Boko Haram Nigeria

Na Omar Msangi

Wiki iliyopita nilipata ujumbe wa maandishi wa simu (sms) kupitia msomaji. Ujumbe huo ulisema, nanukuu: “Habari za kazi wapendwa, mimi ni msomaji sana wa gazeti lako pamoja na kwamba ni Mkristo. Kuna suala la Boko haram nilitegemea gazeti lako lingeandika habari hizo kwa sababu linakemea uovu, lakini wapi au ni kwa sababu waliouliwa ni Wakristo na wanawalazimisha kuhama wawapishe Waislamu. Uwe mkweli Shehe wangu kwani Uislamu unasema hivyo. Sema kweli hata kama ni mchungu.”
Ujumbe huu ambao niliupata Ijumaa mchana Januari 6, 2012 nadhani mwandishi aliutuma baada ya kusoma makala yangu juu ya Al Shabaab na jinsi baadhi yetu ama kwa ujinga au kutokujua tunavyoshabikia vita dhidi ya Al Shabaab (ugaidi) bila kujua inakotoka na malengo yake.

Kwanza nianze kwa kusema mambo mawili, tunapoandika mambo haya, tunachozingatia ni masilahi ya umma, masilahi ya jamii na masilahi ya binadamu kwa ujumla. Gazeti hili na mwandishi ameandika sana juu ya uharamia uliofanywa na Marekani kule Nicaragua, Chile, Panama, Cuba, El Salvador, Ecuador na Latini Amerika kwa ujumla. Kule wengi ni Wakristo. Tumefanya vile kwa sababu tunachojali ni ubinadamu.

Tumeandika sana pia juu ya Al Shabaab na tatizo la Somalia kwa ujumla, sio kwa kuwatetea Al Shabaab au Waislamu wa Somalia. Ni kwa sababu tunaona kuna udhalimu unafanyika huku ukweli ukifichwa. Kenya, Uganda na Burundi wataumia kwa kutumbukizwa katika mgogoro huu sambamba na wananchi wa Somalia wanavyoumia. Lakini kama nilivyosema katika makala yangu iliyopita, watu wote wa Afrika Mashariki na Afrika kwa ujumla tupo katika hatari kutokana na jinamizi hili jipya la kubuni hiki la Al Shabaab.

Pili, labda nimwambie msomaji kwamba ipo kanuni ya Qur’an inasema kuwa anapokujia mtu na habari, usikimbilie tu kuamnini na kuifanyia kazi, bali chunguza kwanza upate hakika yake. Kinachosemwa hivi sasa ni kwamba Boko Haramu ni kundi la kigaidi la Kiislamu linalouwa Waislamu Nigeria. Katika matukio ya hivi karibuni tunaambiwa kuwa Boko Haramu walishambulia makanisa siku ya Krisimasi na kuuwa takribani watu 50. Baada ya hapo wakashambulia tena na kuuwa watu wengine wapato 20.

Hata hivyo, mara tu baada ya kutolewa madai hayo, msemaji wa Jama’atu Ahlis Sunna Lidda’awati Wal-Jihad (Boko Haram) alitoa taarifa akikanusha kuwa hawajahusika na mashambulizo hayo ya kanisa siku ya Krismasi na mashambulio mengine yote yanayodaiwa kuwa Boko Haram wameuwa Wakristo. Msemaji huyo Abul Qaqa alisema kuwa mauwaji yote dhidi ya Wakristo yanayodaiwa kufanywa na Boko Haram ni uwongo mtupu kwani hakuna Muislamu anayeweza kuuwa mtu asiye na hatia.

Akifafanua zaidi akasema kuwa hata katika mazingira ya vita (Jihad), mpiganaji Muislamu haruhusiwi kuuwa wanawake, watoto, wazee au mtu yeyote asiyeshika silaha. “All Christians in the north should not panic, as Islam prohibits attack in places of worship and it is haram to burn or attack a church even during jihad. Our prophet told us, do not attack the innocent, women, children and the old,” alisema msemaiji huyo kama alivyonukuliwa na waandishi OLAJIDE FASHIKUN na YUSUF OZI-USMAN wa National Accord.

