Ombi la eneo la bahari kuu lapingwa

Wajumbe wengi wa baraza la wawakilishi visiwani Zanzibar wametaka Waziri wa Maji, Makaazi, na Nishari Zanzibar Juma Shamhuna ajiuzulu. kufuatia sakata la kushirikiana kinyemela na serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania kufanikisha ombi la kutaka nyongeza ya eneo la bahari ikijumuisha mipaka ya visiwa hivyo, pasipo kulishauri baraza hilo.Wito wa kutakiwa kujiuzulu kwa waziri huyo mkongwe visiwani Zanzibar unafuatia hoja binafsi iliyotolewa na mwakilishi wa Jimbo la Mji Mkongwe Ismail Jussa. Kufutia hali hiyo Sudi Mnette alizungumza na Issa Yusuf, Mwandishi kutoka Zanzibar kujua ni yapi yaliyojitokeza hadi wakati huu . Tafadhali bonyeza hapa. Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wamemtaka waziri wa nishati Zanzibar, Ali Juma Shamuhuna ajiuzulu, pamoja na kupitisha azimio la kuitaka Serikali ya Zanzibar kuwasilisha mara moja barua ya kupinga kitendo cha Serikali ya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwasilisha ombi la huko Umoja wa Mataifa (UN) kuongezewa eneo la kiuchumui katika bahari kuu (EEZ).

Azimio hilo limefuatia hoja binafsi iliyowasilishwa na Mwakilishi wa jimbo la Mji Mkongwe  (CUF) Ismail Jussa Ladhu kuhoji uhalali wa serikali ya muungano kuwasilisha ombi hilo UN bila kuishirikisha Zanzibar kikamilifu.

Katika kukabiliana na serikali ya muungano, Jussa akitoa mapendekezo manne ambayo wajumbe wote wapiga kura kuridhia pamoja na pendekezo la tano linaloitaka baraza la mapinduzi Zanzibar kusimamia utekelezaji wa maazimio yaliyopitishwa na baraza la wawakilishi mwezi Aprili mwaka 2009.

Mapendekezo ya Jussa ni kama ifuatayo: Kwamba seriklai ya Zanzibar iiandikie serikali ya muungano barua ya kusitisha mara moja mchakato wa maombi ya kutaka kuongezewa eneo la ukanda wa bahari kuu, na kwamba iwapo serikali ya muungano ikipuuza serikali ya Zanzibar ipeleke ujumbe UN kutaka mchakato usimamishe.

Wiki iliyopita Serikali ya Jamhuri ya Muungano kupitia Waziri wake wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makaazi Anna Tibaijuka iliwasilisha maombi katika umoja wa mataifa kuomba eneo la ziada la maili 150 nje ya eneo la sasa la maili 200 za ukanda wa kiuchumi wa eneo huru la bahari.

Katika mchakato huo serikali ya muungano ilimshirikisha waziri wa nishati wa Zanzibar,  Ali Juma Shamuhuna kama alivyokiri mwenyewe kwa wajumbe wenzake ndani ya baraza la wawakilishi wiki iliyopita. “Kama waziri ni serikali, basi Zanzibar ilishirikishwa,  na nilimpeleka msaidizi wangu kuniwakilisha, lakini kama serikali ni baraza la mapinduzi, basi haikushirikishwa katika jambo hili,” Shamuhuna alisema.

Kauli yake ilizuwa maswali mengi kwa wajumbe wenzake miongoni mwa maswali hayo yakiwa ni inakuwaje jambo zito kama hilo Shamuhuna analibeba peke yake wakati baraza lilipitisha azimio linalotaka eneo lote la bahari la EEZ pamoja na maliasili ya mafuta liondolewe katika orodha ya muungano?

Serikali ya muungano haijajibu hadi leo kuhusu azimio la baraza, lakini viongozi wa seriklai ya muungano wamekuwa wakitoa kauli kwamza matatizo yote ndani ya muungano yatashughulikiwa.

