Tunapaswa kuunga mkono maneno ya Mheshimiwa Hamza

Hamza Hassan Juma ni Mwakilishi wa Jimbo la Kwamtipura (CCM) akichangia mada katika moja ya semina za wajumbe wa baraza la wawakilishi zilizofanyika katika ukumbi wa baraza hilo huko Mbweni Mjini Zanzibar

Katika wakati ambao ni muhimu sana kuunganisha nguvu zetu ikiwa kama wazanzibari basi ndio wakati huu kuliko wakati mwengine wowote na kwa hivyo nachukua fursa hii adhimu msimamo wa mtandao huu wa zanzibaryetu kwamba kulipongeza baraza la wawakilishi na wajumbe wake wote waliochangia hoja ya Mheshimiwa Ismail Jussa Ladhu Mwakilishi wa Jimbo la Mji Mkongwe (CUF) lakini pia kukubaliana na kuiunga mkono kauli ya Mheshimiwa Hamza Hassan Juma Mwakilishi wa Jimbo la Mwamtipura (CCM) aliyeitoa katika kikao cha baraza la wawakilishi akisema kama ni agizo maalumu kwa wazanzibari lisemalo hivi, na ninanukuu ” Mheshimiwa Hoja hii aliyeitoa Mheshimiwa Jussa isije ikachukuliwa kisiasa, isije ikachukuliwa kuwa imetolewa na Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF) lakini hoja hii ichukuliwe kuwa imetolewa na Mwakilishi wa Jimbo la Mji Mkongwe, Mheshimiwa Ismail Jussa, Mwakilishi halali wa wananchi, tunaomba hoja hii isichukuliwe kisiasa maana hoja hii ikichukuliwa kisiasa itatugawa na tutaweza kupoteza rasilimali na uwezo wa baraza la wawakilishi kuisimamia serikali” Mwisho wa kunukuu. Hayo ndio maneno yake Mwakilishi wa Mwamtipura (CCM) Mheshimiwa Hamza Hassan Juma. Mimi kama mmiliki wa mtandao huu wa zanzibaryetu na ni mzanzibari halisi ninayejivutia uzanzibari wangu na heshima ya nchi yangu adhimu Zanzibar, basi nasema kwamba kwa hakika  ni maneno ya maana sana na ni maneno ya hekima kubwa na ni maneno ya kutia moyo sana kwetu sote wazanzibari kwani kauli hiyo sio tu nzuri bali inajenga zaidi na inaonesha ukomavu kwa wazanzibari kwamba wamefika pahala hawataki tena kuchezewa wala kukoseshwa haki zao kwani ni maneno na kauli ya kuonesha umoja na mshikamano wetu katika kuitetea nchi yetu, hivyo nachukua fursa hii kuwaomba wazanzibari wote kuiunga mkono kauli hii kwa nia safi na kwa dhati kabisa lakini pia kuisambaza kwa kila mmoja wetu ili tufahamu kwamba wakati ndio huu na tukipoteza fursa hii ya umoja na mshikamano wetu na tukikubali kuwapa maadui nafasi wakatupoteza kama walivyofanya huko nyuma basi naamini hatutaweza tena tuunganisha nguvu zetu na umoja wetu tena hivyo basi fursa kama hiyo tutakuja kuitaka tuikose, shime basi tuwaunge mkono wawakilishi wetu katika kuitetea nchi yetu, sasa ni wakati wa kuungana zaidi na kuongeza nguvu bila ya kujali huyu anatoka chama gani, na hilo sio geni kwetu wazanzibari ikiwa tuliweza katika suala la kuambiwa Zanzibar sio nchi tuliungana na kusema Zanzibar ni nchi itakuwaje tushindwe katika hili?. Na ikiwa tuliweza kuungana katika suala la kupigania mafuta yetu na wazanzibari wote walisimama kidete kupitia wawakilishi wao na kusema ni haki ya Zanzibar hata kama sio kwa vitendo lakini kwa kauli lilisimamiwa kwa dhati na na kwa moyo mmoja na kila mmoja kwa nafasi yake alichukua juhudi kuhakikisha suala hilo naye ameliwakilisha basi iweje tushindwe katika hili? Imani yangu kwamba huu ndio wakati muhimu sana kwetu kusimamia na kuitetea nchi yetu bila ya kujali chochote kwani kutetea nchi yako ni moja katika wajibu wako. 


