Rais atia saini miswaada mitatu- Spika

 

Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Pandu Ameir Kificho

Spika wa baraza la wawakilishi Pandu Ameir Kificho amewaambia wajumbe wa baraza hilo kwamba tayari rais wa Zanzibar Dk Ali Mohammed Sheni ametia saini miswaada mitatu iliyopitishwa na wajumbe hao katika kipindi cha Baraza la Wawakilishi kilichopita na sasa kuwa sheria kamili. Kificho alisema miswaada mitatu iliyotiwa saini na rais ni pamoja na mswaada wa kuanzishwa kwa maabara ya mkemia mkuu wa serikali, mswaada wa kuanzishwa kwa shirika la taifa la biashara Zanzibar (ZSTC) pamoja na usanifu wa kuendesha mazao mengine na mswada wa kurekebisha baadhi ya sheria na kuweka kanuni za baraza.

‘Wajumbe wa baraza la wawakilishi nafurahi kuwajulisha kwamba miswaada mitatu iliyopitishwa na baraza hili tayari imekuwa sheria baada ya kutiwa saini na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi’ alisema Spika.

Aidha Spika aliwajulisha Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kuhusu mabadiliko yaliyofanywa na rais wa Zanzibar Dk Sheni ya kumuondowa katika nafasi ya katibu wa baraza, Ibrahim Mzee Ibrahim.

Kificho alisema kwamba Ibrahim ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa mashtaka wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na kusema huo ni wadhifa mkubwa hata kuliko nafasi yake ya awali.

‘Nataka wajumbe wa baraza la wawakilishi kukujulisheni mabadiliko hayo ambapo sasa mwenzetu Katibu wa Baraza Ibrahim hayupo tena na sisi baada ye kuteuliwa kushika wadhifa wa Mkurugenzi wa Mashtaka Zanzibar (DPP)’ alisema Kificho.

Kificho aliwafahamisha wajumbe wa baraza la wawakilishi na kusema kwamba wadhifa huo ni mkubwa wenye hadhi ya kimataifa ikiwa ni sawa na Jaji wa Mahakama Kuu.

Advertisements

3 responses to “Rais atia saini miswaada mitatu- Spika

  1. Kila la heri kwa uteuzi mkubwa kuliko Ukatibu wa Baraza. Tumuombee utekelezaji madhubuti katika majukumu yake na asiche ukweli kwa kuhofia kutengwa na baadhi ya wanajamii.Aendelee kusema na Kuutetea ukweli kila inapo bidi;Amiin

  2. Hakika office ya MKEMIA MKUU haina maana zanzibar kwani hivi sasa ipo lakini MCHELE WA MAPEMBE PIA NAO UPO ZANZIBAR. Jee ofisi hii ni ya wahindi tu au WAZANZIBAR.

  3. Sasa nimekubali smz kuna ccm na CUF ambao wanajali maslahi ya znz. He! Mpaka KIFICHO kusema ama kweli mwenye kubagua wapemba na wakaskazini UNGUJA yuko bara (shamsi vuai nahoza) kipindi cha uwaziri wa shamsi vuai znz waliajiriwa MAKUNDUCHI TU. Mungu amuue huko huko bara kabla hajarudi znz.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s