Mswada wa rushwa wawasilishwa

Baadhi ya wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wakiwa katika Ukumbi wa Mkutano wakisikiliza mswaa wa kuzuwia rushwa ualipowasilishwa barazani hapo na Waziri wa Nchi Ofisi ya rais Utumishi wa Umma na Utawala Bora Haji Omar Kheri

Waziri wa Nchi Ofisi ya rais Utumishi wa Umma na Utawala Bora Haji Omar Kheri amewasilisha mswada wa kuzuwia rushwa na uhujumi uchumi ambao lengo lake kubwa ni kudhibiti vitendo vya rushwa vinavyodhoofisha maendeleo ya uchumi na ustawi wa jamii hapa Zanzibar.

Kheri alisema Serikali imewasilisha mswada huo kutokana na kilio cha muda mrefu cha kutokuwepo kwa taasisi hiyo kufuatia kuwepo kwa malalamiko ya kukithiri kwa vitendo vya Rushwa.

Alisema mswada huo umekuja kutokana na utekelezaji wa ilani ya Chama cha Mapinduzi na sera zake ya mwaka 2010-2020 ambazo zinasisitiza kuwepo kwa chombo kitakachodhibiti rushwa na kukomesha vitendo hivyo moja kwa moja.

`Tumedhamiria kupambana na vitendo vya Rushwa ikiwemo kuwasilisha mswada huu ambao pia utapambana na vitendo vya uhujumu uchumi nchini’ alisema.

Alisema kwa muda mrefu Zanzibar haikuwa na chombo kinachoshungulikia na kudhibiti vitendo vya rushwa ambapo kazi hizo zilikuwa zikifanywa na Jeshi la Polisi jambo ambalo huzusha malalamiko makubwa kutoka kwa wananchi mbali mbali.

waziri huyo alisema hata hivyo jeshi la polisi lilikuwa likijishungulisha zaidi na masuala ya kukamata watu wanaofanya vitendo vya rushwa na sio kuzuwia rushwa pamoja na uwezo wa kisheria wa kufilisi mali za Rushwa.

Alisema kwa matumaini makubwa Serikali itafanikiwa kupambana na rushwa baada ya kupitishwa kwa mswada huo ambao umekuja baada ya kupata michango mbali mbali kutoka kwa wataalamu wa fani mbali mbali.

Kheri alisema miongoni mwa kazi zitakazofanywa na taasisi ya kupambana na kuzuwia Rushwa ni kutoa elimu kwa wananchi kuhusu madhara ya rushwa na njia za kupambana na tatizo hilo.

Advertisements

One response to “Mswada wa rushwa wawasilishwa

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s