Advertisements

8 responses to “Tunapaswa kuunga mkono maneno ya Mheshimiwa Hamza

 1. Mh Hamza ni Mzanzibari kindakindaki na mwenye uchungu na Zanzibar,Hii sio mara ya kwanza kuonyesha uzalendo na ukomavu wake wa kisiasa. Nimekua nikifatilia mara nyingi vikao vya Baraza la Wawakilishi na anaonekana wazi kua linapokuja suala la maslahi ya Zanzibar anaweka pembeni itikadi za vyama na kushirikiana na wenzake kutetea maslahi ya Zanzibar.Ameonyesha hilo katika suala la mafuta na hata pale inapokuja miswada mibovu kama huu wa mafao ya wakubwa.Maslahi ya wanyonge ameyaeka mbele zaidi kuliko ya vigogo. Wazanzibari tuwaunge mkono Wawakilishi wetu wote kwa kuonyesha kua wako pamoja nasi kwa vitendo.Barza hili la 2010-2015 limeonyesha kua lina uwezo na ari ya kutetea maslahi ya Zanzibar na Wazanzibari kwa ujumla tofauti na lile la miaka ileeeee ambalo lilibatizwa jina la viberenge.Hili la 2010-2015 sio tena la kuburuzwa ni V8 engine. LONG LIVE ZANZIBAR.

 2. ni wakati muafaka kuzinduka kwa wananchi wa zanzibar kwa kuwaunga mkono waakilishi woootee wanaojali maslahi ya wazanzibar na maslahi ya wanyonge,nasema hivi kwasababu zipo tetesi kuwa iwapo muakilishi au kiongozi yeyote hasa wa (C.C.M)maslahi ya wanyonge nakuweka mbali ukiritimba wakubwa!basi akifika tawini anakaripiwa nakuwambiwa kama ataendelea kusema kweli basi atang’olewa uongozi na atatolewa kwenye chama.hivyo basi nawwaomba wananchi wenzangu wazinduke juu ya hili,ili kuwaonga mkono na kuwalinda vingozi watakaokuwa tayari kujitolea kwa maslahi ya ummah.a

 3. Historia itawakumbuka akina Jussa na Hamza kama watetezi wa kweli wa uhuru wa Zanzibar na itawahukumu wengine kwa usaliti na uroho wa madaraka kwa kuiuza zanzibar kwa thamani isiyostahili
  Allah ibariki Zanzibar

 4. Mimi ni mmoja ambaye BLW halinifurahishi kwa kuwa halifanyi kile kinachopaswa kufanywa. Mfano hoja ya Mafuta ilikuwa isiwe chini ya SMZ bali iwe chini ya Wananchi ili wasipate hasara Wananchi kama walivzopata kwenye UTAALII kwa kungolewa mazao na makazi yao na kujengwa Vihoteli Makuti ambapo wale wananchi hawamo kwenye HISA za Hoteli ijapokuwa Idara ya Utalii inafaidika.

  Nchi kama Malaysia ingetokea hili basi wale wavuvi na Wananchi wangepata HISA. BLW linaendeshwa kama Club na haliwakilishi ZNZ bali linawakilisha Wawakilishi na vyama vyao.

  Bado ninaamini Hoja ya Mheshimiwa Jussa ifanyiwe Utafiti wa Kina ili kieleweke na vile vipengele vifutwe once for all kwa kuipandisha hii hoja kwenye ngazi za Mahakama ya Katiba na Hata ICJ . Sote tunajuwa power ya Wizara ya Ardhi ZNZ ni kugawa viwannja kwa Wananchi haipatapo kuwakisha MAP ya ZNZ na maeneo za Bahari kuu ndomana wale Samaki walivuliwa Bahari kuu wakaishia wizara ya Tanzania.

  Kauli ya Hamza na Jussa itaishia kuwa Usanii ikiwa hawakutowa MAP ya ZNZ iliopitishwa na SMZ na tamko la Government Gazzette kuhusu mipaka na bahari kuu.

  Wa ZNZ mpaka lini tutawwacha kuwa na hoja zinazoishia vibarazani na kutowa Headlines kwenye magazeti. SUK imefanya uzuri na tuisaidie kuizinduwa ili tuwakilishwe ipasavyo.

  mtoa maoni haya binfasi amekataa kutajwa jina lake lakini ametaka maoni yake yawekwe na uongozi wa zanzibaryetu, shukran kwa maoni yako, uongozi wa zanzibaryetu

 5. EWE MZANZIBARI ELEWA BILA YA BENDERA YA SMZ KUBADILISHWA KWA KUONDOLEWA KILE KIBENDERA CHA MUUNGANO KINACHOASHIRIA KUWA ZANZIBAR NI WIZARA KAMA ZILIVYOWIZARA ZOTE ZA TANZANIA basi uhuru wa znz hautapatikana milele.

 6. Tafadhalini ndugu zangu, tuzisome “Articles of Union, 1964” na zile 11 zilizo engezwa muda baada ya muda na kufikia zote 22. Vilevile tuisome Katiba ya JMT. Huyu bwana aliokataaa kutajwa jina lake alioyaeleza yanafaa tuyazingatie. Tuwache huu mtindo wa tangu 1964, mtindo wa kusema bila ya hoja za msingi. Tusome Katiba ya JMT.

  Wa Billahi Tawfiiq

  Farouk

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s