Huduma ya maji Kiuyu Pemba

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akizungumza baada ya kufungua mradi wa maji wa Kiuyu na Maziwang’ombe katika Wilaya ya Micheweni.Wengine kutoka kulia ni Waziri wa Mifugo na Uvuvi Said Ali Mbarouk na Waziri wa Ardhi, Makaazi, Maji na Nishati Ali Juma Shamuhuna, na kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba, Dadi Faki Dadi, na Naibu waziri wa Ardhi, Makaazi, Haji Mwadini Makame

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad amesema kuimarika kwa miundombinu katika Wilaya ya Micheweni kutalifanya eneo hilo kutimiza azma ya serikali ya kulifanya kuwa eneo huru la kiuchumi. Amesema wawekezaji watavutiwa zaidi kuwekeza vitega uchumi vyao ikiwa watahakikishiwa upatikanaji wa huduma muhimu zikiwemo maji, barabara na umeme.
Makamu wa Kwanza wa Rais alieleza hayo jana huko Micheweni Pemba baada ya kufungua mradi wa maji wa Kiuyu na Maziwang’ombe, ikiwa ni katika shamrashamra za maadhimisho ya miaka 48 ya Mapinduzi ya Zanzibar. Maalim Seif ameitaka Wizara ya Ardhi, Makaazi, Maji na Nishati kuutunza mradi huo na kuhakikisha kuwa huduma hiyo inawafikia wananchi kwa wakati wote.

Kwa upande wake Waziri wa Wizara hiyo Mhe. Ali Juma Shamuhuna amesema kufunguliwa kwa mradi huo katika Wilaya ya Micheweni kunathibitisha nia ya serikali kuwakomboa wananchi wa maeneo yote ya Unguja na Pemba.

Mradi huo uliosimamiwa na kujengwa na mafundi wazalendo wa Mamlaka ya maji Zanzibar (ZAWA) kwa kushirikiana na mafundi wa Idara ya Ujenzi umetekelezwa kwa pamoja kati ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Mashirika ya Umoja wa Mataifa, na umegharimu zaidi ya shilingi milioni mia tano.

Wakati huo huo Makamu wa Kwanza wa Rais Maalim Seif Sharif Hamad ameitembelea na kuifariji familia iliyofikwa na msiba mkubwa uliotokana na kula kasa katika kijiji cha Tumbe Wilaya ya Micheweni. Katika msiba huo watu wanane wakiwemo saba wa familia moja walifariki dunia hivi karibuni, wengi wao wakiwa ni watoto. Ameitaka familia hiyo kuwa na subra katika kipindi hiki kigumu cha msiba na kuwaombea marehemu makazi mema Peponi.

Habari na Hassan Hamad, Picha na Salmin Said (OMKR)

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s