haitakiwi kuwa na sauti katika jukwaa lolote la kimataifa na hata kucheza dimba katika FIFA-Shiriklisho la kabumbu Ulimwenguni.

KABLA SHEREHE ZA MIAKA 50 ZA MUUNGANO 2014, MAITI  ya (ZANZIBAR) iwe tayari kuzikwa kupitia KATIBA MPYA YA TANZANIA. Zanzibar inazikwa kule kule UMOJA WA MATAIFA,NEW YORK, na sio Mwanakwerekwe ambako kaburi lake lilichimbwa  tayari 196 4   pa le kiti chake kama dola huru huko kilipotoweka kwa  kiini macho. Tanzania-bara (Tanganyika) inajua kucheza turufu  zake huko  ili kuizika Zanzibar katika  kaburi lile lile iliochmba 1964  kufuatia Muungano.
Baada ya kupora fedha zetu kutoka Jumuiya ya Afrika Mashariki iliovunjika ,sasa mshirika  wetu wa Muungano amejiwinda kupora gesi na mafuta yetu kwa  njia ya kuitanua mipaka ya bahari kama alivyotanua mipaka ya aridhi katika ile Tanganyika kubwa  kwa jina la Tanzania. Wakati maliasili zao kama gesi,Tanzanite, dhahabu, almasi ,makaa ya mawe na nyenginezo, ni  mali zao pekee yao, mafuta na gesi ya Zanzibar na Pemba  eti ni ubia.

VIONGOZI WETU WA ZANZIBAR NA SISI UMMA WA ZANZIBAR,  TUTATUMBUA MACHO MPAKA LINI ? AU
MPAKA TUZIKWE KABISA HUKU SANDA TUMESHASHO NEWA  NA TUNAIONA ?

Kuna usemi “Kila  Umma  hupata viongozi  uliostahiki kuuongoza.Ukiwa  Umma  ni ngangari, utapata viongozi ngngari kama akina  Jussa,Hamza na Mansuri -wenye kupaza sauti kuutetea Umma.La ,ukiwa  Umma ni wazembe, watapata viongozi wazembe.

Wazanzibari mpo ?
Tusigeuke  ile hadithi ya Mnyamwezi ” Ninamtajama tu” kumbe mwenzake anamharibu.Eti anatafuta ushahidi.
USHAHIDI kuwa mshirika mwenzetu wa Muungano hakuwa na nia njema tangu awali, ilidhihiriuka pale alipopiga msumari wa kwanza,April 26,1964 kwa kuifuta Tanganyika .
Ilikua tangu wakati ule Viongozi wetu  wawaambie  ndugu zetu kuwa, BILA YA TANGANYIKA, HAKUNA MUUNGANO.Mumeuvunja wenyewe. TUNAWEZA HATA KUWAAMBIA HIVYO LEO LAIT”I TUNA VIONGOZI NGANGARI- KERO ZIMETOKA WAPI IKIWA HAKUNA MUUNGANO.JAMANI “SI ULIANZA UFIZI NDIPO YAKAOTA MENO ?”

Ningelikua mimi ni  Rais wa Zanzibar,ningekwenda Studio za Raha leo na kulihutubia Taifa nikiwaamrisha wabunge wote wa Zanzibar katika Bunge la Muungano huko Dodoma, warudi Zanzibar mpaka  kwanza waziri-mkuu  Pinda, ama amewataka radhi  Wazanzibari na Rais wao au washirika wetu katika huo Muungano,wameifufua Tanganyika  walioifuta  kwa kini-macho.
Je, Wazanzibar mpo au tunasubiri kuzikwa kabisa  2014?
ILI KUZUWIA KUPIGWA MSUMARI WA MWISHO KATIKA JENEZA LETU  ,TUDAI TUJADILI KWANZA UHALALI WA MUUNGANO KABLA KATIBA MPYA.KWANI, ULIANZA UFIZI NDIPO YAKAOTA MENO !

Advertisements

21 responses to “Misumari ya mwisho katika jeneza la Zanzibar

 1. Washirika wanzetu wa Muungano wanafaa kunyongwa na kuuvunjilia mbali huo Muungano kwani zaidi ya Misumari wanayoendelea kuligongomelea jeneza la Jamhuri ya Zanzibar hauna maana wala faida yoyote kwetu bali ni kiini macho, wizi mtupu, ushenzi na ujangili tu.

  • Maoni yangu ni kwamba lazima kwanza tuwe na mambo yafuatayo.
   1. mpango mkakati wa kufikia maamuzi yanayotakiwa na wazanzibar
   2. tutumie haki yetu ya katiba ya zanzibar ya kura ya maoni kuondoa jamboi moja moja au hata kujitoa kwenye muungano.
   3. tuzingatie muda kwani muda wa mabadiliko ni sasa. baadae kazi itukuwa ngumu kutokanan na ukweli kwamba adui yetu ana tumia kila hila kuthujumu hararkati zozozta za mabadiliko.

