Mkurugenzi wa Bandari ahamishwa

Mkurugenzi wa Bandari Kuu ya Malindi Zanzibar, Mustapha Aboud Jumbe akipeana mkono wa Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohammed Shein , Jumbe kwa sasa ameondoshwa katika wadhifa wake huo na kuhamishiwa wizara ya miundo mbinu kufuatia mapendekezo ya ripoti ya kuchunguza ajali ya meli ya Mv. Spice Islender iliyosababisha vifo vya wananchi kadhaa

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeanza kutekeleza taarifa ya ripoti ya Tume ya kuchunguza ajali ya meli ya Mv. Spice Islander  kwa kumuondowa katika wadhifa wake Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Bandari la Zanzibar Mustafa Aboud Jumbe. Jumbe katika barua yake ametakiwa kuripoti kazi katika Wizara ya Miundo Mbinu na Mawasiliano na atapangiwa kazi nyengine.

Kwa mujibu wa afisa mmoja wa wizara hiyo aliyohamishiwa alikiri kuwa Jumbe aliripoti katika wizara ya miundombinu lakini alisema hajui amepewa kazi gani kwa kuwa ndio kwanza barua yake ya kufika katika wizara hiyo amepewa na atalazimika kuhudhuria katika ofisi yao.

Ni kweli ameripoti kazi katika Wizara ya Miundo Mbinu na Mawasiliano hapa jirani na makao makuu ya shirika la bandari…..sijuwi kwa sasa atapangiwa kazi gani’ alisema Afisa mmoja wa wizara hiyo.

Uamuzi huo unatokana na amri iliyotolewa na katibu mkuu kiongozi Dk Abdulhamid Yahya Mzee ambaye wakati akiwasilisha taarifa hiyo wiki iliyopita aliyataja makundi mawili ya watendaji watakaochukuliwa hatua za kisheria na kinidhamu.

Mzee alisema wapo watendaji ambao hawakutajwa moja kwa moja na Tume hiyo akiwemo Mkurugenzi wa Shirika la Bandari ambaye atahamishwa katika sehemu yake ya kazi na kuhamishiwa sehemu nyengine.

Mkurugenzi wa Shirika la Bandari katika taarifa ya tume anatajwa kuzembea na kushindwa kutekeleza wajibu wake katika eneo lake la kazi.

Aidha taarifa ya Tume imesema Jumbe alishindwa kusimamia watendaji wake katika sehemu za kazi na kuruhusu watu kuingia bila ya utaratibu katika eneo la bandari.

Jumbe mbaye ni nahodha katika meli mbali mbali nchini, amekuwa Mkurugenzi wa Bandari ya Zanzibar kwa muda wa miaka 15 mfululizo.

Hata hivyo haijajulikana hatma ya Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Usafiri baharini Haji Vuai Ussi ambaye katika taarifa ya Tume hiyo anatakiwa kuwajibika moja kwa moja. lakini kuna taarifa ambazo hazijathibitishwa na mamlaka husika zinasema kwamba tayari Vuai ameshaachishwa kazi.

Akipokea ripoti ya tume iliyoundwa kuchunguza ajali ya kuzama kwa meli ya Mv. Spice Islander, rais wa Zanzibar Dk Ali Mohammed Sheni alisema hatua za kinidhamu na kisheria zitachukuliwa kwa watu wote waliohusika katika uzembe wa kuzama kwa meli hiyo na kusababisha vifo vya wananchi kadhaa.
Mbali ya mapendekezo ya kuwawajibisha watendaji hao walioshindwa kusimamia kazi zao lakini pia ripoti hiyo imetaka kufikishwa katika vyombo vya sheria wale wote waliohusika na uzembe pamoja na kulipwa fidia kwa waathirika wote wa ajali hiyo.

Tayati baadhi ya wamiliki na meli hiyo wameshafikishwa mahakamani na wengine wanaendelea kuchunguzwa kutokana na ajali hiyo ambayo ilisababisha vifo kadhaa na baadhi ya watu kupotea hadi leo.

Advertisements

9 responses to “Mkurugenzi wa Bandari ahamishwa

  1. Je kunauzowefu gani wa kazi ya Abuud jumbu kuhamishwa ktk shirika la bandari hadi wizara ya Miundo mbinu Jamani hii si kudhorotisha Utendaji wakazi Ktk wizara Chamsing Alikua afukuzwe kazi na sikulindana..!

  2. CHA MSINGI ZAIDI ALIKUWA ACHIE NGAZI TENA KASHATUIBIA SANA KWENYE BANDARI ILA SEREKALI YETU INAMPANGO WA KUTIZAMANA SURA HUYU MTOTO WA NANI NA YULE AMEFANYA NINI AWAMU ZIZLIZOPITA SASA HATUWEZI KUSONGA MBELE HATA SIKU MOJA UBINAFSI TUU TUANGALIENI MBELE NA TUJUWE NINI TUNACHOKIFANYA SAWA HUYU NI MMOJA NA SHAMUHUNA WAPILI KUTUUZIA ZNZ YETU

  3. MAFISADI WA TANZANIA HUJIVUA GAMBA LAKINI HUYU MTOTO WA RAIS MSTAAFU ANAHAMISHIWA MIUNDOMBINU ILI SIM ZIANZEKUWA NETWORK BUSY AJALI ZA NDEGE KUONGEZEKA NA BARA BARA MBOVU ZANZIBAR KUZIDI.

  4. HIO KWA KWELI HAIELEKEI KABISA, MAANA SERIKALI ILIKUWA IMSIMAMISHE KAZI NA IMSHITAKI NA SIO KUMHAMISHA HAPO NDIPO TUNAPOLIKOROGA, ASHITAKIWE NA IKIBIDI ANA MAKOSA AHUKUMIWE NA SIE ANAPELEKWA PAHALA PENGINE NAKO PIA AKAFANYE MANYAGO.


  5. Serikali hapa kwa kweli huyu Mkurugezi sio wa kumbadilisha sehemu ni wakuachishwa kazi moja kwa moja bado mnalindana je na huko anaweza kufanya kulikon ya hayo.

  6. mtu aliofanya uzembe na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 1000 anahamishwa wizara,, kwanini mwizi wa nazi na kuku musimhamishe mtaa baada ya kumfunga hiyo ni haki nazi na roho za watu ni sawa,, kwa kweli zanzibar inatakiwa dua na watu wamrejee mungu kumshitakia ila hali haitokuwa nzuri na hatuna lakusema mbele ya allah siku ya mwisho hatoki mtu marungu na moto tu.
    dhulma unyanyasi wa haki mnyonge siku zote ni mtu wa kusononeka lakini iko siku kila mmoja atapewa kitabu chake asome aloyatenda katika ardhi ya allah.

  7. mawazo yenu swadakta,ni kufukuzwa tu,kwanza huyu jamaa anakibri ajab bandarini watu wafika kusema watakula halua na kahawa akifuzwa kazi ,sote tunamchukia huyu jamaaaa hasbia llahu wa niima l wakili

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s