Hata hivyo habari hiyo haikupewa nafasi bali kila uchao vyombo vya habari vimekuwa vikikariri juu ya kuuliwa kwa Wakristo. Na juzi Jumatano BBC na vyombo vingine vya habari vikaja na mtindo ule wa ki-AL Qaida, ikatangazwa kuwa Boko Haram wametoa kanda ya video na kuiweka katika mtandao ambapo inatetea uamuzi wake wa kuuwa Wakristo.
Kwa wanaofuatilia mambo, huu ndio mtindo ulikokuwa ukitumika dhidi ya Usamah Bin Laden na Al Qaidah. Kwamba linafanyika shambulio na habari ya video inatiwa katika mtandao ikidaiwa kuwa msemaji anadhaniwa kuwa msemaji wa Osamah, jambo ambalo huwezi kulithibitisha.
.
Katika ujumla wa mambo jamii ya Wanigeria na walimwengu kwa ujumla tumefikishwa mahali kuamini kuwa Boko Haram ni Waislamu wauwaji. Wauwaji wanaouwa Wakristo wa Nigeria.

Wakati natafiti juu ya kundi hili la Boko Haram, nimekutana na makala moja iliyoandikwa na Profesa Jean Herskovits, ambaye ni profesa wa historia katika Chuo Kikuu cha New York (State University of New York). Katika makala hiyo aliyoipa jina, “Boko Haram Is Not the Problem” ya tarehe 03 Januari, 2012 Prof. Herskovits anasema kuwa, japo huko awali palikuwa na kundi linaloitwa Boko Harama, ambalo kama anavyofahamu yeye lilikuwa na malengo mazuri ya kidini; hivi sasa kunahitajika uangalifu mkubwa katika hizi taarifa zinazotolewa kuwa Boko Haramu wanauwa Wakristo. Anatlia shaka mpaka zile taarifa za kuuliwa Wakristo siku ya Krisimasi.

“…the news media and American policy makers are chasing an elusive and ill-defined threat; there is no proof that a well-organized, ideologically coherent terrorist group called Boko Haram even exists today. Evidence suggests instead that, while the original core of the group remains active, criminal gangs have adopted the name Boko Haram to claim responsibility for attacks when it suits them.”

Anasema Bibie Prof. Herskovits katika makala yake ambayo ilichapishwa na gazeti la New York Times akiitahadharisha serikali ya Obama kwamba (kama haihusiki na ‘mapango’ huu wa Boko Haram), basi ijiepushe na kujiingiza katika hii inayoonekana kuwa vita dhidi ya Wakristo ambayo inalenga kuisambaratisha Nigeria iwe nchi isiyokalika ya vita baina ya Waislamu na Wakristo.
Anasema, kinachofanywa katika mchezo huu ni kujenga picha ionekane kuwa Waislamu wanawapiga Wakristo halafu nchi kama Marekani iingie upande wa serikali ya Goodluck Jonathan, Mkristo, na hapo Waislamu nao hawatakubali, watakuja juu. Nchi itakuwa imesambaratika.

Wasiwasi wa Profesa Herskovits ni kuwa wapo watu katili wakitumiwa na wanasiasa iwe wa ndani au nje ya Nigeria wanaofanya mashambulizi na mauwaji haya kisha hutangaza kuwa waliofanya ni Boko Haram. Anasema, mpaka sasa hakuna anayeweza kumweleza huyo anayejitangaza kama msemaji wa Boko Haram ni nani, bali kinachofanyika ni kunukuu tu taarifa zisizofahamika zimetokea wapi na kisha husambazwa katika vyombo vya habari.

Kinachoshangaza anasema Profesa Herskovits ni ile hali ya serikali ya Marekani na taasisi zake za kijeshi kujiingiza kwa haraka katika suala hili la Boko Haram. Anasema, Agosti mwaka jana kamanda wa Africom Gen. Carter F. Ham, alionya kuwa Boko Haram, wana uhusiano na Al Qaida na kwamba kuanzia hapo ndio mashambulizi ya Boko Haram yakawa yanaongezeka kila uchao.

“Shortly after General Ham’s warning, the United Nations’ headquarters in Abuja was bombed, and simplistic explanations blaming Boko Haram for Nigeria’s mounting security crisis became routine. Someone who claims to be a spokesman for Boko Haram — with a name no one recognizes and whom no one has been able to identify or meet with — has issued threats and statements claiming responsibility for attacks. Remarkably, the Nigerian government and the international news media have simply accepted what he says.”

Anasema Prof. Jean Herskovits akionesha wasiwasi wake juu ya uhusiano huu wa kauli za Africom/Pentagon, kuongezeka kwa mashambulizi na kauli za kulihusisha kundi la Boko Haram ambazo hazifahamiki zinakotokea.
Akifafanua na kuonesha wasiwasi zaidi amesema kuwa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Usalama wa Ndani wa Marekani, (Homeland Security) nayo Novemba mwaka jana ilitoa kauli ikisema kuwa Boko Haram inahatarisha usalama wa ndani wa Marekani, ambacho kinachofuatia ni kikundi hicho kuwekewa mikakati ya kutoka White House na Pentagon kama ile ya Ki-Al qaida na Taliban.