 2. VIONGOZI WETU WA ZANZIBAR NA SISI UMMA WA ZANZIBAR, TUTATUMBUA MACHO MPAKA LINI ? Mimi nafikiri kama UMMA tumeshasema sana lakini tusitegemee hata siku moja viongozi wetu wa kisiasa kutamka wazi wazi kile tunachokitaka wazanzibari, lililobaki kwao ni kuzunguka mbuyu tu, mara serikali 3, mara katiba mpya lakini ukweli hawausemi. Kwa mtazamo wangu kama UMMA kunahaja sasa ya kuwalazimisha viongozi wetu kutamka wazi wazi kuwa Tunataka Jamhuri yetu ya Zanzibar irejeshwe na Zanzibar kwanza katiba baadaye. Hili litawezekana ikiwa na sisi Wazanzibari tutafikiria kuanzisha ” TAHRIR SQUARE” yetu Kama walivyofanya wamisri, hii ndio njia yakuwasindikiza viongozi kile tunachokitaka vinginevyo ndo hivyo tutabaki kutumbua macho mpaka tutazikwa tukiwa hai.

 3. wazanzibari muwe makini katika maneno msemayo, kudai haki yeni ni jambo la msingi linalokubalika lakini mnapo ongea juweni mnaongea na nani wapo watanganyika wanayajua hayo msemayo na wanatamani mpate haki yenu lakini mkitumia maneno machafu kwa watanganyika wote matajua mnakosea hata wanaowaunga mkono mtawapoteza.

 4. Mimi nahisi hii misumari ya mwisho kwa jeneza letu,tatizo si wazanzibari viongozi wetu ndio wahusika ama kwakuushika msumari au kupigilia nyundo kwa sababu hao tunaowaita viongozi wetu nichaguo kutoka Tanganyika na wamewekwa kulinda nakutetea maslahi ya Tanganyika, na wakotayari nchi iangamie na raia wake sawa mradi wao wananufaika kwa hio juhudi inatakiwa kwa wazanzibari wenyewe kuhakikisha tunalinda na kutetea mastahi yetu kwa nguvuzote kwa pamoja tunaweza tushirikiane tutashi Insha-allah.

 5. kama hayo yote hayatoshi iliyobaki ni kuvunjwa hata hio smz waka declare mkoa rasmi hakuna jengine lipi zaidi chembelecho alietangulia kusema tukingojea wanasisa tutangojea sanaaaaaaaaaaaaaaaaaaa

 6. Wazanzibari lazima tufahamu ikiwa viongozi wamechaguliwa na sultani basi kazi yao itakuwa kuchunga maslahi ya sultan

  sasa tunashangaa nini wakitufanyia hayo.lakujiuliza Shamhuna kaahidiwa nini na hao watanganyika? na wakishaangamiza hivi nini tena watakitoa kikoa?

  nawatakapoisha kuiiangamiza watarubuniwa nini tena? nawao watakuwa nani?

 7. Ni kweli Muharram. Mie ni mmojai wa Wabara ambao nimekuwa nikitetea sana haki za Zanzibar. Lakini sasa nakata tamaa kwa lugha ninazoziona.

  • ILI WAZANZIBAR TUFANIKIWE KUPATA UHURU WA ZANZIBAR NILAZIMA TUMWAGE DAMU ZA WABONGO WALIOPO ZNZ TUKIUA WABONGO 2OOO TU BASI VIONGOZI WAO WATAJUA KUWA WAZANZIBAR WANATAKA UHURU. uhuru wa znz hautapatikana kwa njia ya amani mpaka tumwage damu za makafiri wa bara.

 8. Jamani hii ya faa kuweka picha ya Jeneza la binadamu mwenzio halafu kaandika mambo ya pato la kidunia baada ya kutafakur siku ya Qiyama…kwani hakuna mifano mengine na sijui hii picha kama si mazishi ya Al-Marhum Nassor (shifta). Mchangani.

 9. assalaamu aleikum: Licha ya yote lakini wazanzibari hawato nyamaza kuidai haki yao. Insh’Allah halitokuwa lengo lao la kutufisidi.

  feisal

 10. TANGAZO: MTU YOYOTE ATAKAE NILETEA KICHWA CHA MOH’D ABOUD NITAMZAWADIA Tsh50000000/-hapo hapo. Pia, mtu yoyote atakayesababisha kifo cha mfanyakazi waTRA znz nitamzawadia Tsh20000000/- hapo hapo.

 11. binafsi naskuru kwa kuwa na upendo na uzalendo na nchi yetu na hiyo ndo inayotakiwa tuwe kuanzia kwa mtu m1 hadi ngazi ya taifa ila cha kusikitisha ni wananchi wa chini ndo tunajali na kuongelea madhila na manyanyaso tunayofanyiwa na walanguzi wachache wanaojita wakombozi, kwa maslahiyao binafsi ila iko siku dhambi ya dhulma itawarudia, cha msingi na cha sekondari ni kua huu ndo mda sahihi wa kubadilika na tukifika kwenye kubiga kura tusidanganyike!

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s