SMZ yatakiwa kutoa maelezo juu ya nyongeza ya masafa ya bahari

Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Pandu Ameir Kificho akiendesha kikao cha baraza hilo kinachoendelea katika ukumbi wa Mbweni nje kidogo ya Mji wa Zanzibar

Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Pandu Ameir Kificho ameitaka Wizara ya Ardhi, Makaazi, Maji na Nishati kutoa taarifa katika baraza la mawaziri suala la Tanzania kuwasilisha ombi la nyongeza masafa ya bahari kuu kwenye Umoja wa Mataifa. Kificho alisema hivyo baada ya Waziri wa Ardhi, Makaazi, Maji na Nishati, Ali Juma Shamuhuna kusema kwamba yeye kama wizara taarifa anayo hiyo lakini katika baraza la mawaziri hakuna taarifa ya jambo hilo iliyowasilishwa.

“Nakuomba waziri mheshimiwa Ali Juma Shamuhuna kuleta taarifa hiyo baraza la mawaziri kwa ajili ya kuifanyia kazi pamoja na wajumbe wa baraza la wawakilishi” alisema Spika Kificho.

Kificho, aliwaambiwa wajumbe wa baraza hilo wasubiri na kuiagiza Serikali kulifuatilia suala hilo kikamilifu ili wananchi wa Zanzibar wajue lengo la hatua hiyo kwa serikali ya Tanzania.

Alitoa agizo kwa serikali kutoa maelezo juu ya upande mmoja wa Muungano kupeleka maombi hayo kwa Umoja wa Mataifa bila kuushirikisha upande wa pili.

Aliitaka Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kufuatilia jambo hilo kabla ya maamuzi ya Umoja wa Mataifa hayajatolewa kuhusiana na suala hilo kwani suala hilo linahusu pande mbili na wananchi wa Zanzibar wana haki ya kujua mwenendo wa mambo katika nchi yao.

Awali Mwakilishi wa jimbo la Mji Mkongwe (CUF) Ismail Jussa Ladhu alitoa taarifa mbele ya wajumbe wa baraza la wawakilishi   kwamba Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imewasilisha ombi katika umoja wa mataifa kuomba kuongezewa masafa zaidi ya maili mia mbili katika bahari kuu.

Jussa alitoa hoja ndani ya baraza la wawakilishi akiwataka wajumbe wa baraza hilo lijadili suala hilo kwa uwazi hasa kwa kuzingatia suala hilo lina athari kubwa kwa wazanzibari iwapo litafanikiwa.

Alisema hatua hiyo ya Serikali  ya Muungano ni nzito na inayogusa wananchi kwa hiyo, ilitakiwa kuangaliwa vizuri kwani waathirika wakuu huenda wakawa zaidi ni wazanzibari.

Jussa alifahamisha kuwa kwa mujibu wa taarifa iliyotoka ndani ya vyombo vya habari ombi hilo linawasilishwa jana katika ofisi za Umoja wa Mataifa huko New York, Marekani.
“Waheshimiwa wawakilishi hoja hiyo imetugusa sana wananchi wanzanzibari tunaomba muichangamkie, hatutaki mambo ya hewala bwana, hoja ya serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kusema kuwa Zanzibar imeshirikishwa kwa vile mjumbe mmoja kutoka Zanzibar anaonekana katika picha ya pamoja na mama tibaijuka katika kuwasilisha ombi hilo la umoja wa mataifa hatuitaki wala haitoshelezi” alisema Jussa katika kikao hicho cha baraza la wawakilishi kinachoendelea huko Mbweni Zanzibar.
Kwa upande wake Mwakilishi wa Kuteuliwa na Rasi, Ali Mzee Ali, alisema kuwa ingekuwa jambo la maana suala kama hilo likapigiwa kura kutokana na umuhimu wake kitaifa na sio kuamuliwa na upande mmoja.

Suala la masafa ya bahari kuu limekuwa na mgogoro kati ya Zanzibar pamoja na serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania kiasi ya baraza la wawakilishi kupitisha azimio kuhusu jambo hilo, ambalo limeingizwa katika orodha ya kero za muungano.

Akitoa ufafanuzi zaidi, Shamuhuna alisema kwamba wizara yake inayo taarifa kamili ya suala hilo ambapo alitakiwa yeye kufunga safari kwenda umoja wa mataifa kuwasilisha ombi hilo pamoja na waziri wa ardhi, nyumba na maendeleo ya makaazi wa jamhuri ya muungano Bi Anna Tibaijuka.

Hata hivyo Shamuhuna alisema kwamba kutokana na kutingwa na kazi nyingi alimtuma afisa wake kufuatana na ujumbe huo kwenda katika safari hiyo.

“Ujumbe huo kwa sasa upo katika umoja wa mataifa na tayari unatarajiwa kuwasilisha ombi hilo ambapo Tanzania baadaye itapangiwa tarehe kwenda kusikiliza shauri lao”.

Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar baadhi yao wamehoji hatua ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupeleka maombi Umoja wa Mataifa (UN) kuomba kuongezewa ukubwa wa eneo la bahari na kutaka ufafanuzi wa suala hilo kuwasilishwa ndnai ya kikao hicho, hatua ambayo kimsingi Spika Kificho alikubaliana nao wajumbe hao na kuiagiza serikali kuwaislisha suala hilo barazani hapo.

Tanzania inawasilisha ombi la kuongezwa zaidi masafa ya eneo la bahari kuu kutoka mia mbili na sasa kufikiya mia nne, kama shauri hilo litakubaliwa.

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka, anaelezwa kuwasilisha hoja hiyo na kuiwasilisha Umoja wa Mataifa (UN) huko New York Marekani.

Advertisements

10 responses to “SMZ yatakiwa kutoa maelezo juu ya nyongeza ya masafa ya bahari

  1. Kwanza napenda kumpa pongezi za thati kabisa Mh. Jussa kwa bidii zake za kuibua hoja ndani na nje ya baraza letu kuhusu mustakbali wa Zanzibar yetu.yeye akiwa ni muwakilishi wa watu waliomchagua na kumpa kura zote ni wajibu wake kufanya kazi bila kumuogopa yoyote kwakua tuliompa dhamana hiyo ni sisi wananchi kwa kumuona anatufaa kututetea na kutetea haki zetu wazanzibar,tunakuahidi tupo pamoja na wewe wananchi tuliokuchagua huna haja ya kutetereka juu ya kazi yako. Pili Wazanzibar wezangu kwa hili hakuna haja ya kulifumbia jicho hata kwa smz ni lazima watoe ufafanuzi wa kina juu ya suala hili kulikubali bila ridhaa ya wananchi wake na hususan kuwa yumo mjumbe wa smz ktk suala hilo, tunapenda muelewe dhama tuliyokupeni ni sisi wananchi kwa kura zetu kukupeni mtuongozi vipi leo muamue wenyewe kwa wenyewe na hata siku moja hatujawahi kuskia uyo Mh. Shamhuna akiileta hoja hiyo kwenye baraza la wawakilishi ili kuijadili hilo ndio kosa moja la waziri huyo anaehusika kwaiyo vipi mtatueleza kijujuu tu kuwa eti Tanzania imepeleka ombi la mipaka na pia eti limejadiliwa na pande zote 2 za muungano kivipi? Wazanzibar wezangu lazima tuamke na tuwe macho tuondoshe itikadi zetu za vyama na tuwe kitu kimoja naamini sauti moja lazima itakua na nguvu, tusikubali kuyumbishwa na huu Muungano na nguvu ya Umma ndio inayohitajika.

  2. hapa inamaana shamuhuna na jamaa zake wa donge ndio ameuza nchi kwa nini hata baraza la mawaziri halijuwi yeye akasema kuwa amepeleka mjumbee mungu hukumu unayo wewe

  3. Wazanzibar wamechemsha mara tu baada ya Kuzidiwa akili au kupokea rushwa kwa viongozi wa smz na kufanya zanzibar kuwa wizara ya TZ. Kutokana na ufanano uliopo wa bendera ya smz na bendera zote za serekali ya TANGANYIKA. Hivi naomba kuuliza jee hawa waliounda bendera ya smz hawakujua kuwa ZANZIBAR WAMESHAIUA KUTOKA KWENYE NCHI NA KUWA WIZARA YA TZ.

  4. Wazanzibar wamechemsha mara tu baada ya Kuzidiwa akili au kupokea rushwa kwa viongozi wa smz na kufanya zanzibar kuwa wizara ya TZ. Kutokana na ufanano uliopo wa bendera ya smz na bendera zote za serekali ya TANGANYIKA. Hivi naomba kuuliza jee hawa waliounda bendera ya smz hawakujua kuwa ZANZIBAR WAMESHAIUA KUTOKA KWENYE NCHI NA KUWA WIZARA YA TZ. Watanganyika hawajaamua kuchukua 150km. Wakiamua hakuna mwakilishi atakaesema kitu. Watanganyika wamejipanga muda kuteka znz.

    • bahari ni miongoni mwa hio kero inayotupelekea tutake katiba mpya kwa hivyo usitwambie tushuhulikea katiba tuache nchi yetu ikiuzwa kutakua kuna faida gani ya kushughulikia hio katiba mpya au wew ni mtanganyika?

  5. Mie naona huyu Shamuhuna aulizwe kapewa pesa kiasi gani hata akakubaliana na wabara hata waunguja wenziwe asiwambie

  6. Kwanza na penda kukupongeza mh jussa kwa hatuaa zako kwa kuibua hoja zenye nguvu ndani na nje ya baraza kwa kua hii yote unaitakia mema zanzibar yetu tunawaomba wakilishi wengine wafuate mfano wako ikiwa hata ccm au hata etc

  7. hakuna wakushkuriwa ispoku menyezi mungu kumjalia Mr Jussa kuamacho kuleta nguvu ya hoja ila me ningeomba kesi viongozi wakishida watanganyi wasipewe eneo basi Mr shamhuna afunguliwe kesi mahakamani kwanini akubali bila kuwajulisha wenzake

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s