Akielezea historia ya Boko Haram alisema kundi hili lilianza mwaka 2002 kama kikuindi cha Kiislamu kilichokuwa kikifanya shughuli zake kwa amani. Lakini baadhi ya wanasiasa wakaanza kukitumia visivyo. Akasema, hakuna tukio wala ushahidi wowote unaweza kuonesha kwamba Boko Haram waliwahi kufanya shambulio la kuhatarisha amani kabla ya mwaka 2009. Anasema ilikuwa mwaka huo ambapo kiongozi wa kikundi hicho Mohammed Yusuf aliuliwa akiwa mikononi mwa polisi na hakuna hatua zilizochukuliwa.

“Seeking revenge, Boko Haram targeted the police, the military and local politicians — all of them Muslims.”
Kwamba, katika kutaka kulipiza kisasi juu ya ‘Mwembechai’ hiyo, vituo vya polisi vilishambuliwa ambao wote waliolengwa walilengwa kama watumishi wa vyombo vya dola, sio kama Wakristo.

Anachosema Profesa Jean Herskovits ambaye anafundisha katika Chuo Kikuu hichi cha New York, Marekani, ni kuwa hivi sasa jina la Boko Haram linatumiwa na makundi ya kihalifu (na wanasiasa) wenye malengo mabaya na Nigeria.

Akitoa mfano anasema kuwa Idara ya Usalama ya Nigeria Novemba 30, 2011 ilitoa taarifa kwamba imegundua mtandao wa vikundi vinne vya uhalifu (criminal syndicates) ambavyo hutumia jina Boko Haram na kwamba vikundi vitatu katika hivyo vipo Nigeria ya Kusini ya Wakristo. Akaongeza kuwa moja ya vikundi hivyo vya Nigeria Kusini ndio kilituma taarifa ya kitisho kwamba kingeshambulia hoteli za kitalii, na jambo la kuvuta fikra na kutafakari zaidi ni kuwa taarifa za kikundi hicho ndio zilizodakwa na Ubalozi wa Marekani na kutoa onyo kwa raia wake na wageni wengine kuhama maoteli ya kitalii.

“And last week, the security services arrested a Christian southerner wearing northern Muslim garb as he set fire to a church in the Niger Delta. In Nigeria, religious terrorism is not always what it seems.”

Kwamba, ukiacha yote hayo, anasema Profesa Herskovits kuwa wiki iliyopita makachero walimkamata Mkristo mmoja kutoka Kusini akiwa kavaa kanzu na kilemba kama Waislamu wa Kaskazini, Mkristo huyo alikamatwa akichoma moto Kanisa katika Jimbo la Niger Delta. (Kisha husemwa ni Boko Haram.)

Qur’an inasema, “……”
Anachosema Profesa Jean Herskovits ndicho pia anachotahadharisha Gordon Duff, katika makala yake aliyoipa jina “Ngeria: Targeted for destruction? For those who have ears to hear.”

Pamoja na maelezo marefu, Duff ambaye ni afisa wa jeshi la Marekani mstaafu anasema kuwa kinachofanyika sasa hivi chini ya Boko Haram ni maandalizi na mkakati wa kuiangamiza Nigeria kama ilivyoangamizwa Afghanistan. Anasema, hatma ya hali iliyopo hivi sasa Nigeria ni kupatiwa msaada wa kudumu wa kukaliwa kijeshi na Marekani ili kuhakikisha kuwa uporaji wa mafuta ya nchi hiyo unakwenda vizuri.

Anasema, Wakristo watapumbazwa kuwa adui yao ni Waislamu hivyo lazima wapambane nao, lakini mwisho wa yote wote watakuwa watumwa na watumishi wa wale watakaowaletea drone na helkopta za kijeshi. Gordon Duff anasema kuwa mkakati wa kutumia Boko Harama unafanikiwa kwa wepesi kutokana na ufisadi ulioshamiri Nigeria kwa vile inakuwa rahisi kuwatumia wanasiasa na maofisa wa jeshi, polisi na idara za usalama.

Anasema, sio muda mrefu Nigeria itakuwa uwanja mwingine wa kujidai wa drone za Marekani na hapo Africom itakuwa imepata sababu na kisingizio cha kuwepo. “Soon Nigeria will enjoy the sight of armed UAVs, piloted from, just perhaps, Tel Aviv, theoretically there to punish terrorists. Pakistan will explain it to you if you care to listen.” Anasema Gordon akiwatahadharisha Wanigeria.

