Mswaada wa maslahi ya vigogo wapingwa tena

 

Mwakilishi wa Jimbo la Mji Mkongwe (CUF) Ismail Jussa Ladhu akiongea na Waziri wa Fedha, Omar Yussuf Mzee

Mswada wa maslahi ya mafao ya viongozi wa serikali wastaafu ambao umewasilishwa katika kikao cha baraza la wawakilishi umepata pigo baada ya wajumbe waliochangia kuukata na kusema haulengi kuweka usawa wa maslahi ya wananchi walio wengi. Mwakilishi wa jimbo la Mji Mkongwe (CUF) Ismail Jussa Ladhu akichangia mswada huo alisema kwamba umekuja katika wakati ambao haustahiki kwa sababu wananchi wanakabiliwa na hali ngumu ya maisha huku huduma mbali mbali za maendeleo zikiwa duni.

‘Leo tunaleta mswaada huu wakati wananchi wetu wanaishi katika maisha duni sijuwi kama watatuelewa….elimu ipo duni huku mahitaji ya hospitali katika chumba cha wagojwa mahututi (ICU) yakiwa katika mazingira magumu’ alisema Jussa. Alisema yeye binafsi ataupinga mswaada huo kwa sababu haujakidhi mahitaji ya wakati huku huduma za maendeleo zikiwa bado haziridhishi hata kidogo.

Mwakilishi huyo alisema ni vizuri kuwatunza viongozi wastaafu ambao wameleta mchango mkubwa kwa taifa hili kutokana na uongozi busara na hekima zao. Lakini alisema huu si wakati muafaka wa kuwasilisha mswaada huo kwani wananchi wengi matarajio yao katika serikali ya umoja wa kitaifa kuleta mabadiliko makubwa ya uchumi na maisha ambayo hayajafikiwa kwa sasa.

Awali Mwakilishi wa jimbo la Ziwani (CUF) Rashid Seif alisema yeye haungi mkono mswaada huo kwa sababu umelenga zaidi katika kuimarisha hali za viongozi wastaafu wa kisiasa na huku watumishi wa umma wanaostaafu wakikabiliwa na hali ngumu ya maisha.

Alisema ni jambo la busara kuwapatia mafao wastaafu ambao mchango wao kwa taifa ni mkubwa lakini zaidi ilipaswa kuangaliwa hali ya uchumi wa visiwa vya Zanzibar na muelekeo wa uchumi.

‘Hivi sasa tunashindwa kutekeleza miradi mbali mbali ya maendeleo ikiwemo skuli pamoja na kujenga hospitali bora kwa sababu hatuna fedha za kutosha….kwa nini tunataka kutumia fedha nyingi kuwalipa mafao wastaafu pamoja na familia zao?’alihoji Mwakilishi huyo.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Mwinyihaji Makame Mwadini aliwasilisha mswaada wa mafao ya viongozi wastaafu ikiwa unaletwa hapo kwa mara ya pili.

Dk Mwinyihaji aliwaambiya Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kwamba mswada huo umefanyiwa marekebisho makubwa kwa lengo la kukidhi mahitaji ya viongozi hao ambapo sasa tafsiri ya viongozi wa kisiasa imepanuliwa zaidi ambapo wajumbe wa Baraza la Wawakilishi na Mwanasheria Mkuu wa Serikali wameingizwa katika mswaada huo.

Advertisements

6 responses to “Mswaada wa maslahi ya vigogo wapingwa tena

  1. I like this! Hivi ndivo tunavyotaka wawakilishi wafanye kazi. Maslahi ya wengi yaekwe mbele na sio kujali maslahi binafsi kama walivyofanya wabunge wa Bunge la jamhuri. Hiyo ya kuwatambua Wawakilishi na mwanasheria mkuu kua na wao ni viongozi wa kisiasa ambao wanastahiki mafao hayo ni aina mpya ya rushwa inayofanywa na serikali kuwarubuni wawakilishi waukubali mswada huo. Mswada huu ni ufisadi mtupu na hauna sababu yoyote ile ya kupita kama maslahi ya wengi hayajashughulikiwa kwanza.Nadhani Jussa ameelezea vizuri nini maslahi ya walio wengi.

  2. Naunga mkono Wawakilishi walioupinga mswada huo maana maisha ya Wananchi ni mbaya sana hasa vijijini. Pia, sioni sababu ya kutumia Tshs. millioni 700 kwa sherehe za Mapinduzi wakati hayo malengo ya Mapinduzi hayapewi kipao mbele kama Matibabu bora, Elimu n.k

  3. Kama naona kizunguzungu vile?kwa mara ya kwanza wawakilishi mmeweka maslahi
    ya wananchi walio wengi na mliowahagua mbele si kwa kuyafikiria matumbo yenu na
    familia zenu.Hakika mkiendelea hivyo wananchi watawaamini

  4. Ismail Jussa Ladhu pamaoja na wote wanao kuunga mkono… Jitahidini kutuwakilisha sisi tulo wanyonge zaidi na ndo wengi wa Zanzibar, kwanza. M/Mungu atakujazeni kila lenye kheri, kukuongezeeni Elimu na kupanua fikra zenu. jitahidini kutetea maslahi ya wanyonge wenu. na Inshaallah Pepo itakua ndo malipo yenu.

    ZANZIBAR DAIMA!!!

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s