Mswada wa mafao ya vigogo waondoshwa

Waziri wa Nchi Afisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Mwinyihaji Makame Mwadini

 Waziri wa Nchi Afisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Mwinyihaji Makame Mwadini ametangaza kuondowa mswada wa mafao na maslahi ya  viongozi wa kisiasa wastaafu akisema unahitaji kurudishwa tena katika kamati za baraza kwa ufafanuzi wa kina.

 

Hatua hiyo ilizusha shangwe na furaha kwa wajumbe wa baraza la wawakilishi zaidi wanaotoka katika majimbo ya uchaguzi ambao wakati wa wakijadili mswada huo walipinga vikali na kusema huu si wakati muafaka wa kuleta mswada huo kwani wananchi hawatoifahamu serikali yao.

“Mheshimiwa spika kwa kutumia kifungu cha baraza 85(1) naomba kuahirisha kutoa majumuisho yangu katika mswada huu wa kujadili mafao ya viongozi wa kisiasa……mswada hauondoshwi lakini unarudishwa katika kamati za baraza kwa majadiliano zaidi” alisema Dk Mwinyihaji.

Mwinyihaji alichukuwa nafasi ya kuwashukuru wajumbe wa baraza la wawakilishi waliochangia mswada huo ikiwemo wajumbe wa baraza la wawakilishi kutoka katika majimbo ya uchaguzi kwa kuchangia na kutoa hoja zenye msingi.

Spika wa Baraza la Wawakilishi Pandu Ameir Kificho alisema mswada huo unaondoshwa kwa ajili ya kutoa nafasi zaidi kwa wajumbe katika kamati za baraza kuufanyia kazi, ambapo utaletwa tena katika kikao kijacho.


Mwakilishi wa viti maalumu wanawake Asha Bakari ambaye ni makamo mwenyekiti wa jumuiya ya wanawake nchini UWTZ alisema mswada huo ulipaswa kuondolewa katika meza ya shunguli za baraza kwa sababu hauna maslahi kwa wananchi wa Zanzibar.


“Huu mswada hauna maslahi kwa wananchi wetu na haufai kuletwa katika kipindi hichi ambacho wananchi wetu wanakabiliwa na matatizo mbali mbali” alisema Asha Bakari ambaye amewahi kuwa waziri katika awamu ya Dk Salmin Amour Juma.

 

Alisema kazi kubwa inayotakiwa kufanywa na serikali kwa sasa ni kuhakikisha inatekeleza mambo muhimu ya msingi kwa wananchi ikiwemo huduma za jamii maji safi na salama pamoja na matibabu.

 

Mwakilishi wa jimbo la Mji Mkongwe (CUF)  Hamza Hassan Juma (CCM) wote walifurahishwa na uamuzi wa Serikali kwa kuzifahamu hoja  na hisia za wajumbe wa Baraza la Wawakilishi zinazotokana na matakwa ya wapiga kura wao.

 

Nashukuru Mungu hatimaye Serikali imetufahamu nini tunasema na wananchi wake wanataka nini kwa wakati huu ambapo wananchi wanakabiliwa na hali ngumu ya maisha” walisema wawakilishi hao.

Advertisements

One response to “Mswada wa mafao ya vigogo waondoshwa

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s