“UAV attacks are how terrorists are recruited, how wars are instigated and how the disjointed and unsettled are turned into an enemy camp. The presentations have been made and the purchase orders await only the promised “backhanders” or as we call it here, “kickbacks” to be executed.” Anasema zaidi Gordon Duff akionya.

Naye mwandishi Nile Bowie katika makala yake, “Lagos Dissents under IMF Hegemony: Nigeria Next Front for AFRICOM” (January 08, 2012), anasema kuwa maandamano yanayoendelea Nigeria juu ya kupanda kwa bei ya mafuta na suala la Boko Haram, kwa pamoja yanatoa kisingizio kizuri kwa AFRICOM (Marekani) kuingia Nigeria.

Anasema, si muda mrefu, nchi hiyo itakuwa imeungana na Uganda na Eritrea kuwa na kambi za kijeshi za Marekani kwa kisingizio cha kusaidia kulinda usalama wa nchi. Nile akifafanua hoja zake anasema kuwa kupandisha bei ya mafuta ni mkenge ilioingizwa Nigeria kutoka mipango ya IMF huku wenyewe IMF na wenye IMF yao wakijua wazi kuwa ushauri huo wa kuondoa ruzuku ya mafuta katika ule makakati mzima wa kigonjwa wa ‘Structural Adjustment Policies (SAP), lazima uitie Nigeria katika machafuko kama ilivyotokea kwa nchi za Asia mwaka 1997. (Kwa wanaojua Kiingereza soma makala ya Nile Bowie uk. 9)

Nimalizie kwa kusema kuwa hivi sasa Rais Goodluck Jonathan anashutumiwa kuwa kawa kibaraka wa Marekani aliyepitiliza mipaka. Inadaiwa kuwa hata hotuba yake ya hivi karibuni ya siku ya uhuru wa Nigeria iliandikwa Marekani au kama iliandikwa ndani ya Nigeria, basi aliyeiandika ni Mmarekani.

Wachunguzi na wachambuzi wameichambua hotuba hiyo kifungu kwa kifungu na kuonesha vifungu ambavyo ni maarufu katika hotuba za Marais wa Marekani. Kwamba hotuba nzima inaonekana kana kwamba Rais Goodluck Jonathan anawahutubia Wamarekani.

Mmoja wa watu wa karibu na Rais Jonathan alipoulizwa juu ya hali hiyo ya ukibaraka unaochefua, alijibu kwa kifupi tu kwamba: ambaye hataki kusikia la Marekani, atizame alichofanywa Gaddafi. Si hivyo tu, lakini wachunguzi wa mambo wanasema kuwa Rais Jonathan ashafikishwa mahali ambapo haamini kabisa vyombo vyake vya usalama.
Kwa ushauri anaopewa na Washington, hivi sasa analipa kiasi cha dola milioni 100 kila mwezi kuwalipa FBI na Mossad kwa ajili ya ulinzi wake.

“The president has no option than to bring in the FBI, CIA, Israeli MOSSAD, no matter what it will cost the nation, the president’s security and the first family and presidency is first and foremost the most important…”, ananukuliwa afisa mmoja wa serikali.

Hata hivyo kuonesha kuwa hayo hayakuwa maamuzi ya hiyari ya serikali ya Nigeria, afisa huyo alipoulizwa kuwa haoni kuwa gharama hiyo ni kubwa sana ya kuitia umasikini nchi alijibu:
“You cannot fight America, go and ask Muammar Gaddafi Libya, how about Saddam Hussein of Iraq; my friend, the international and local chase game, is new game-changer, you either be on the winning side or get annihilated”.

Majibu haya wakati swali lilikuwa la gharama kuwa kubwa, inaonesha kuwa Rais Jonathan alifanywa kuona kuwa vyombo vyake vya usalama havina maana na badala yake akatakiwa kuwategea FBI, CIA na Mossa kwa gharama kubwa.
Inapokuwa CIA na Mossad ndio wamekabidhiwa jukumu la usalama wa Rais na usalama wan chi, hapana shaka taarifa za Boko Haram zitazidi kunonga na kupamba kurasa za magazeti.

Alijisemea mwandishi mmoja, “..the question is what-else is left of what is called Nigeria at 51st Independence Anniversary? Absolutely nothing!” Aliyasema haya akihoji kuwa kama Nigeria imefikia mahali pa kukabidhi usalama wake kwa FBI na hotuba ya Rais kuandikwa kutoka Washington, kuna kilichosalia tena katika nchi hiyo?

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s