Katika kuonesha kutoridhika na Shamuhuna, ndipo baadhi ya wajumbe wakamtaka waziri huyo ajiuzulu mwenywe au rais amtimue kazi kutokana na madai ya kuidhalilisha baraza baada ya kushirikiana na Prof Tibaijuka kupeleka ombi UN.

“Inakuwaje waziri anakuja hapa bila ya kuwa na msimamo juu ya maswala nyeti kama haya…waziri Shamuhuna inabidi ajiuzulu au rais amuwajibishe. Kama hatua haitochukuliwa, tunaweza kutumia kifungu cha 41 kupiga kura ya kutokuwa na imani na serikali…,” alisema mwakilishi Hamza Hassan Juma (CCM Kwamtipura).

Wajumbe wengine ambao walitoa kauli za waziwazi dhidi ya Shamuhuna na kumtaka aachiye ngazi ni Hija Hassan Hija (CUF- Kiwani), Mbarouk Wadi Mussa (CCM- Mkwajuni), Asha Bakari Makame (CCM wanawake), Omar Ali Shehe (CUF-Chakechake), na Rashid Seif Suleiman (CUF- Ziwani).

Ali Mzee Ali (CCM kuteuliwa) alitumia lugha ya kiprofesa pia kumlaumu Shamuhuna kwamba alijitia kitanzi mwenyewe katika kuelezea ushiriki wake katika swala ambalo bazara tayari limetolewa msimamo mwaka 2009.

Juhudi la mwanasheria mkuu wa serikali Othman Masoud kujaribu kutaka kumkingia kifua hazikufua dafu, kwani aliposema kwamba ni mapema kumhukumu mtu barazani  alijibiwa kwa wajumbe kuguna, na baadae Jussa kumwambia kuwa wazanzibari ambao wamekuwa wakimheshimu sana wameanza kuvunjika moyo naye tangu alipopata wadhifa wa mwanasheria mkuu.

Hivi sasa kinachosubiriwa kwa hamu kubwa ni jibu la serikali ambalo makamo wa pili wa rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi aliahidi wiki iliyopita kuwa katika kikao cha baraza la mapinduzi swala hilo litazungumzwa na kujadiliwa ikiwa pamoja na kuangalia athari ya ombi la serikali ya muungano la kutaka nyongeza ya EEZ kwa Zanzibar.

Advertisements

4 responses to “Ombi la eneo la bahari kuu lapingwa

  1. Inabidi ifikie wakati watumishi wajue umuhimu wa dhama walizopewa kuwa wanawakilisha akina nani, kwani inasikitisha kuwa waziri wetu mpendwa aliyeaminiwa na taifa anatoa taarifa kama hiyo mbele ya baraza bila ya kuangalia maslahi ya wale anaowawakilisha.Inakuwaje waziri anashiriki jambo zito kama hil bila ya kuwashirikisha wajumbe ambao tumewapa dhamana ya kutuwakilisha anataka kuiuza nchi yake kwa urahisi kiasi hiki. Kwa nia njema nimuombe mheshimiwa waziri ili abaki na hadhi yake ambayo wazanzibari wamempa na wanaendelea kumpa ,basi afuate nyayo za akina mhe.lowasa.ninaimani kubwa kuwa atafanya hivyo.na mhe.mwanasheria si dhani kuwa hana uchungu na znz.

  2. Ni wakati sasa umefika zanzibar kupeleka ombi la kuvunja muungano wa Tanzania umoja wa mataifa kwani sisi wenyewe hapa tumeshindwa kutokana na kuwaogopa Tanganyika. Seif sharif hamad ni wakati wa kujutia makosa yake kwani yeye ndio uliyefanya mpaka Rais wa pili wa Zanzibar ajiuzulu kwa kutaka kupeleka ombi la Zanzibar kuvunja muungano. Sisi Wanzibar tunamtaka yeye na serikali yake wapeleke ombi hili la kuvunja muungano umoja wa Mataifa kwani inaonekana wazanzibar wote Pamoja na viongozi viongozi wao wameshachoka na muungano. Tunawaona Watanganyika wanataka kuimaliza zanzibar sisi bado tunasubiri nini? USHHIDI KAMILI?

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s